Kwa hili la Wafanyakazi wa Ndani, Serikali inakosea sana

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari wana JF

Kumekuwa na uwepo wa matukio ya kikatili na Unyanyasaji yanayofanywa na watoto /mabinti wanaoitwa wafanyakazi wa ndani

Nimekaa nikawaza sana, binafsi sikuoni kosa la hawa mabinti ila Serikali ndio inafanya siasa inayoharibu kizazi hiki na Kijacho. Kwa kifupi hawa watoto ni watu waliopigwa na Maisha.

Kuna vitu viwili Serikali ingefanya kuweza Kusaidia hawa Watoto na Jamii kwa Ujumla :-
  1. Hii ajira ya wafanyakazi wa Ndani ilasimishwe. Hapa pawekwe kima cha Chini cha Kueleweka mfano 250K. Umri uzingatiwe na Watu wasaini mikataba na asiruhusiwe kukaa mtu na mtu wa kazi bila Mkataba hii itafanya hii ajira isiwe ya watu waliopigwa Maisha na itaboresha ufanisi katika Ajira hii. Ni ukweli kwamba hawa watoto wananyanyaswa pia na Hawalipwi. Hii Ajira haijakaa sawa kabisa, hivi Mtu anae ingiza kipato cha chini ya 500K anawezaje mmiliki mfanyakazi wa Ndani? Atamlipa nini? Zaidi ya kumzungusha tu
  2. Hawa Mabinti/watoto Wanahitaji kusaidiwa kimaisha na kimatibabu. Kwa nature ya hii ajira ilivyo hakuna mzazi yeyote anaeweza mtoa mtoto wake akamfanyie kazi za ndani mzazi mwingine. Hivyo ni ajira ya Watoto waliotelekezwa, waliopigwa na maisha, waliotoroka kuja mjini etc .. Kwa kifupi ni watoto walio kwenye maisha Magumu na wengi wao tayari athari ya Afya ya akiri hasa PTSD -post traumatic stress disorders. Hivyo ni group la watoto Serikali inabidi liangaliwe kwa jicho tofauti sio ajira za Ndani.
Hawa watoto haya matukio wanayofanya na matokeo ya maisha waliyo ishi huko Nyuma wengine wanahitaji Matibabu.
 
Una hoja ya kimsingi SANA, mf., mshahara wa 40'000 kwa mwezi kiukweli haotoshi kabisa- Huu ni utumwa uliokithiri. Kufanya kazi isiyo na maslahi bora wala ukomo wa muda wa kazi kwa siku yahitaji moyo wa ki-MUNGU. Hawa wadada wataendelea sana kuwa makatili endapo waajiri wao wasipo watengenezea maslahi bora na kujaliwa kwa dhati- Hakuna shortcut kwenye hili
 
Ni hatari sana
 
Mkuu ulishawahi kuishi na hawa wasichana, ukazijua walau kidogo familia wanazotokea??
Hapo serikali unailaumu bure tu, kwani unadhani hiyo ajira sio rasmi. Kwa hao viongozi na watu wenye wadhfa kuna wadada wa ndani wanaolipwa hiyo mishahara.

Ila huku kwetu huku eti iwekwe sheria strictly kabisa walipwe zaidi ya laki aisee utaibua tatizo jingine la biashara ya binadamu.
Ujue hawa wadada mara nyingi huwa wanachukuliwa vijijini huko, ambako sh. 10k ni kubwa mno, kiasi kwamba akilipwa hiyo 30k mzazi akatumiwa yote au akakaa miez 2 akatumiwa 50k, sio rahisi kumshawish eti mwane aondoke huko anakofanya kaz.

Tatizo kubwa ni umaskini ndgu yangu, kimjini mjini wanalipwa elfu 30 kwa mwezi, pesa ndogo mnoo lakini kwa familia walizotokea ni pesa nzuri kwao, hawataki kuacha, mzazi wake hataki aache. Kuna dada aliambiwa na baba yake ukirudi nyumbani basi sisi sio wazazi wako. Sasa kwa umri wao na hayo maneno sio rahisi kusepa.
 
Mkuu hii ajira inabidi ilasimishwe na waajiriwe walipwe pesa ya kutosha otherwise tutaendelea kuona mengi na serikali iangalie namna ya kuwasaidia hao watoto .
 
Tuanze kwako tukiachana na unafiki, unaweza kutoa 250k kwa mfanyakazi wa ndani ?

Cha msingi kinachotakiwa ni kuishi nao vizuri Sana pia wachukulie Kama wanao au wadogo zako, wape amani muda wote Sasa kinachofanyika wafanyakazi hao wanateswa na kunyanyaswa, wanakosa amani muda wote ni masimango na kutukanwa, hapo unategemea nn?
 
250,000 per month that's impossible kwa dada wa kazi na majukumu yanatofautiana familia Moja Hadi nyingine.

Kubwa wanaMAMA punguzeni midomo kutwa gubu mtoto wa watu hujawahi hata kumwonyesha sura ya tabasamu Kila kitu ni malalamiko+ unamtreat kama sio part ya familia, magubu yenu ya kutaka uperfection mtaendelea kuona mengi kutoka kwa hao wadada wa kazi mnaona hiyo 50k mnayowalipa ni nyingi.

Money can't buy everything,
Humanity comes first
 
Kuna watu ni very insane, unakuta kwenye baadhi ya familia dada wa kazi analala saa 7 usiku na kuamka saa 10 alfajiri, sasa huyu si anakuwa punda? 🤣 🤣 🤣 . Matukio hayatoisha unless waajiri na wenyewe waanze kubadilika- Kuna familia unakuta mwajiri ni very exceptional, anasomesha hadi wafanyakazi wa ndani na kuwapatia muda wa kutosha wa mapumziko which is very rare.
 
Nakubaliana na wewe kwamba maslahi yao ni madogo. Lakini natofautiana hapo kwamba ndio chanzo Cha ukatili na unyama. Ndio maana wapo wanaolipwa kidogo na hawatathubutu kufanyia mtoto ukatili na wapo wanaofanya unyama Kwa watoto bila kujali maslahi.

Kama ambavyo wanawake wanauwawa na wanaume katili au wanawake wachache wananyanyasa waume zao.

Hawa watu unawezamchukulia kama mwanafamilia akakutenda, ukashangaa sehem ananyanyaswa haruhusiwi hata kuketi sebuleni au kula na familia na Bado ana utii na unyenyekevu wa hatari.
 
Unajua Kuna watu wanapokea huo mshahara wa 250k Sasa akitakiwa kulipa hiyo si atajikuta anamfanyia kazi house girl. Halafu wengine maisha yakwao mlo tu shida kwahiyo wengine kula tu ni mshahara tosha + hiyo 25/40 kwake muruuua kabisa
 
Tuanze kwako tukiachana na unafiki, unaweza kutoa 250k kwa mfanyakazi wa ndani ?

Cha msingi kinachotakiwa ni kuishi nao vizuri Sana pia wachukulie Kama wanao au wadogo zako, wape amani muda wote Sasa kinachofanyika wafanyakazi hao wanateswa na kunyanyaswa, wanakosa amani muda wote ni masimango na kutukanwa, hapo unategemea nn?
Hakuna TANZANIA mtu ampae dada wa Kazi 250 hata Waziri halipi sana Sana atampa 80 au laki.
 
Nakubaliana na wewe kwamba maslahi yao ni madogo. Lakini natofautiana hapo kwamba ndio chanzo Cha ukatili na unyama. Ndio maana wapo wanaolipwa kidogo na hawatasubutu kufanyia mtoto ukatili na wapo wanaofanya unyama Kwa watoto bila kujali maslahi.

Kama ambavyo wanawake wanauwawa na wanaume katili au wanawake wachache wananyanyasa waume zao.

Hawa watu unawezamchukulia kama mwanafamilia akakutenda, ukashangaa sehem ananyanyaswa haruhusiwi hata kuketi sebuleni au kula na familia na Bado ana utii na unyenyekevu wa hatari.
Ukatili ni tabia hautokani na kipato wapo waliolipwa vizuri na kufanyiwa wema wote lakini wakaishia kuwafanyia ukatili mabosi zao
 
Hapa ndipo ushangaa serikali kuzuia mabinti wasiende uarabuni kufanya Kazi eti wananyanyasika, kwani hapa nchini awanyanyasiki?.
Popote alipo mwanamke atamnyanyasa mwanamke mwenzake, labda angalau Ulaya kule angalau Wana utu na Sheria kali zinazowalinda madada wa Kazi.
 
