KWA HILI CHUO KIKUU ARDHI HAMJAWATENDEA HAKI WANAFUNZI

mzee wa kismati

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
2,292
795
Mlitoa tangazo kwamba mnatoa muda wa siku tano kwamba kuanzia tarehe 11 mpaka tarehe 15 wanafunz wote ambao hawajakamilisha usajiri wawe wamefanya hivyo.
muitikio ulikuwa mkubwa idadi kubwa ya wanafunzi walifanikiwa kusajiriwa

ajabu mi kwamba leo malipo ya awamu ya pili ya pesa za kujikimu yani BOOM yamefika, lakini kwa wanafunzi waliosajiliwa kipindi hiki wengi hawajapata fedha hizo

nimeshuhudia idadi kubwa ya wanafunzi wakilaani kitendo hicho cha kibaguzi wakiwa wamejawa na sura zenye majonzi, mmesababisha usumbufu mkubwa kwani idadi kubwa ya watoto hawa wa wakulima wametumia nauli zao kwenda benki kutoa hela kwa ajili ya kulipa kodi ya nyumba na kuambulia patupu

mimi kama mzazi nalaani sana kitendo hiki cha kibaguzi na kionevu kwanini kuwasumbua vijana hivi yamkini mkijua hamuwapi pesa zao? mmeshindwa hata kutoa taarifa fupi? naomba mamlaka zinazohusika mlishughulikie hili kabla halijafika kwa magufuli
 
Usilalamike taratibu ndiyo zilivyo. Unasajiri ndiyo majina yanaenda kwa ajiri ya ku process malipo. Next time wafanye mapema
 
Mlitoa tangazo kwamba mnatoa muda wa siku tano kwamba kuanzia tarehe 11 mpaka tarehe 15 wanafunz wote ambao hawajakamilisha usajiri wawe wamefanya hivyo.
muitikio ulikuwa mkubwa idadi kubwa ya wanafunzi walifanikiwa kusajiriwa

ajabu mi kwamba leo malipo ya awamu ya pili ya pesa za kujikimu yani BOOM yamefika, lakini kwa wanafunzi waliosajiliwa kipindi hiki wengi hawajapata fedha hizo

nimeshuhudia idadi kubwa ya wanafunzi wakilaani kitendo hicho cha kibaguzi wakiwa wamejawa na sura zenye majonzi, mmesababisha usumbufu mkubwa kwani idadi kubwa ya watoto hawa wa wakulima wametumia nauli zao kwenda benki kutoa hela kwa ajili ya kulipa kodi ya nyumba na kuambulia patupu

mimi kama mzazi nalaani sana kitendo hiki cha kibaguzi na kionevu kwanini kuwasumbua vijana hivi yamkini mkijua hamuwapi pesa zao? mmeshindwa hata kutoa taarifa fupi? naomba mamlaka zinazohusika mlishughulikie hili kabla halijafika kwa magufuli
Mkataa pema pabaya panamwita, mlikataa elimu bure
 
Back
Top Bottom