Wanitakiani
JF-Expert Member
- Apr 18, 2008
- 641
- 135
Bw. John Pombe Magufuli amekosea! Tumesikia mabadiliko yaliyotokea katika Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuondolewa kwa CEO wake Bw. Makumba Kimweri na kupelekwa Wizarani.
Magufuli amejizolea sifa nyingi miongoni mwa watz kama kiongozi mzuri na mchapakazi hasa kwa staili yake anayoitumia ya ufuatiliaji na udikteta. Kwani wakati mwingine sifa hiyo ni nzuri, lkn kuna nyakati inaweza pia kuleta madhara kwa sababu haizingatii utawala wa sheria (rule of law).
Magufuli kwa waliofanya naye kazi kwa karibu wanaweza kukupa story tofauti na usiweze kuamini kama huyu ndiye yule Magufuli anayepambanuliwa miongoni mwa viongozi wengi kuwa ni muadilifu. La hasha! Magufuli hayupo hivyo, ni mnafiki anayevaa ngozi ya kondoo kuwahadaa Watz. Ni fisadi na mpenda majungu kupita kiasi.
Magufuli anaweza kufanyia kazi hearsay as if amepewa taarifa za kweli na zilizothibitishwa, inategemea nani kawahi kumpa majungu na ni nani kwake.
Kuondolewa kwa Mkurugenzi mkuu wa TBA Bw. Kimweri kulianza kama mchezo. Chokochoko ilianzia kwa mtumishi mmoja wa idara ya uhasibu Bw. Kapongo ambaye ni jamaa yake Magufuli, wengine wanasema ni mjomba wake alipopewa uhamisho kwenda Wizarani baada ya kuwepo kutoelewana na wafanyakazi wenzie.
Kapongo alipopata barua ya uhamisho alianza kuwapiga mkwara wenzie kuwa wasubiri watakiona cha mtema kuni Waziri Magufuli akirudi toka bungeni, kwamba wamefanya kosa kumhamisha.
Ukweli ni kwamba Kapongo hana sifa na hata wenzie wana-doubt kama ana cheti hata cha form IV tu achilia mbali cha taaluma ya uhasibu. Maana hajuwi kazi yoyote zaidi ya kusaini cheque tu, hata kuandaa vote book hafahamu!
Magufuli alipoingia Dar toka bungeni Dodoma, Kapongo kwa kuujua udhaifu wa Waziri alimfuata akiwa na some docs zenye signature yake na bosi wake aitwaye Lyatuu na nyinginezo (God knows kama ni za kweli au si za kweli!) akamjaza maneno mengi sana kuwa Bosi wake Bw. Lyatuu ni mwizi sana anaiba pesa za Serikali etc.
Magufuli bila kuuliza akatoa amri Kapongo arudishwe TBA na akaufuta uhamisho wake, at the same time akatoa amri kuwa kesho yake anataka Lyatuu aripoti Kigoma na Bw. Nsangalo aliyekuwa Mwanza aripoti Dar haraka sana. Bw. Kapongo aliporudishwa TBA akawatambia wenzie kuwa "si nilisema? Mmeona nini kimefanyika?"
Baada ya tukio hilo ambalo Magufuli hakumshirikisha Katibu Mkuu wake wala Naibu katibu Mkuu wake, Bw. Kimweri alimuandikia barua Kapongo ya utovu wa nidhamu, kwa kitendo chake cha kuruka ngazi zote hadi kwa Waziri ilhali uongozi wa TBA haufahamu kama kulikuwa na matatizo hayo aliyodai Kapongo.
Mbaya zaidi wiki iliyopita mwishoni baada ya kupokea barua toka kwa CEO wake Kimweri, Kapongo aliibeba barua hiyo na kwenda moja kwa moja kwa Magufuli kushtaki, kuwa Kimweri kamwandikia barua ya kumuonya.
Magufuli bila kuuliza kitu alifunga safari hadi TBA, ambako aliingia kwa mkwara mkali, alianza kutukana kuanzia nje ya ofisi, alipofika mlangoni akafungua mlango kwa kuupiga teke. Akamaka "TBA mmejaa majizi matupu, hili lijizi likubwa liko wapi…" maneno hayo aliyaropoka mbele ya wafanyakazi waliopigwa na butwaa.
