Kwa hili la Wafanyakazi wa Ndani, Serikali inakosea sana

Una hoja ya kimsingi SANA, mf., mshahara wa 40'000 kwa mwezi kiukweli haotoshi kabisa- Huu ni utumwa uliokithiri. Kufanya kazi isiyo na maslahi bora wala ukomo wa muda wa kazi kwa siku yahitaji moyo wa ki-MUNGU. Hawa wadada wataendelea sana kuwa makatili endapo waajiri wao wasipo watengenezea maslahi bora na kujaliwa kwa dhati- Hakuna shortcut kwenye hili

Kula , kuvaa .,matibabu ,kulala ,na mengineyo apewe 250k sio? Wakati Kima cha chini napokea 260k Acha kukurupuka mzee mzima
 
Imebidi ni~log in ili kuweka mawazo yangu kwenye uzi huu: bongo kuna kawaida ya kutatua changamoto bila kufikiria kwa kina(ref: uamuzi wa watawala kupandisha bei ya mafuta ya taa ili ikaribiane na ya diesel ili kuzuia uchakachuaji!).
Si sawa mdada wa kazi kufanya kazi hadi usiku wa manane, lakini sikubaliani na wenye mtazamo kuwa elfu 30, 40 ni ndogo!
Mimi huwa naichukulia kuwa ni hela anayoweza kuweka akiba baada ya matumizi yote ya lazima....
Malazi, chakula, mavazi, matibabu, hadi kwa wengine nauli ya kwenda kwa wazazi wake na kurudi ni juu ya mwajiri. Nakumbuka home madada wa ndani walikuwa ndio watumiaji wakubwa wa tv kuliko wanafamilia. Familia nyingi mno zina wasaidizi wa ndani wanaoishi nao kawaida mno. Tatizo kubwa ni kuwa kwa wengi wanakuwa kwenye ule umri wa mabadiliko ambao hata watoto wa familia tu ni pasua kichwa!
Hivi hili wazi la wasaidizi wa ndani kulipwa tuseme laki mbili ni ili akapange na kujitegemea wakati wengi wao kiumri wanatakiwa kuwa chini ya malezi au ni vipi?!
 
Kuna watu wanakurupuka hawajui na wala hawajawahi kupata kadhia za hawa mabinti wa kazi...aloo mwingine hata umchkulie vipi kama mwanafamilia atakutenda tu na hard haridhiki.. nmeishi na binti vizuri kabisa kuanzia kusuka kwake nguo za ndani ziwezi nunua nguo za wanangu bila kumletea na nayeye,bites nlirudi jioni nkiletea wanangu na yeye pia ,viatu achilia mbali hela za vocha sijawahi mcheleweshea mshahara nliongeza zaidi mshahara tulikubaliana still alikaa miezi saba tu nkaona anataka usawa,kazi akifanya anataka na mm nifanye..alijua sina jeuri yayakumuondoa kwa kuwa nlimpenda na alipenda watoto..kazi nimuelekeze up upya kama mgeni jeuri kiburi simu kumzuzua kapata wajanja mtaani wkampa somo kalielewa mimba kapata skuwa na namna nkamuondoa..nimeibiwa sana na kukamata wadada sina ham nao
 
Kupitia au kutopitia haku-justify wafanyakazi watumikishwe kama punda, at the end of the day ni binadamu na wanastahili kupewa haki zao na hali bora kwenye ofisi zao. Ni vyema serikali kutengeneza a fair working environment na good standards.
 
Mtu anayemlipa mfanyakazi 30K acha tu atendewe ubaya,hata sense ya kawaida tu hiyo siyo pesa ya kuthubutu kumsubirisha nayo mtu hata kama ni maskini kiasi gani!
Hujafikia kiwango chao cha umaskini ndgu yangu.
Mpaka mtu anakubali hiyo pesa jua ana hali mbaya, na hiyo ni kwa sababu ni kula na kulala bure.
Mkuu hata sasa hivi ukipost tangazo hapa jf useme unataka mfanya kazi utamlipa 30k na kula na kulala bure, utaona kama sio chini ya watu 10 hawajakufata pm kuulizia hiyo fursa.
 
Duh, mtu unamlipa 30000 halafu anafanya kazi zote wa kwanza kuamka wa mwisho kulala, sio haki.
Ndo ivo lakini kuondoa hili kwa serikali yetu hii bado saana yaani bado mno.

Umaskini ni mkubwa sana nchi hii kuliko jinsi watu wanavyodhani.

Just imagine mtu anakupa mwanae akusaidie kazi na hata usimlipe aje tu aishi kwako coz uhakika wa kula na kulala upo!! Ni kweli sio utani huu mkuu

Sasa fikiria mzazi anaona kumlisha tu huyo mtoto hiyo gharama haiwezi, haya sasa mwanae haishi bure unamlipa na ka30k, huyo mzee atasema mwanae ardi kwake???
 
