Kwa haya, Utaifa wa chadema una walakini...!

Kwa haya, Utaifa wa chadema una walakini…!

Baada ya yote yanayotokea naomba turudi kuzungumzia maadili ya utaifa. Kwa maana ya utaifa kama msingi na alama ya uwepo wetu kama WATANZANIA, bila ya watanzania kuwa na maadili ya utaifa hakuna Maendeleo ama mabadiliko ambayo yatakuwa na maana.

Maadili ya utaifa yana maana kubwa sana kwa kila mtanzania, tujivunie utaifa wetu na tupende kutambulika kwa utaifa wetu.

Lakini maadili ya Taifa pia ni kutojiona bora kuliko wengine, kutokuwa mbinafsi kwa kujijali mwenyewe ama kikundi chako ama taasisi yako ama chama chako na badala yake kufanya kila jambo huku ukijali na kuweka mbele maslahi ya taifa. Tukianzia hapo, tutapata viongozi ama utawala unaojali zaidi maslahi ya taifa.

Tarehe 26/04/ ni siku ya muungano, muungano ni moja ya nembo muhimu kama Taifa, lakini pia ni ishara ya uwepo wa Taifa liitwalo Tanzania kwani Taifa hilo linatokana na maamuzi ya busara yaliyofanywa na waasisi wa muungano huo. Lakini pia ni elimu, historia na kumbukumbu kwa watoto na kizazi cha sasa kuwa kulikuwapo na matukio muhimu ya namna hii ambayo yalikuwa ni asili ya umoja wetu na utaifa wetu.

Kitendo cha viongozi waandamizi wa chadema kutohudhuria katika sherehe hizi kumeacha maswali na mkanganyiko mkubwa katika vichwa vya watanzania juu ya misimamo na itikadi za viongozi wa chama hiki kikuu cha upinzani hivi sasa.

  • Je, kwa kitendo hiki wanataka watanzania waamini kuwa wao hawana haja ya muungano na kwa maana hiyo muungano kwao sio kitu cha msingi kuadhimishwa
  • Ama hii ndiyo maana ya falsafa ya upinzani kuwa unapinga kila kitu kilichoasisiwa na viongozi wa chama tawala na serikali ( hata yale yanayowakilisha utaifa wetu)
  • Lakini tafsiri ya kuwepo kwa viongozi wengine wa vyama vya siasa (ccm, cuf, tlp,udp, cck n.k) na kukosekana kwao wao pekee ni ishara kuwa wao ni bora kuliko hawa wengine wote..?
  • Lakini kama hayo hayatoshi, viongozi hawa wananafasi gani katika matukio kama haya kulingana na falsafa ya wajibu wa raia “citizens obligation to nation” ni kweli wanayo nafasi ya kufanya dharau hii..?
  • Haya pamoja na mengine mengi ikiwemo kauli ambayo mpaka leo haijawahi kukanushwa ya mmoja wa vongozi waandamizi wa chadema kuwa hatahakikisha kuwa nchi hii “HAITAWALIKI” vina nafasi gani katika dhana ya UTAIFA wetu.

Labda niseme kuwa, ni vyema kwa watanzania, wanaharakati na yeyote aliye katika ari ya kuona mustakibali mwema wa nchi hii akatambua kuwa tunahitaji kuheshimu na kufuata maadili ya taifa na kusimamia utaifa wetu.
Ni kweli kuwa tunahitaji mabadiliko katika Nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, siasa na hata mabadiliko katika mienendo ya jamii yetu ila kwa hili la kudharau misingi ya umoja wetu na utaifa si jambo jema na wala hatuhitaji kufanya mabadiliko kwenye misingi ya utaifa wetu.

Wewe ndugu yangu una mambo unashangaa CHADEMA kutofika kwenye sherehe wakati cdm haina serikali kWA NINI USUSHANGAE RAIS WA ZANZIBAR KUTOFIKA KWENYE SHEREHE HIYO? VITU VINGINE BWANA CHUNGUZENI KWANZA KABLA YA KULAUMU. MWENYE MSIBA HALII WEWE JIRANI UNALIA MPAKA KUZIMIA HIVI JIRANI ATAKUWA NA UCHUNGU ZAIDI KULIKO NDUGU? UNAFIKI HAUTAKIWI CHADEMA WAKO SAHIHI ASILIMIA MIAMOJA. ALIYEKUJA PALE NI KARUME AMBAYE HANA SERIKALI HAMADI ULIMUONA? BALOZI SEIF IDD ALIKUWEPO? KAMA HAO HAWAKUWEPO CHADEMA WAMESAHAU NINI PALE MPAKA WAENDE?
 
...kwa akika chadema hamuwezi kutuongoza sisi, mpaka leo hakuna chama chenye welekeo wa kuongoza labda kina mwamunyange ndo wakabidhiwe dola ili tueshimiane, chadema mna visasi hamuwezi kuongoza, na kwa taarifa yenu mpaka inafika 2015 mtakuwa mmemeguka vipandevipande, hii issue ya muungano ni ya kitaifa si ya kisiasa mlipashwa kuudhulia kama wenzenu walivyofanya

Chama chochote cha siasa duniani kina misingi na misimamo yake. Hakuna chama chochote duniani chenye ridhaa ya kuburuza chama kingeni kwa kigezo cha mambo ya kitaifa. Nani mwenye ushahidi ndani ya CCM au nje ya CCM kuwa muunganano wa Tng na Zn imetokana na ridhaa ya wananchi wa pande zote hizo mbili. Its obvious kwamba hakuna, maana hata muungano wenyewe umekaa kiuchonganishi na kichokozi zaidi. Muungano wenyewe hauna hati ya maridhiano, sasa ya nini kuishinikiza CDM kusherehekea nosence. Huu ni ubatili mtupu wenye masilahi kwa CCM na viongozi wake wenye laani ya kufisidi nchi!
 
...kwa akika chadema hamuwezi kutuongoza sisi, mpaka leo hakuna chama chenye welekeo wa kuongoza labda kina mwamunyange ndo wakabidhiwe dola ili tueshimiane, chadema mna visasi hamuwezi kuongoza, na kwa taarifa yenu mpaka inafika 2015 mtakuwa mmemeguka vipandevipande, hii issue ya muungano ni ya kitaifa si ya kisiasa mlipashwa kuudhulia kama wenzenu walivyofanya

Chama chochote cha siasa duniani kina misingi na misimamo yake. Hakuna chama chochote duniani chenye ridhaa ya kuburuza chama kingeni kwa kigezo cha mambo ya kitaifa. Nani mwenye ushahidi ndani ya CCM au nje ya CCM kuwa muunganano wa Tng na Zn imetokana na ridhaa ya wananchi wa pande zote hizo mbili. Its obvious kwamba hakuna, maana hata muungano wenyewe umekaa kiuchonganishi na kichokozi zaidi. Muungano wenyewe hauna hati ya maridhiano, sasa ya nini kuishinikiza CDM kusherehekea nosence. Huu ni ubatili mtupu wenye masilahi kwa CCM na viongozi wake wenye laani ya kufisidi nchi!
 
Kwa haya, Utaifa wa chadema una walakini…!

Baada ya yote yanayotokea naomba turudi kuzungumzia maadili ya utaifa. Kwa maana ya utaifa kama msingi na alama ya uwepo wetu kama WATANZANIA, bila ya watanzania kuwa na maadili ya utaifa hakuna Maendeleo ama mabadiliko ambayo yatakuwa na maana.

Maadili ya utaifa yana maana kubwa sana kwa kila mtanzania, tujivunie utaifa wetu na tupende kutambulika kwa utaifa wetu.

Lakini maadili ya Taifa pia ni kutojiona bora kuliko wengine, kutokuwa mbinafsi kwa kujijali mwenyewe ama kikundi chako ama taasisi yako ama chama chako na badala yake kufanya kila jambo huku ukijali na kuweka mbele maslahi ya taifa. Tukianzia hapo, tutapata viongozi ama utawala unaojali zaidi maslahi ya taifa.

Tarehe 26/04/ ni siku ya muungano, muungano ni moja ya nembo muhimu kama Taifa, lakini pia ni ishara ya uwepo wa Taifa liitwalo Tanzania kwani Taifa hilo linatokana na maamuzi ya busara yaliyofanywa na waasisi wa muungano huo. Lakini pia ni elimu, historia na kumbukumbu kwa watoto na kizazi cha sasa kuwa kulikuwapo na matukio muhimu ya namna hii ambayo yalikuwa ni asili ya umoja wetu na utaifa wetu.

Kitendo cha viongozi waandamizi wa chadema kutohudhuria katika sherehe hizi kumeacha maswali na mkanganyiko mkubwa katika vichwa vya watanzania juu ya misimamo na itikadi za viongozi wa chama hiki kikuu cha upinzani hivi sasa.

  • Je, kwa kitendo hiki wanataka watanzania waamini kuwa wao hawana haja ya muungano na kwa maana hiyo muungano kwao sio kitu cha msingi kuadhimishwa
  • Ama hii ndiyo maana ya falsafa ya upinzani kuwa unapinga kila kitu kilichoasisiwa na viongozi wa chama tawala na serikali ( hata yale yanayowakilisha utaifa wetu)
  • Lakini tafsiri ya kuwepo kwa viongozi wengine wa vyama vya siasa (ccm, cuf, tlp,udp, cck n.k) na kukosekana kwao wao pekee ni ishara kuwa wao ni bora kuliko hawa wengine wote..?
  • Lakini kama hayo hayatoshi, viongozi hawa wananafasi gani katika matukio kama haya kulingana na falsafa ya wajibu wa raia “citizens obligation to nation” ni kweli wanayo nafasi ya kufanya dharau hii..?
  • Haya pamoja na mengine mengi ikiwemo kauli ambayo mpaka leo haijawahi kukanushwa ya mmoja wa vongozi waandamizi wa chadema kuwa hatahakikisha kuwa nchi hii “HAITAWALIKI” vina nafasi gani katika dhana ya UTAIFA wetu.

Labda niseme kuwa, ni vyema kwa watanzania, wanaharakati na yeyote aliye katika ari ya kuona mustakibali mwema wa nchi hii akatambua kuwa tunahitaji kuheshimu na kufuata maadili ya taifa na kusimamia utaifa wetu.
Ni kweli kuwa tunahitaji mabadiliko katika Nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, siasa na hata mabadiliko katika mienendo ya jamii yetu ila kwa hili la kudharau misingi ya umoja wetu na utaifa si jambo jema na wala hatuhitaji kufanya mabadiliko kwenye misingi ya utaifa wetu.
Majibu aliyatoa Dr. Slaa juu ya kwanini CDM hawakushiriki sherehe za muungano. Lakini cha msingi kama una uchungu na utaifa wetu basi ujiulize kwanza kati ya ccm na CDM nani wana utaifa? CDM wanaogomea sherehe na CCM wanaolea mafisadi nani anabomoa utaifa? CHADEMA wanaohoji hati ya muungano na CCM wanaopalilia udini ili tu wabaki madarakani nani wanabomoa utaifa? CDM waliokataa kwenda uwanja wa uhuru na ccm wanaowalinda na kusamehe wezi nani anabomoa utaifa? CDM wanaodai mfumo wa muungano ubadilishwe ili kukidhi mahitaji ya sasa na ccm wanaong'ang'ania mfumo wa serikali mbili nani anabomoa muungano?
 
Kama w/mkuu hajui Znz ni nchi au la,ww unayeadithiwa tu utaniamisha vipi kuna muungano wa haki?makubaliano yeyote halali duniani huwekwa kimaandishi.
 
Walikuwa wanapanga jinsi ya kuanza tena maandamano yao yasiyo kuwa na tija kwa taifa

lenye tija hapa ni lipi ikiwa tu hata historia ya muungano ina chakachuliwa,tuwe wa kweli hao CDM wana sababu yao ya msingi cha muhimu ni kuwaomba walete ufafanuzi.Lakini hta kwa akili ya haraka haraka utawezaje kukaa na fisadi meza moja ilihali yeye ana tafakari kuiibia nchi yetu
 
Ooh...oooh!!...natamani wananchi wangeulizwa kuhusu huu muungano.Tupige kura kuuhalalisha tu.
 
Henge unafikiri kwa kutumia masaburi kabisa! Ni tabia yao kutohudhuria shughuli za kitaifa siyo hiyo tu, si unakumbuka hawakumtambua Rais lakini wakaenda kunywa kahawa walipokuwa na lao jambo. Sisi tunawajua hao CDM wanapenda umaarufu kwa vitu vidogo vidogo kama hivyo. Lazima wajitathimini kama kweli wanataka tuwapatie dhamana ya nchi hii. Kamwe hatutawapatia kama wana akili hilo za kipumbavu!
Uwezo wako wa kufikiri ulipogota, ukadhani watu wote wana upumbavu vichwani mwao kama wewe. Rais anaenda kuvunja baraza la wezi, we bado unawatetea kisa Muungano. Mshenzi mkubwa, kama unafaidika sie hatupo ila jua moja tu, CCMajambazi, chukua Cahako Mapema, Kwishny. Muunagano tutashehekea na viongozi wasafi wasio wezi, na walioingia madarakani kiharali. Sote twaupenda Muungano.
 
Hee..! kuazimisha sherehe ya Mungano wakati mabilioni ya watanzania yanaliwa na chama tawala ndo Utaifa huo....!!!!??? Tafakari, chukua hatua
 
It depends wewe unadefine vipi utaifa, Kukacha sherehe na wizi, kusababisha maumivu kwa wananchi ni kipi utaona kama kuusaliti utaifa? hebu zama kidogo uone kwa jicho la ukweli CDM hata ndani ya bunge wanatetea utaifa kwa kujali lasimilimali za nchi yetu!
 
Kwa hiyo utaifa ni kwenda kwenye sherehe za mwenge, Kuhudhulia sherehe za muungano n.k. wizi, ufisadi, upendeleo vyote ivyo utaifa? sijakuelewa you seems you impart yiourself a myopic sightation!
 
Ms umerudi tena? Siku nyingi hujaonekana. Kuhusu utaifa wa cdm kamuulize msajiri wa vyama vya siasa!!!!!!!!!!
 
utaifa ni upendo wa mtu kwa taifa lake..,una njia nyingi za kujionesha si tu kwa kuhudhuria sherehe za muungano..,lakini ni wao viongozi wa chadema kwanini hawakuhudhuria.,mbona wanakuwa watata sana hawa jamaa.,wana nini...?
 
Back
Top Bottom