Kwa haya, Utaifa wa chadema una walakini...!

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Kwa haya, Utaifa wa chadema una walakini…!

Baada ya yote yanayotokea naomba turudi kuzungumzia maadili ya utaifa. Kwa maana ya utaifa kama msingi na alama ya uwepo wetu kama WATANZANIA, bila ya watanzania kuwa na maadili ya utaifa hakuna Maendeleo ama mabadiliko ambayo yatakuwa na maana.

Maadili ya utaifa yana maana kubwa sana kwa kila mtanzania, tujivunie utaifa wetu na tupende kutambulika kwa utaifa wetu.

Lakini maadili ya Taifa pia ni kutojiona bora kuliko wengine, kutokuwa mbinafsi kwa kujijali mwenyewe ama kikundi chako ama taasisi yako ama chama chako na badala yake kufanya kila jambo huku ukijali na kuweka mbele maslahi ya taifa. Tukianzia hapo, tutapata viongozi ama utawala unaojali zaidi maslahi ya taifa.

Tarehe 26/04/ ni siku ya muungano, muungano ni moja ya nembo muhimu kama Taifa, lakini pia ni ishara ya uwepo wa Taifa liitwalo Tanzania kwani Taifa hilo linatokana na maamuzi ya busara yaliyofanywa na waasisi wa muungano huo. Lakini pia ni elimu, historia na kumbukumbu kwa watoto na kizazi cha sasa kuwa kulikuwapo na matukio muhimu ya namna hii ambayo yalikuwa ni asili ya umoja wetu na utaifa wetu.

Kitendo cha viongozi waandamizi wa chadema kutohudhuria katika sherehe hizi kumeacha maswali na mkanganyiko mkubwa katika vichwa vya watanzania juu ya misimamo na itikadi za viongozi wa chama hiki kikuu cha upinzani hivi sasa.

  • Je, kwa kitendo hiki wanataka watanzania waamini kuwa wao hawana haja ya muungano na kwa maana hiyo muungano kwao sio kitu cha msingi kuadhimishwa
  • Ama hii ndiyo maana ya falsafa ya upinzani kuwa unapinga kila kitu kilichoasisiwa na viongozi wa chama tawala na serikali ( hata yale yanayowakilisha utaifa wetu)
  • Lakini tafsiri ya kuwepo kwa viongozi wengine wa vyama vya siasa (ccm, cuf, tlp,udp, cck n.k) na kukosekana kwao wao pekee ni ishara kuwa wao ni bora kuliko hawa wengine wote..?
  • Lakini kama hayo hayatoshi, viongozi hawa wananafasi gani katika matukio kama haya kulingana na falsafa ya wajibu wa raia “citizens obligation to nation” ni kweli wanayo nafasi ya kufanya dharau hii..?
  • Haya pamoja na mengine mengi ikiwemo kauli ambayo mpaka leo haijawahi kukanushwa ya mmoja wa vongozi waandamizi wa chadema kuwa hatahakikisha kuwa nchi hii “HAITAWALIKI” vina nafasi gani katika dhana ya UTAIFA wetu.

Labda niseme kuwa, ni vyema kwa watanzania, wanaharakati na yeyote aliye katika ari ya kuona mustakibali mwema wa nchi hii akatambua kuwa tunahitaji kuheshimu na kufuata maadili ya taifa na kusimamia utaifa wetu.
Ni kweli kuwa tunahitaji mabadiliko katika Nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, siasa na hata mabadiliko katika mienendo ya jamii yetu ila kwa hili la kudharau misingi ya umoja wetu na utaifa si jambo jema na wala hatuhitaji kufanya mabadiliko kwenye misingi ya utaifa wetu.
 
Hoja yako ni nzuri kwa kuwa muungano ni jambo jema sana,lakini kuna kimoja ambacho CCM inafanya makosa,muungano huu wameukumbatia sana wao kama chama na kuwanyima wenzao kufahamu baadhi ya mambo!kwa mfano mkataba wa muungani kwa nini uwe siri na mbaya zaidi ni siri ya CCM! Kwa hili CDM wananifurahisha sana kwa kuwa nionavyo mimi muungano huu ni wa CCM!
 
Muungano nini bana mnawaambukiza wenzenu wazanzibar wizi tu... Kule kulikuwa hakuna kuibiana kura yahe mbaka wabara wa ccm walivyokwenda kule ... Waacheni wazanzibar wa watu wajikalie tuwe tunaenda kuwatembelea tu...
 
Henge unafikiri kwa kutumia masaburi kabisa! Ni tabia yao kutohudhuria shughuli za kitaifa siyo hiyo tu, si unakumbuka hawakumtambua Rais lakini wakaenda kunywa kahawa walipokuwa na lao jambo. Sisi tunawajua hao CDM wanapenda umaarufu kwa vitu vidogo vidogo kama hivyo. Lazima wajitathimini kama kweli wanataka tuwapatie dhamana ya nchi hii. Kamwe hatutawapatia kama wana akili hilo za kipumbavu!
 
Walikuwa wanapanga jinsi ya kuanza tena maandamano yao yasiyo kuwa na tija kwa taifa
 
Nilimuona lipumba, Maalim Seif pamoja na CCM- C Cheyo, vipi mliadhimisha muungano wa CCM na CUF au upi huo?. Kama ni ule wa Tanganyika na Zenji mbona hakuna aliyewahi kuona hiyo hati ya muungano?. Au muungano ni ule wa mchanganyiko wa mchanga wa unguja na ule wa DSM?. Na tukichukua mchanga mwingine kule Nairobi tukachanganya na wa kutoka Tanga hiyo nayo utaita muungano?.
 
Wala Nchi hii haihitaji jambo moja kubwa kuliko yote UNAFIKI niambie maana ya utaifa. Muungano ambao hati yake inafichwa! Muungano ambao kuujadili ni Uhaini!

Muungano ambao ni kama ndoa iliyolazimishwa na wazazi, muungano ambao unatumika kuua demokrasia. Suala la msingi hapa siyo kuusherehekea ila kuujadili. Sijawahi ona NDOA ambayo wanandoa hawajadili mapungufu yao ili kuimarisha ndoa. HUU NI UNAFIKI CDM haihutaki.

UNAFIKI NA WOGA VINAUA NCHI!!
 
Kwanza kabisa CDM hatupendi unafiki, hatuwez tena hatuwez kabisa kutoa sura ya furaha huku nafsi zetu zikiwaka moto kwa kutendwa dhuluma, tuna fanya mambo kwa maana, UTAIFA UNAOUSEMA WEWE NI ULE WA MAIGIZO, UTAIFA WA KWELI NI ULE WA KUTETEA HAKI YA TAIFA LAKO na HAKI YAKO KTK TAIFA LAKO. Naona Umevurugwa kijana.
 
Henge unafikiri kwa kutumia masaburi kabisa! Ni tabia yao kutohudhuria shughuli za kitaifa siyo hiyo tu, si unakumbuka hawakumtambua Rais lakini wakaenda kunywa kahawa walipokuwa na lao jambo. Sisi tunawajua hao CDM wanapenda umaarufu kwa vitu vidogo vidogo kama hivyo. Lazima wajitathimini kama kweli wanataka tuwapatie dhamana ya nchi hii. Kamwe hatutawapatia kama wana akili hilo za kipumbavu!
MPUMBAVU ni wewe katika hili. Akili isiyo na uchambuzi ni janga linaloendelea kuitafuna TAIFA. Wewe ngojea uangukie na hilo jumba bovu CCMAJAMBAZI kabla ya 2015. Ridhaa yako ni sumu kwetu CDM
 
Hoja yako ni nzuri kwa kuwa muungano ni jambo jema sana,lakini kuna kimoja ambacho CCM inafanya makosa,muungano huu wameukumbatia sana wao kama chama na kuwanyima wenzao kufahamu baadhi ya mambo!kwa mfano mkataba wa muungani kwa nini uwe siri na mbaya zaidi ni siri ya CCM!Kwa hili CDM wananifurahisha sana kwa kuwa nionavyo mimi muungano huu ni wa CCM!
Hili la kuwa hati ya muungano ni siri ya CCM mimi binafsi sina ushahidi nalo labda ukinithibitishia kuwa mkataba wa muuungano ni siri ya CCM..,lakini kama hilo ndilo kuwa ni siri ya CCM suluhisho lake ni kuwa chadema wasiudhurie kwenye maadhimisho ya muungano huo???
wakumbuke kuwa hata kuwepo kwao wao kama chama cha upinzani ni siri ya CCM.,kwani watanzania walipinga vyama vingi kwa maoni yao yaliyokusanywa chini ya tume ya jaji nyalali ni siri ya CCM na serikali kuleta vyama vingi.,lakini mbona leo hii hatukatai vyama vingi kwa kuwa kuanzishwa kwake ilikuwa ni siri ya CCM.
 
Magamba hoyeeeeeeeeeeeee!!!!!!! TUNDU LISSU HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!! UVCCM ARUSHA HOYEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni vema tukatafakari mambo kwa kina kama watanzania kabla ya kutoa hoja zetu hapa kwenye jukwaa, nionavyo mimi madai ya chadema kuhusu hati ya muungano ni ya msingi sana. Kwa hali halisi muungano unaoneka ni wa upande fulani jambo ambalo litaathiri muungano wetu tukufu hapo baadaye. Wito wangu tuache unafiki na tuungalie muungano kiuhalisia.
 
Henge unafikiri kwa kutumia masaburi kabisa! Ni tabia yao kutohudhuria shughuli za kitaifa siyo hiyo tu, si unakumbuka hawakumtambua Rais lakini wakaenda kunywa kahawa walipokuwa na lao jambo. Sisi tunawajua hao CDM wanapenda umaarufu kwa vitu vidogo vidogo kama hivyo. Lazima wajitathimini kama kweli wanataka tuwapatie dhamana ya nchi hii. Kamwe hatutawapatia kama wana akili hilo za kipumbavu!

na wewe umetumwa na hao magamba?
 
Ninachoamini mimi sasa ni kwamba nchi hii bado inao wajinga wengi, hivi wewe unadhani watu wangapi wanafaidi muungano huu ambao umegeuzwa kuwa sehemu ya kuwaibia wazanzibari? je unafikiri wazanzibari wanautaka muungano kama wewe unavyoutaka? je wewe mwenyewe umekufaidia nini?au wewe unafuata chama,cdm wako kimaslahi ya watanzania zaidi hivyo usiwe mjinga kiivyo
 
Uwepo wa chdm katka uso wa siasa tz, ni kutokana na kutambulika na hiyo katba ya muungano, isingekuwepo!
Lakini, ni ukweli kuwa kuna mbinu tofauti tofauti za kuonesha kutokubaliana na jambo fulani, nadhani chdm wametumia moja wapo!
Je, ni sahihi kwa mtu kushiri na mwizi kwa kuwa ni nduguye, upi ni utaifa ambao umeadhimishwa? Serikali imesaliti utaifa wetu, na walishauzika zamani, tusijidanganye kuurudisha kwa vinubi vya harusini.
 
Siku zote akili nyingi huondoa maarifa.

Poleni sana Chadema.
Kama walikuwa hawautambui muungano mbona walikwenda kugombea uwakilishi kule Uzini.

Unafiki mtupu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom