Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Ikiwa ndio anamalizia muda wake wa ukuu wa mkoa Arusha na kwenda mapunzikoni, wakazi wa jiji la Arusha tunakupongeza sana bwana Isidori kwakuliona hili tatizo la kusimamisha lile zoezi la watoza ushuru wa wrong parking kwa waendesha magari hapa jijini Arusha. Ilikua ni kero kubwa sana kwetu sisi waendesha magari, kwanza hii kazi ingetakiwa iwe ya Traffic na sio wao, yaani unawakuta hawa jamaa wanatembea na lichuma fulani hivi na kuwawekea wenye magari na kudai ushuru wa shilingi elfu 40000 kisa umepaki vibaya na hapo ulipopaki hakuna alama inayoonyesha kua sio halali kupaki hapo, ukiwauliza wapi kibao kinachoonyesha kua umepaki vibaya hawakuelewi na muda huo tayari wameshakuwekea hilo chuma. kweli ilishafikia wakati unaendesha gari lako mwenyewe lakini huna uhuru nalo ilkua ni kero mbaya sana. Asante sana bwana Shirima japokua ulichelewa kusimamisha hili zoezi na tumeshaliwa hela nyingi lakini Mungu akubariki huko unapokwenda kumalizia uzee wako. Naunga mkono hoja.