Hawa watoto haya matukio wanayofanya na matokeo ya maisha waliyo ishi huko Nyuma wengine wanahitaji Matibabu
Matibabu ya akili na vipimo vya mara kwa mara vya akili kama ilivyo kwa marubani ni muhimu
 
Kuna watu ni very insane, unakuta kwenye baadhi ya familia dada wa kazi analala saa 7 usiku na kuamka saa 10 alfajiri, sasa huyu si anakuwa punda? 🤣 🤣 🤣 . Matukio hayatoisha unless waajiri na wenyewe waanze kubadilika- Kuna familia unakuta mwajiri ni very exceptional, anasomesha hadi wafanyakazi wa ndani na kuwapatia muda wa kutosha wa mapumziko which is very rare.
Kuna manyanyaso mengi sana chini ya kapeti na wanayavumilia
 
Mkuu ulishawahi kuishi na hawa wasichana, ukazijua walau kidogo familia wanazotokea??
Hapo serikali unailaumu bure tu, kwani unadhani hiyo ajira sio rasmi. Kwa hao viongozi na watu wenye wadhfa kuna wadada wa ndani wanaolipwa hiyo mishahara.

Ila huku kwetu huku eti iwekwe sheria strictly kabisa walipwe zaidi ya laki aisee utaibua tatizo jingine la biashara ya binadamu.
Ujue hawa wadada mara nyingi huwa wanachukuliwa vijijini huko, ambako sh. 10k ni kubwa mno, kiasi kwamba akilipwa hiyo 30k mzazi akatumiwa yote au akakaa miez 2 akatumiwa 50k, sio rahisi kumshawish eti mwane aondoke huko anakofanya kaz.

Tatizo kubwa ni umaskini ndgu yangu, kimjini mjini wanalipwa elfu 30 kwa mwezi, pesa ndogo mnoo lakini kwa familia walizotokea ni pesa nzuri kwao, hawataki kuacha, mzazi wake hataki aache. Kuna dada aliambiwa na baba yake ukirudi nyumbani basi sisi sio wazazi wako. Sasa kwa umri wao na hayo maneno sio rahisi kusepa.
Duh, mtu unamlipa 30000 halafu anafanya kazi zote wa kwanza kuamka wa mwisho kulala, sio haki.
 
Mkuu ulishawahi kuishi na hawa wasichana, ukazijua walau kidogo familia wanazotokea??
Hapo serikali unailaumu bure tu, kwani unadhani hiyo ajira sio rasmi. Kwa hao viongozi na watu wenye wadhfa kuna wadada wa ndani wanaolipwa hiyo mishahara.

Ila huku kwetu huku eti iwekwe sheria strictly kabisa walipwe zaidi ya laki aisee utaibua tatizo jingine la biashara ya binadamu.
Ujue hawa wadada mara nyingi huwa wanachukuliwa vijijini huko, ambako sh. 10k ni kubwa mno, kiasi kwamba akilipwa hiyo 30k mzazi akatumiwa yote au akakaa miez 2 akatumiwa 50k, sio rahisi kumshawish eti mwane aondoke huko anakofanya kaz.

Tatizo kubwa ni umaskini ndgu yangu, kimjini mjini wanalipwa elfu 30 kwa mwezi, pesa ndogo mnoo lakini kwa familia walizotokea ni pesa nzuri kwao, hawataki kuacha, mzazi wake hataki aache. Kuna dada aliambiwa na baba yake ukirudi nyumbani basi sisi sio wazazi wako. Sasa kwa umri wao na hayo maneno sio rahisi kusepa.
Mtu anayemlipa mfanyakazi 30K acha tu atendewe ubaya,hata sense ya kawaida tu hiyo siyo pesa ya kuthubutu kumsubirisha nayo mtu hata kama ni maskini kiasi gani!
 
Yupo mmoja alimtia kid wa mwenye nyumba aged 6½month kwenye fridge akakimbia mwenye nyumba kurudi akakuta nyumba nyeupe akaenda kutoa taarifa polisi amerudi anasema ngoja ninywe maji ya baridi kufungua fridge akakuta mwanae ameshakufa.

Zipo pia case za watoto kupigishwa deki kwenye nyuchi za hawa mahaus gel wazazi wawapo makazini unamlipa mshahara vizuri ukijua hatamdhuru kumbe anamtia mtoto cancer ya koo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom