Kwa hali hii kikwete atafika kweli?

kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,173
114
Mshiriki namba 6, Pendo Sam alizomewa alipokuwa anajibu swali lililomtaka aseme ni sifa gani za kiongozi anayemtaka kuwa Rais wa Tanzania.

Pendo, alijitahidi kueleza sifa kulingana na kiwango chake cha ufahamu lakini alipoanza kumpigia debe Rais Jakaya Kikwete alikiona pale hadhira ilipomgeuka na kumzomea kwamba pale hapakuwa mahali pake.
 
Si kosa lake binti pendo kwani alidhani hadhira yake ilitaka jibu kama alilotoa. Pia kwa vile alikuwa katika mechi bila shaka alidhani jibu lake lingemwongezea maksi toka kwa majaji.

Anyway hadhira yake imemsahihisha na kuonesha kuwa JK hafai. Nawapongeza kwa ushujaa huo. Asanteni, ujumbe wenu umefika.

Ombi langu dogo kwao ni kuwa waoneshe kwa matendo tarehe 31.10.10, kuwa JK hafai kuongoza tena nchi yetu, hivyo apunzishwe kwa lazima, kwa vile mwenyewe hakutaka kwa hiari yake.
 
alimzimikia mzee kwani hata akitoka nje ya nchi inasemekana tz tunasifika kwa na rais mzuri wa sura lkn dhaifu wa kuongoza.................binti hajakosea ameona asiusemee moyo wake....................
 
Mrembo hajakosea bse unaweza kuta kwa maneno yale tuu akaukwaa UDC!
 
Thread yako haina tija kwa jamii ya watanzania.

Aliboa sana huyu mrembo!
Watu wameingia kwa nauli na kiingilio chao pale(100,000), halafu wanakuja kusikia mpiga debe wa JK, what a fuss!...Huenda wangekuwa ni wale wa mashati ya kijani na wameletwa na malori pale wangemchagua!
Labda angemfagilia DrSlAA angekuwa miss Tz fasta!...
 
Mrembo hajakosea bse unaweza kuta kwa maneno yale tuu akaukwaa UDC!

Kwiwkwiii.. mkuu umenifurhisha sana,
Ila nimpe pole hakuna UDC anymore, Raisi wetu mteule Dr. waslaa ameahidi kuondoa hivyo vyeo visivyo na tija kwa Taifa letu, na hata hivyo vyeo vya undugu, kujuana na na vya kupeana nyuma ya pazia huo ndo utakuwa mwisho wake! KATIBA MPYA NDANI YA SIKU 100! ukiritimba na ubaradhuli wote bye bye!!
 
JK kumkampeni kunahitaji moyo.

Watu wamemchoka
.

unaakili sana , umeandika neno zito sana.
"...........ccm imeajiri wapuuzi ili wafanye kazi za kipuuzi"..Jenerali Ulimwengu.

kumkapenia Kikwete lazima kwanza uwe mpuuzi ama unamtatiziko wa mawazo na akili, ama njaa iwe kali kufikia kiasi cha kupofusha macho ya aibu na fedhea, kumkapenia Kikwete yata moyo.
 
KWA kWELI BINTI ANGEUKWAA UMISS LAKINI TATIZO ALIIINGIZA MAMBO YA SIASA NA KUONYESHA UWEZO WAKE WAKUFIKIRI NI MDOGO SANA HEKO MAJAJI KWA KUMMWAGA ALISTAHILI KUSHINDWA. ALINIBOA KWELI SIKU ILE!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom