Kwa hili la TBA Mhe. Magufuli umekosea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili la TBA Mhe. Magufuli umekosea!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wanitakiani, Aug 22, 2011.

 1. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bw. John Pombe Magufuli amekosea! Tumesikia mabadiliko yaliyotokea katika Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuondolewa kwa CEO wake Bw. Makumba Kimweri na kupelekwa Wizarani.

  Magufuli amejizolea sifa nyingi miongoni mwa watz kama kiongozi mzuri na mchapakazi hasa kwa staili yake anayoitumia ya ufuatiliaji na udikteta. Kwani wakati mwingine sifa hiyo ni nzuri, lkn kuna nyakati inaweza pia kuleta madhara kwa sababu haizingatii utawala wa sheria (rule of law).

  Magufuli kwa waliofanya naye kazi kwa karibu wanaweza kukupa story tofauti na usiweze kuamini kama huyu ndiye yule Magufuli anayepambanuliwa miongoni mwa viongozi wengi kuwa ni muadilifu. La hasha! Magufuli hayupo hivyo, ni mnafiki anayevaa ngozi ya kondoo kuwahadaa Watz. Ni fisadi na mpenda majungu kupita kiasi.

  Magufuli anaweza kufanyia kazi hearsay as if amepewa taarifa za kweli na zilizothibitishwa, inategemea nani kawahi kumpa majungu na ni nani kwake.

  Kuondolewa kwa Mkurugenzi mkuu wa TBA Bw. Kimweri kulianza kama mchezo. Chokochoko ilianzia kwa mtumishi mmoja wa idara ya uhasibu Bw. Kapongo ambaye ni jamaa yake Magufuli, wengine wanasema ni mjomba wake alipopewa uhamisho kwenda Wizarani baada ya kuwepo kutoelewana na wafanyakazi wenzie.

  Kapongo alipopata barua ya uhamisho alianza kuwapiga mkwara wenzie kuwa wasubiri watakiona cha mtema kuni Waziri Magufuli akirudi toka bungeni, kwamba wamefanya kosa kumhamisha.

  Ukweli ni kwamba Kapongo hana sifa na hata wenzie wana-doubt kama ana cheti hata cha form IV tu achilia mbali cha taaluma ya uhasibu. Maana hajuwi kazi yoyote zaidi ya kusaini cheque tu, hata kuandaa vote book hafahamu!

  Magufuli alipoingia Dar toka bungeni Dodoma, Kapongo kwa kuujua udhaifu wa Waziri alimfuata akiwa na some docs zenye signature yake na bosi wake aitwaye Lyatuu na nyinginezo (God knows kama ni za kweli au si za kweli!) akamjaza maneno mengi sana kuwa Bosi wake Bw. Lyatuu ni mwizi sana anaiba pesa za Serikali etc.

  Magufuli bila kuuliza akatoa amri Kapongo arudishwe TBA na akaufuta uhamisho wake, at the same time akatoa amri kuwa kesho yake anataka Lyatuu aripoti Kigoma na Bw. Nsangalo aliyekuwa Mwanza aripoti Dar haraka sana. Bw. Kapongo aliporudishwa TBA akawatambia wenzie kuwa "si nilisema? Mmeona nini kimefanyika?"

  Baada ya tukio hilo ambalo Magufuli hakumshirikisha Katibu Mkuu wake wala Naibu katibu Mkuu wake, Bw. Kimweri alimuandikia barua Kapongo ya utovu wa nidhamu, kwa kitendo chake cha kuruka ngazi zote hadi kwa Waziri ilhali uongozi wa TBA haufahamu kama kulikuwa na matatizo hayo aliyodai Kapongo.

  Mbaya zaidi wiki iliyopita mwishoni baada ya kupokea barua toka kwa CEO wake Kimweri, Kapongo aliibeba barua hiyo na kwenda moja kwa moja kwa Magufuli kushtaki, kuwa Kimweri kamwandikia barua ya kumuonya.