Akapiga simu kwa Katibu Mkuu wake akisema akifumba na kufumbua anataka kumuona Bw. Nsangalo kakalia kiti chake. Aliendelea kubwata mbele ya wafanyakazi kuwa akiamka kesho yake Kimweri u-CEO atausikia tu. Kwakweli ilikuwa ni hali ya udhalilishaji kazini na mtu kama Magufuli kwa nafasi yake hakupaswa ku-handle situation hiyo kwa staili ya mithili ya mtu aliyepagawa.
Kweli, kesho yake Magufuli akatoa amri Bw. Kimweri aondolewe TBA na kupelekwa wizarani na nafasi yake akakaimishwa msaidizi wake. Kama haitoshi sasa Magufuli anampigia debe swahiba wake aitwaye Mwakalinga ndio achukue nafasi ya Kimweri. Mwakalinga ambaye hana uwezo wa kushika nafasi hiyo jina lake kalipeleka kwenye Bodi na Bodi imekataa kupitisha jina hilo.
Bodi ya wakandarasi sasa inatishia kufanya mgomo kupinga maamuzi ya kidikteta ya Magufuli. Hali si shwari tena TBA, ukali na njia anazotumia Magufuli bila utaratibu zinawafanya watu kuwa waoga, maana hawajuwi nani atasingiziwa nini wapi iwapo watatofautiana na Waziri wao. Magufuli anampigia debe Mwakalinga kwa sababu ya uswahiba walio nao na pia kwa sababu huyo Mwakalinga kwa kushirikiana na Kapongo ndio waliomjengea nyumba yake.
Magufuli ili awe kiongozi mzuri inabidi afuate taratibu na sheria zilizopo, kama kuna wizi umefanyika anapaswa kuitisha Auditing team kubaini tatizo na si kukurupuka tu kwa majungu anayopelekewa na kuumiza wengine wasio na hatia. Mbona yeye mwenyewe ni fisadi? Kiongozi anayetumia nafasi yake vibaya ni ufisadi.
Magufuli ameshindwa kuangalia rekodi ya utendaji kazi ya Bw. Lyatuu ambaye tangu ameshika nafasi hiyo TBA ameingiza miradi mingi na fedha nyingi kuliko alipokuwepo Bw. Nsangano (aliyerudishwa tena) aliyeiacha TBA na sh. 4m tu wakati Lyatuu ameiinua TBA kwa ukusanyaji mzuri wa madeni na kutafuta miradi inayoifanya TBA kujiendesha yenyewe.
Magufuli amemrudisha Nsangalo aliyeshindwa kabla na ambaye hana PR yoyote kuwezesha TBA kupata miradi na kujiendesha. Alipohamishiwa Mwanza TBA huko imekufa, haina kitu kabisa na sasa kamrudisha Dar aiue pia.
Magufuli tutamuamini vipi kuwa ni msafi baada ya kujijengea magorofa manne (4) yaliyopo kitalu 172 Upper Kinondoni, magorofa aliyojengewa kwa msaada wa Mwakalinga na Nsangalo, magorofa aliyowapangisha Wakandarasi aliowapa kazi mwenyewe! Magufuli anawezaje kufuta hisia zetu kuwa hachukuwi 10% za wakandarasi hao?
Ndio maana pia Magufuli aliharakisha zoezi la kumuondoa Ephraem Mrema wa TANROADS, aliyetengenezewa zengwe na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Miundombinu by then Bw. Omar Chambo na kumpa nafasi hiyo Bw. Mfugale – swahiba wake pia. Ndio maana hadi leo TANROADS tangu aondoke Mrema bado hakujatulia. Hii ni kwasababu ya maamuzi yasiyozingatia sheria ya watawala wetu wanaoangalia interest zao kwanza. This is not health for our country's development.
Magufuli anapaswa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo akishauriana na subordinates wake kama Katibu Mkuu, naibu katibu Mkuu, Menejimenti, Bodi etc. alichokifanya TBA is very unethical and it is against good governance and rule of law.
Kwani mtu kama Kapongo kama si majungu baada ya matukio hayo hakupaswa kumrudisha tena TBA, ambako hata yeye amechangia machafuko. Kama ni kuhamisha alipaswa ahamishe wote, kumrudisha Kapongo TBA tafsiri yake ni nini? Vyombo vinavyohusika fuatilieni hili na mtabaini mengi yaliyo nyuma ya pazia.
Hayo ni maoni yangu.