Kwa hili la Mtwara, CCM imenifariji...!

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
NAFARIJIKA...!


Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.


Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maagizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni. Agizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.


Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!
 
Hii ni ahadi ya ngapi kwa kipindi hiki cha mwisho cha jk pekee? 66+3=? Kwe tanzania inawezekana kuongozwa hata na mtoto wa chekechea,kama ahadi za miaka ya nyuma hazijatimizwa na bado unaongezwa ahadi nyingine na unachekelea!!we ni mtu wa aina gani??kweli ccm ina haki ya kutudharau!kwani wanaelewa wazi kuwa inaongoza mataahira+mabwege.
 
Hizo ni ngonjera wenzako wanafisadi wakijiandaa kuachia ngazi 2015! Ccm iwaambie kila mtanzania anadaiwa sh ngapi kwa deni la nje na sh ngapi kwa deni la ndani. Maana kila kukicha ni kuendelea kukopa tu. Vijana mpo? Nchi yetu hii tunauzwa tukikodoa macho!
 
Wewe Ray Jay kweli ni mtu wa Mtwara au umeamua kufanya Sarakasi na taulo mchana kweupe?,CCM sasa ndiyo inaadhirika ,kwani haukuona jana pale ,Viongozi walivyozomewa?,kama kusoma haukusoma je hata Picha kaka?.
 
Suala la mafanikio ya ziara kama hii tunaweza kuyapima kwa kuyalinganisha na mafanikio ya kwanza ya Mheshimiwa Nape Nnauye katika ziara yake ya kuimarisha chama ambapo alitembelea mikoa ya Sumbawanga na kumaliza kabisa tatizo la Maji mkoani humo, pamoja na ardhi, na pia kukagua na kongeza nguvu ujenzi wa hospitali ya rufaa katika Mkoa wa Singida na sasa hospitali hiyo inakaribia kukabidhiwa kwani tayari imekamilika kwa ujenzi ambao ulikuwa unalegalega ama kusimama kabisa ila baada ya Mheshimiwa Nape kupita kukagua na kuwataka wakandarasi kuendelea na ujenzi kwa spidi mpya na hivyo kufanikisha mradi huo mkubwa wenye msaada mkubwa kwa wakazi wa Singida.
 
Kama zuzu vile, au unaamka usingizini, ulikuwa unaota.ndio matatizo ya kushindia chilimundu
 
Wewe Ray Jay kweli ni mtu wa Mtwara au umeamua kufanya Sarakasi na taulo mchana kweupe?,CCM sasa ndiyo inaadhirika ,kwani haukuona jana pale ,Viongozi walivyozomewa?,kama kusoma haukusoma je hata Picha kaka?.


Mimi si mtu wa Mtwara bali ni mtu wa Nachingwea wilaya iliyopo mkoa wa Lindi, lakini matatizo ama kero hizo za Mtwara juu ya korosho hazina tofauti na huku kwetu, lakini si tu kuwa matatizo yetu yanafanana lakini pia aina ya watu wake tunafafa, ninayo haki lakini pia wajibu wa kuyazungumza yale yanayowahusu watu wa kusini, haya ni yetu...!
 
Maneno ya mfa maji, ina maana wakati nyinyiemu inaomba ridhaa haikujua kuwa inatakiwa kuwatumikia wananchi?

  • A%20S%20angry.gif


 
... Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara...
Viongozi wa chama kutoa maagizo kwa viongozi wa serikali! Labda tusubiri utekelezaji wa maagizo! Hata Nape alitoa maagizo nyufa za majengo kule UDOM zizibwe!
 
Mimi si mtu wa Mtwara bali ni mtu wa Nachingwea wilaya iliyopo mkoa wa Lindi, lakini matatizo ama kero hizo za Mtwara juu ya korosho hazina tofauti na huku kwetu, lakini si tu kuwa matatizo yetu yanafanana lakini pia aina ya watu wake tunafafa, ninayo haki lakini pia wajibu wa kuyazungumza yale yanayowahusu watu wa kusini, haya ni yetu...!


Kumbeeeee ni kule kwa Waziri Chikawe,Vipi ulipata zile Sanda za Mheshimiwa ?,Sanda ni matayarisho ya awali ya Kuzika ,sijui umenipata?.
 
Mimi naamini kama Serikali itatilia nguvu rasilimali za Mtwara basi uchumi wa nchi yenu utapanda sana na Kwa kuwa na bandari, Gas na ardhwi yenye rutba kwa kilimo cha Ufuta na Korosho ninaamini Mtwara baada ya miaka si zaidi ya mitano itakuwa na uchumi mkubwa ikizidiwa na dar tu huko Tanzania.

Wengi wa wawekezaji wanajikita kutaka kufungua viwanda huko.

Hongera Mtwara
 
Viongozi wa chama kutoa maagizo kwa viongozi wa serikali! Labda tusubiri utekelezaji wa maagizo! Hata Nape alitoa maagizo nyufa za majengo kule UDOM zizibwe!

Nafasi ya kiongozi wa Chama kwa kiongozi wa serikali ni kuagiza na maagizo haya yanatokana na Ilani ya Chama ambapo kila wizara na waziri husika wanapewa na kuagizwa kuitekeleza, inapotokea kulegalega nafasi ya kiongozi wa chama ni kukumbusha kwa kuyataja maagizo hayo kwa waziri ama kiongozi husika chini ya wizara fulani juu ya utekelezaji wa agizo hilo ambalo lipo kwenye ilani ya Chama.

Jambo hili la kufufua viwanda na kupanua wigo wa ajira hasa kwa vijana lipo katika maagizo ya Chama kwa serikali chini ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2010. lakini pia jambo hili lipo katika jarida dogo la chama linalotaja MWELEKEO WA SERA ZA CCM katika miaka ya 2010 hadi 2020. Si jambo ambalo linabebwa na kuletwa kama agizo from no where..! ni agizo ambalo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Kinana analifahamu kwa undani na anatambua ni nini anakiagiza...!
 
Je na ile Ahadi ya M bunge Murji ya kuchimba Visima vya Kudril kwa kila Mtaa wa JIMBO la Mtwara Mjini kaitimiza tayari?.Acha porojo ww ,Mtwara siyo ile ya miaka ya 1995.Upo?.
 
... kulegalega nafasi ya kiongozi wa chama ni kukumbusha kwa kuyataja maagizo hayo kwa waziri ama kiongozi husika chini ya wizara fulani juu ya utekelezaji wa agizo hilo ambalo lipo kwenye ilani ya Chama
Kwa hiyo hapa unatuambia kwamba viongozi wa serikali ya CCM ( kama vile mawaziri na wakuu wa Mkoa) hawafai kuongoza nchi hii kwa kuwa wanasubiri kukumbushwa vitu vilivyomo kwenye ilani ya chama, ambayo nakala zake wanazo maofisini! Na kwa kuwa hawafai, basi tuchague chama kingine ambacho serikali yake haihitaji kukumbushwa mambo yaliyo bayana!
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Huyu mleta mada anataka kunitafutia ban mie niwe Guest tu hapa jamvini ,ngoja niendelee na shughuri zangu mie .
 
Back
Top Bottom