Una hoja ya kimsingi SANA, mf., mshahara wa 40'000 kwa mwezi kiukweli haotoshi kabisa- Huu ni utumwa uliokithiri. Kufanya kazi isiyo na maslahi bora wala ukomo wa muda wa kazi kwa siku yahitaji moyo wa ki-MUNGU. Hawa wadada wataendelea sana kuwa makatili endapo waajiri wao wasipo watengenezea maslahi bora na kujaliwa kwa dhati- Hakuna shortcut kwenye hili
Umewahi kusikia watu wakubwa Serikalini au Madaktari au manesi au askari wa maliasili au Wafanyabiashara wameua watu kinyume na taratibu za kazi ? Kama ndio , je, ni maadili au sababu ya mishahara? Mbona Ukifika benki Kuna askari wanalinda mabilion na kulala nje ya nyumba zao lakini wanalipwa kidogo ukilinganisha na wanacholinda?

Dunia Kwa Sasa imejaa watu waliojaa uchungu mioyoni mwao?
Nani aliyekuambuia kuwa maskini ndio wauajji ?
Juzi Kuna mtu kaua mkewe na yeye kujiua ishu sio pesa Bali mapenzi.

Wakina mama wengi ni wakorofi Kwa wadada wa kazi bila sababu mara nyingine kuwatuhumu kuwa wanawachukulia mabwana zao. Lakini pia wanaume wengine wanatembea na wadada wa kazi ,jambo linalowafanya wawadharau wakina mama na watoto wao. Lakini wapo wadada vichaa wenye matatizo ya akili kuanzia majumbani kwao walikotoa, wengine ni washirkina , wengine Wana hasira kupita kiasi. Hizo ni tabia mbaya za binadam
 
Wafanyakazi kwenye baadhi ya familia unakuta wananyimwa chakula, hawapewi nafasi ya kulala inavyostahili, hawalipwi mshahara bora, wanapigwa, wanachomwa, hawaruhusiwi kujumuika na wengine katika familia, wanafanyiwa ukatili wa kijinsia- unategemea wanakuja kuleta matokeo gani kwenye jamii zaid ya wao kuja kuwa na watukio ya ajabu? and at the same time wafanyakazi wengi wa majumbani ni watoto wadogo wengine mpaka 12 years
 
Tuanze kwako tukiachana na unafiki, unaweza kutoa 250k kwa mfanyakazi wa ndani ?

Cha msingi kinachotakiwa ni kuishi nao vizuri Sana pia wachukulie Kama wanao au wadogo zako, wape amani muda wote Sasa kinachofanyika wafanyakazi hao wanateswa na kunyanyaswa, wanakosa amani muda wote ni masimango na kutukanwa, hapo unategemea nn?
Mfanyakazi wa kima cha chini serikalini...

Anapanga chumba/nyumba
Anajitegemea kwenye chakula/usafiri
Analipa bill ya maji/umeme
Anasomesha watoto
Anasaidia wazazi

Atapata wapi 250K ya kumlipa housegirl

Watu wanasahau housegilrL anakula bure, analala bure, anatibiwa na kupata huduma za kijamii bure. Hiyo 50K anaweza kuitunza yote na kujipatia mtaji wa kuanzia biashara ndogo ndani ya mwaka mmoja
 
Inategemea mtu na mtu. Kuna house girls pasua kichwa tangu day one anaingia ndani ya nyumba japo atakuta wenye nyumba ni wastaarabu.

Na kuna House girls wanakuwa wastaarabu sn na wavumilivu lkn wanakuta wenye nyumba ndio Sio wastaarabu, watesaji n.k.

Ni kuomba Mungu kwa sana tu. Mwenye nyumba ukiwa Sio mtu wa kutesa wafanyakazi basi Mungu Akujaalie mstaarabu mwenzio na ikitokea kataka kuondoka basi aondoke kwa salama na Amani na Sio aache madhara.

Wasichana wengi wa kazi wanakuwa kwenye ile age ya pasua kichwa na akili zao bado hazijapevuka.

Ila sisapoti msichana wa kazi kulipwa 30/40K kwa maisha ya sasa. Hata kama mahitaji mengine muhimu anapata hapo kwako
 
Kumbuka wapo watu wanaolipwa 150,000 na sio house girl lakini wanajitegemea Kila kitu, usafiri, kula, chumba nk. Msichukulie Mambo poa. Nenda tu viwanda vya wachina na wahindi uulizie wafanyakazi wa chini wanalipwa kiasi gan na wanajitegemea Kila kitu
 
Mnapojadili ni vema kuzingatia ukubwa wa familia.

Kuna familia nyingine house girl akishafanya usafi asubuhi atashinda kutwa nzima hana kazi hadi jioni ndio apike chakula cha jioni.

Mchana ni kulala na kuangalia TV tu.

Sasa wa hivyo utamlipa shilingi 100,000/- ?
 
Pia zingatieni kuwa house girls anakaa kwenye familia anayofanya kazi.

Iwapo angefanya Kwa mhindi au familia zenye uwezo angekuwa anaenda asubuhi na kurudi jioni ,

Hapo angeyakiwa apange chumba lakini anakaa nyumbani anajifanya kazi,

Kwa hiyo mwenye kukaa na yaya iwapo analala chumba chake peke yake inabidi kukithaminisha iwapo angepanga mtaani angelipa shilingi ngapi ?

Akiumwa anatibiwa,

Chakula anachokula asubuhi mchana na jioni, unajua mfanyakazi wa serikali wa kina cha chini huwa anajitegemea chakula ?!

Lakini yaya anakula milo yote anakofanya kazi,

Je tuithaminishe?

Sabuni anayoogea na kufulia nguo zake,

Mafuta ya kupaka,

N.k

Ukithaminisha hivyo vyote utakuta pesa yake ni nyingi.
 
Yupo mmoja alimtia kid wa mwenye nyumba aged 6½month kwenye fridge akakimbia mwenye nyumba kurudi akakuta nyumba nyeupe akaenda kutoa taarifa polisi amerudi anasema ngoja ninywe maji ya baridi kufungua fridge akakuta mwanae ameshakufa.

Zipo pia case za watoto kupigishwa deki kwenye nyuchi za hawa mahaus gel wazazi wawapo makazini unamlipa mshahara vizuri ukijua hatamdhuru kumbe anamtia mtoto cancer ya koo.
So sad
 
Pia zingatieni kuwa house girls anakaa kwenye familia anayofanya kazi.

Iwapo angefanya Kwa mhindi au familia zenye uwezo angekuwa anaenda asubuhi na kurudi jioni ,

Hapo angeyakiwa apange chumba lakini anakaa nyumbani anajifanya kazi,

Kwa hiyo mwenye kukaa na yaya iwapo analala chumba chake peke yake inabidi kukithaminisha iwapo angepanga mtaani angelipa shilingi ngapi ?

Akiumwa anatibiwa,

Chakula anachokula asubuhi mchana na jioni, unajua mfanyakazi wa serikali wa kina cha chini huwa anajitegemea chakula ?!

Lakini yaya anakula milo yote anakofanya kazi,

Je tuithaminishe?

Sabuni anayoogea na kufulia nguo zake,

Mafuta ya kupaka,

N.k

Ukithaminisha hivyo vyote utakuta pesa yake ni nyingi.
Lakini sio kwa kulipa 30k
 
Habari wana JF

Kumekuwa na uwepo wa matukio ya kikatili na Unyanyasaji yanayofanywa na watoto /mabinti wanaoitwa wafanyakazi wa ndani

Nimekaa nikawaza sana, binafsi sikuoni kosa la hawa mabinti ila Serikali ndio inafanya siasa inayoharibu kizazi hiki na Kijacho. Kwa kifupi hawa watoto ni watu waliopigwa na Maisha.

Kuna vitu viwili Serikali ingefanya kuweza Kusaidia hawa Watoto na Jamii kwa Ujumla :-
  1. Hii ajira ya wafanyakazi wa Ndani ilasimishwe. Hapa pawekwe kima cha Chini cha Kueleweka mfano 250K. Umri uzingatiwe na Watu wasaini mikataba na asiruhusiwe kukaa mtu na mtu wa kazi bila Mkataba hii itafanya hii ajira isiwe ya watu waliopigwa Maisha na itaboresha ufanisi katika Ajira hii. Ni ukweli kwamba hawa watoto wananyanyaswa pia na Hawalipwi. Hii Ajira haijakaa sawa kabisa, hivi Mtu anae ingiza kipato cha chini ya 500K anawezaje mmiliki mfanyakazi wa Ndani? Atamlipa nini? Zaidi ya kumzungusha tu
  2. Hawa Mabinti/watoto Wanahitaji kusaidiwa kimaisha na kimatibabu. Kwa nature ya hii ajira ilivyo hakuna mzazi yeyote anaeweza mtoa mtoto wake akamfanyie kazi za ndani mzazi mwingine. Hivyo ni ajira ya Watoto waliotelekezwa, waliopigwa na maisha, waliotoroka kuja mjini etc .. Kwa kifupi ni watoto walio kwenye maisha Magumu na wengi wao tayari athari ya Afya ya akiri hasa PTSD -post traumatic stress disorders. Hivyo ni group la watoto Serikali inabidi liangaliwe kwa jicho tofauti sio ajira za Ndani.
Hawa watoto haya matukio wanayofanya na matokeo ya maisha waliyo ishi huko Nyuma wengine wanahitaji Matibabu.

Huwezi kusimamisha ajira.. kuna watu ni madaktari wana appointment za kufanyia wagonjwa upasuaji. Huo upasuaji utaufanya wewe? Usifikirie kama bata fikiria kama binadamu . Baba yako hakupoteza pesa kukusomesha ili uweke akili yako uvunguni
 
Back
Top Bottom