  Magufuli bila kuuliza kitu alifunga safari hadi TBA, ambako aliingia kwa mkwara mkali, alianza kutukana kuanzia nje ya ofisi, alipofika mlangoni akafungua mlango kwa kuupiga teke. Akamaka "TBA mmejaa majizi matupu, hili lijizi likubwa liko wapi…" maneno hayo aliyaropoka mbele ya wafanyakazi waliopigwa na butwaa.

  Akapiga simu kwa Katibu Mkuu wake akisema akifumba na kufumbua anataka kumuona Bw. Nsangalo kakalia kiti chake. Aliendelea kubwata mbele ya wafanyakazi kuwa akiamka kesho yake Kimweri u-CEO atausikia tu. Kwakweli ilikuwa ni hali ya udhalilishaji kazini na mtu kama Magufuli kwa nafasi yake hakupaswa ku-handle situation hiyo kwa staili ya mithili ya mtu aliyepagawa.

  Kweli, kesho yake Magufuli akatoa amri Bw. Kimweri aondolewe TBA na kupelekwa wizarani na nafasi yake akakaimishwa msaidizi wake. Kama haitoshi sasa Magufuli anampigia debe swahiba wake aitwaye Mwakalinga ndio achukue nafasi ya Kimweri. Mwakalinga ambaye hana uwezo wa kushika nafasi hiyo jina lake kalipeleka kwenye Bodi na Bodi imekataa kupitisha jina hilo.

  Bodi ya wakandarasi sasa inatishia kufanya mgomo kupinga maamuzi ya kidikteta ya Magufuli. Hali si shwari tena TBA, ukali na njia anazotumia Magufuli bila utaratibu zinawafanya watu kuwa waoga, maana hawajuwi nani atasingiziwa nini wapi iwapo watatofautiana na Waziri wao. Magufuli anampigia debe Mwakalinga kwa sababu ya uswahiba walio nao na pia kwa sababu huyo Mwakalinga kwa kushirikiana na Kapongo ndio waliomjengea nyumba yake.

  Magufuli ili awe kiongozi mzuri inabidi afuate taratibu na sheria zilizopo, kama kuna wizi umefanyika anapaswa kuitisha Auditing team kubaini tatizo na si kukurupuka tu kwa majungu anayopelekewa na kuumiza wengine wasio na hatia. Mbona yeye mwenyewe ni fisadi? Kiongozi anayetumia nafasi yake vibaya ni ufisadi.

  Magufuli ameshindwa kuangalia rekodi ya utendaji kazi ya Bw. Lyatuu ambaye tangu ameshika nafasi hiyo TBA ameingiza miradi mingi na fedha nyingi kuliko alipokuwepo Bw. Nsangano (aliyerudishwa tena) aliyeiacha TBA na sh. 4m tu wakati Lyatuu ameiinua TBA kwa ukusanyaji mzuri wa madeni na kutafuta miradi inayoifanya TBA kujiendesha yenyewe.

  Magufuli amemrudisha Nsangalo aliyeshindwa kabla na ambaye hana PR yoyote kuwezesha TBA kupata miradi na kujiendesha. Alipohamishiwa Mwanza TBA huko imekufa, haina kitu kabisa na sasa kamrudisha Dar aiue pia.

  Magufuli tutamuamini vipi kuwa ni msafi baada ya kujijengea magorofa manne (4) yaliyopo kitalu 172 Upper Kinondoni, magorofa aliyojengewa kwa msaada wa Mwakalinga na Nsangalo, magorofa aliyowapangisha Wakandarasi aliowapa kazi mwenyewe! Magufuli anawezaje kufuta hisia zetu kuwa hachukuwi 10% za wakandarasi hao?

  Ndio maana pia Magufuli aliharakisha zoezi la kumuondoa Ephraem Mrema wa TANROADS, aliyetengenezewa zengwe na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Miundombinu by then Bw. Omar Chambo na kumpa nafasi hiyo Bw. Mfugale – swahiba wake pia. Ndio maana hadi leo TANROADS tangu aondoke Mrema bado hakujatulia. Hii ni kwasababu ya maamuzi yasiyozingatia sheria ya watawala wetu wanaoangalia interest zao kwanza. This is not health for our country's development.

  Magufuli anapaswa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo akishauriana na subordinates wake kama Katibu Mkuu, naibu katibu Mkuu, Menejimenti, Bodi etc. alichokifanya TBA is very unethical and it is against good governance and rule of law.

  Kwani mtu kama Kapongo kama si majungu baada ya matukio hayo hakupaswa kumrudisha tena TBA, ambako hata yeye amechangia machafuko. Kama ni kuhamisha alipaswa ahamishe wote, kumrudisha Kapongo TBA tafsiri yake ni nini? Vyombo vinavyohusika fuatilieni hili na mtabaini mengi yaliyo nyuma ya pazia.

  Hayo ni maoni yangu.

   
 2. THE PERFECT

  THE PERFECT Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaweza kufupisha mkuu? all in all Magufuli ni mtu makini sana
  I dont think as you explained
  anyway wakuu watasema
   
 3. c

  chiungutwa Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  inavyoonekana kuna jambo hapo ila mdau kama ulivyotoa wazo tuache vyombo husika wafuatilie mwisho wa siku tutajua tu mbivu na mbichi.
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kaka ndefu mno halafu wabongo wengi wavivu kusoma ungeongeza haya ingekuwa nzuri zaidi..
   
 5. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Habari imejaa chuki binafsi dhidi ya Magufuli.
   
 6. TEMPOLALE

  TEMPOLALE JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Penye blue pamenistua sana. Kuna kila dalili kwamba Magufuli amekugusa pabaya....... any way sisi masikio yetu, tutasikia akiwajibishwa maana kama kweli hafuati utawala wa sheria lazima itakula. Unajua nimejiuliza sana yaani magufuli katukana na kupiga teke milango ya serikali???????? This is too much bwana.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Duh Mkuu umeongea maneno mazito sana. Kama ni hivyo kweli ndivyo alivyo magufuli basi tena!!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  unajua kunawatu wanamwamini sana magufuli ni kwa sababu ni nafuu kati ya magamba lakini kumbukeni magamba hakuna msafi ni system waliojijengea!
  ndo maana tunasema ili nchi iendelee ccm idondoke kwanza!
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Suala la magufuli kupewa ten percent kwenye miradi ya barabara limekuwa likitajwa tajwa mara nyingi, inawezekana ni kweli.

  Hata hivyo hili la udikteata na kuhamisha watu linahitaji ufuatiliaji zaidi manake isije kuwa mdau unayelalamika nawe ni muathirika wa kumbakumba ya magufuli. Nadhani ukweli utajulikana tu muda si mrefu ngoja tuuutafute.
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,964
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Mkuu, inawezekana kweli kuna jambo hapo, lakini jinsi ulivyoipresent hii issue inaonekana kama una chuki binafsi na Magufuli. Mtu akisoma aya ya kwanza tu ya story yako, kabla hata hujaeleza kisa chenyewe, anagundua moja kwa moja kwamba wewe na Magufuli ni mbalimbali. Pre-judgemental presentation imekuinflunce sana ktk kuileta hii habari. Sielewi kama kweli umemtendea haki Magufuli.
   
 11. T

  The Priest JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mtaisha wote!mmetafuna sn nchi yetu,mkipewa demo ndio mnajua kama kuna kanuni na taratibu ktk ajira,magufuli safi sana.big up!
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Sijaelewa hapa, ina maana Magufuri yupo juu ya sheria? au una maana hao uliowataja ndio hawajui haki zao? na kama kumwamisha mtu kwenda Kigoma kuna ubaya gani?

  Kuhusu swala la Mrema si kweli kwamba aliondolewa na Magufuri wala Magufuri hakuwa na uwezo huo ni nyie mnaoongea mambo ya mtaani ndio mnapindisha ukweli, ni kweli kuwa Mrema hakuwa na kosa lolote na pia alikuwa mtendaji mzuri lakini ujuwe kuwa muda wa mkataba wake TANROADS uliisha hata kabla ya Uchaguzi ni kwa vile Rais alisitisha mchakato wa kujaza nafasi yake ili kupisha uchaguzi hivyo ilikuwa ni lazima baada ya uchaguzi nafasi ijazwe, sheria ilikuwa inaruhusu extension ya mkataba ila tayari jamii ilikwisha potoshwa mengi juu ya Mrema na watu kama wewe wanaoongea bila kujuwa ukweli.

  Unachosema hapa hakitoshi kumtoa CE wa Agency, ujuwe kuwa CEO wa Agency siyo mfanyakazi wa wakawaida wa Wizara hivyo hawezi kuamishiwa wizarani maana anafanya kazi kwa mkataba maalum, labda rudi utafute ukweli zaidi utuelete, maana hapa umechanganya ukweli na uongo kwahiyo habari nzima imekuwa uongo. Huyo CEO ama hana qualification au kuna kosa lilofanya ambalo wewe ulijui maana yeye na Magufuli wapo sawa kimadaraka na kisheria hakuna ambaye anaweza kunyea mwingine kiasi hicho kama hakuna mkondo wa sheria uliopita hapo.

  Ni kweli ni Magufuri ni Bogus lakini unayosema hapa hayawezekani hata siku mmoja katika ofisi ya Umma, hata kama ungesema amemfanyia house boy wake bado ningeshangaa maana nao wana haki zao
   
 13. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Samahani ndugu inaonekana kuna maslahi yako yamebanwa kulingana na maamuzi ya magufuli.umeanza kwa chuki za waziwazi juu yake,hata kama ni uswahiba yeye atawasimamia na watafanya kazi,uswahiba umejaa serikali mfano wizara ya maliasili.
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwenye red: Burudani tosha kwangu. Magufuli mwanaume sio hawa wanaoshindwa kufanya maamuzi magumu. Fanya maaumizi na kama ni kulaumiwa ulaumiwe kuliko kukaa kimya. Hongera Magufuli.
   
 15. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  TAARIFA KWA MTOA MADA!CEO WA TBA,muda wa kukaa pale umeisha tangu mwaka huu mwanzoni,na nafasi hiyo iliishatangazwa kwenye magazeti.kwa hiyo kutolewa kwake sio kuonewa hata kidogo.
   
 16. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  whistle blower! Endelea kutupa detail hata km watu watakuwa wagumu kuamini lakini kuna ukweli ktk baadhi ya mambo uliyosema. Me sio mara ya kwanza kusikia hizo habari. Ya jairo yanafanyika hata kwa magufuli kila idara inatenga 20 ml kusaidia kupitisha budget so hakuna msafi ccm wote wezi tu.
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Isije ikawa Pombe amegusa maslai ya mtoa mada!
  Time will tell!
   
 18. k

  king11 JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lakini huna la kufanya kwani mkitaka kuhoji tu magufuli anamtishia rais kwamba yeye atajiuzulu na rais anamuogopa sana

  kumbukeni kipindi cha uteuzi wa chief Tanroads( bw.mfugale) alisema kama si mfugale basi mr president mimi sitaki kuwa katika serikali yako na ndivyo ilivyokuwa
   
 19. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa Mada
  Moja: article yako umeiandika kwa jazba.
  Mbili: maelezo yako yamekaa kimajungu pia.
  Tatu: TBA haijawahi kuwa na mafanikio kama unavyoinadi!! haiyumkini hata humu jamvini kuna wachache saana wanaofahamu kazi za TBA!!!
  Kwa hayo matatu:- Si huyo Lyatuu wala hao unaowasema wameisogeza TBA!! Kwa jinsi ninavyofahamu kazi za TBA nathubutu kusema kuwa utendaji wa Taasisi hiyo ni Mzigo kwa walipa kodi wa nchi hii!!!


   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  napita wakuu
   
Loading...