Kwa dunia ya sasa kuoa si lazima sana

Kwa dunia ya sasa kuoa si lazima sana

Muda ukifika utaoa tu . Mbn haina mjadala, utaoa tu asee

"In Good times ,Friends know you BUT in Sorrow, you know them [emoji23]"
 
Kwa jinsi ninavyojitathimin, mke wangu atakuwa pesa.

Yani kuoa sio kupaumbele kwangu kabsa mpaka sasa, huenda nitabdili mtazamo lakin sio sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hoja ni fikirishi sana.
Talking from experience ukioa/olewa na mtu mnaependana, kuna uwezekano mkubwa mkawa na maisha yenye furaha, amani na raha, ukioa/olewa na mtu usiyempenda, mateso na karaha zake nadhani zinafuatia za Jehanum, na hili linasababishwa na watu wanaooa/olewa on long motives/causes, mfano mtu kuoa/kuolewa na mtu sababu za kiuchumi, misukomo ya kijamii au familia, n.k kwa kweli ndoa itakuwa chungu, Ni bora uchelewe sana kuolewa lakini uoe/olewe na mtu sahihi. Ndoa (iliyotokana na mapenzi ya kweli) ni kitu kizuri sana, narudia ni kitu kizuri sana chenye raha na furaha nyingi,
Mimi niko kwenye ndoa for about a year now, lakini mara nyingi i wish pengine ningechelewa kidogo kuoa, pengine nafikiria nisingemuoa mwanamke huyu niliyemuoa sasa, yaani ningelijua kibao, na maswali mengi yasiyo na majibu.
Ninachoweza kushauri na kusema ni kuwa bado kuna mambo mazuri kwenye ndoa, cha msingi kabla ya kuingia kwenye ndoa fanya utafiti na uchunguzi wa kutosha kwa mtu unayekusudia awe life partner wako, ukioa/olewa na mtu unayempenda, mtu ambaye ni mzuri unavutiwa naye kila siku, mtu ambaye ukimuona unajisikia raha, amani na kupata nuru katika macho na roho yako, hutakuja ujutie ndoa yako.
Tafuta mrembo/hb, i mean mtu unayevutiwa naye (beauty is on the eyes of the beholder) achana na mambo ya tabia, hiyo ni nadharia iliyopitwa na wakati, ni rahisi kumvumilia mtu changamoto zake kwa kufikiria uzuri wake zaidi ya uzuri wa tabia zake ( hapa sitaeleweka).
Nadhani mleta hoja ametoa toa maoni based on his/her experience ambayo of course siyo conclusive kila mtu atafanya maamuzi on his/her best interest.
 
Unaweza pata watt bila hata kuoa halafu jiulize je ipojr kwa mtu ambaye ameoa kisha mke wake akafariki na yeye akwa labda ana miaka kama 60 hivi je uzee wake atasaidiwa na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao watoto wa nje ya ndoa ndiyo wanaoleta shida kubwa kwa kukosa malezi ya wazazi wote wawili na ni kutokana na mmonyoko wa maadili unaozidi kwa nyakati zetu hizi. Mtu ameolewa au ameoa kisha akafiwa akabaki mjane au mgane anaweza kuolewa au kuoa mwingine au atasaidiwa na watoto wake. Kufiwa na mwenza hakuondoi umuhimu wa kuolewa na kuoa.
 
Sooo hypothetical the reality is different though.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio Hypothesis ndiyo nimetumia kujibu ila inapotokea wanandoa hawaifurahii ndoa yao jua katika kufunga ndoa hiyo hawakupendana ila kila mmoja alikuwa na malengo fulani. Ndiyo maana wanaume wanatoka nje ya ndoa vile vile wanawake. Unakuta walikuwa na upendo mwingi lakini baada ya ndoa na kuzaa watoto mvuto wa kimapenzi unapungua hadi kuisha kabisa, vimada vinajitokeza shamba boy au house girl anaingilia ndoa. Pamoja na changamoto zote hizo umuhimu wa ndoa upo pale pale. Tusijidanganye kuwa naongea tofauti na uhalisia wa mambo.
 
Acha waoaneeeee🎼🎵🎶🎤📢📢📢
 
Kula kuku mzima hapo ulipo kiukweli ndoa zinatesa sana sana tuliopo tunatanani kutoka hasa sisi ke ndio waathirika loh ningepata ushauri huu kabla pengine nisinge kua nalia kwa kusalitiwa na wanawake zaidi ya mia sasa du ndoa mtihani

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni mob psychology!ila usemayo ni kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umuhimu wa ndoa unakuja kwenye kuraise familia, kama unataka kuwa na watoto waliokua na kelewa vizuri, ndoa ni muhimu, kinachotakiwa ni kuwa makini tu kwenye kuchagua mwenza, sio mmekutana wiki moja tu unatangaza ndoa, lazima utaumia, mimi tumekaa kwenye uhusiano karibu miaka kumi ndio nikaoa, sijajutia bado, na sitarajii..

hii sasa kali, kama uko sensitive sana na kusalitiwa, ndoa itakuwa changamoto sana, katika mia, ni ndo mbili tu ambazo hawasalitiani, cha msingi ni usiri tu na kuheshimiana, mimi michepuko ninayo kibao tu, ila naamini mke wangu hajui na tunaishi kwa amani. Na inawezekana hata yeye washkaji wanakula kimya kimya, siyo ishu sana, cha msingi ananiheshimu na sijui kama anachepuka.
 
It is possible if you are lucky enough to get the good marriage. But most of the marriage problems will kill u before u become old.
Hehehee ni rahisi sana kwako kusema maneno haya kwakua ww ni mwanaume, fikiria umejaaliwa mtoto wa Kike halafu haolewi, anaishia kuzalishwa na wanaume tofauti ambao hawaoni umuhim wa kuowa km ww, utafurahia binti yako aishie hivi au unaongea tu kwakua ww umeumbwa mwanaume? Halafu ukishafika uzeeni nguvu zishakuishia unafkiri utahudumiwa na mama yako na dada zako au mkeo ndo atakaekustiri? Ndoa ni mapenzi, huruma, stara na heshima..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wa sasa mnaangamia kifikra na kimwili sababu ya kujiweka mbali na MUNGU pamoja na vitabu vyake.

Haya unayoyasema ni matokeo ya kufuata mitazamo, maneno, na kauli za wanadamu wenzako wenye vichwa vilivyojawa na jeuri na kiburi ambavyo vimekuwa ni chachu ya ninyi kushindwa kuuelewa muongozo wa mafunzo ya MUNGU.

Waliposema, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maalifa" hiki ndicho walimaanisha. Na mtaangamia kweli.


Ndoa ndio agizo kuu la MUNGU katika kuingia maisha ya ujana.......yale yote tunayofanya nje ya ndoa huwa ni batili kwa hali ya juu.

Unalala na wanaume sita au kumi halafu wa kumi na moja ndie unataka aje akuoe na amejua historia yako ya wale kumi uliowahi kuwa nao, kisha unataka akuheshimu na kukupa hadhi ya binti bikra, hiyo itawezekanaje?!

Umezaa na wanawake watatu tofauti, kisha unakuja oa binti wa watu na bado una mawasiliano na hao wanawake unataraji huyo mwanamke atakuwa na imani na wewe?!

Kiukweli haya mambo yamekatazwa katika vitabu vya MUNGU na wengi wao ambao walifuata na kushika maagizo ya MUNGU huwezi kuta wanazungumzia kuteseka na mapenzi katika jamii ya leo ambayo imejaa wakosaji wanaolaumiana kila m'moja akisema mwenzake ndio mkosaji. Bali utawaona wapo busy na ujenzi wa familia bora na future ya kutabirika kabisa na kuuona uzee wakiwa pamoja.


Madogo, mrejee vitabu vya MUNGU, vimeandikwa kwa lugha nyepesi kuelewa na ni rahisi kuvifuata mafundisho yake. Tena hasa hasa ninyi watoto wa kike, vitabu vya dini vimewataja mara nyingi kumaanisha ninyi ndie mnanafasi kubwa sana ya kukosea au kupatia. Sasa nyie endeleeni kuruhusu nyuchi zenu kuangaliwa na wanaume kadiri mnavyowabadilisha.......laana ya kuvulia nguo wanaume hovyo, kutoa ujauzito, kufanya ukahaba na umalaya itawafuata hata kama utapendeza siku ya ndoa yako kama malkia ila ule uchafu unaodhania ni siri, MUNGU anaujua na atakuhukumu nao kwa hesabu ile ile ya ukosaji wako
.
Mrejeeni MUNGU kabla ya kukosea ili awalinde na kuwaongoza maishani sio kukalia ujinga ujinga hapa na kulalamika upuuzi kama huyu mleta uzi. Pumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleka mno mkuu. Asante kwamba umenielewa. Nashukuru kwanza kuwajuza na wengine kwamba hii hoja ni fikirishi. Pili nimekuelewa pale uliposema wengi wanaoa au kuolewa kwa kufuata misukumo ya kijamii au familia. Ila daah...kama ulivyoongea wewe (hapa sitaeleweka) ni kweli uzuri tu bila tabia,ni kama naona bure tu. Lakini kiujumla nimekuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa tamu hasa uzeeni namuona Baba yangu anavyofaidi..
Usipooa uzee wako utakua na shida sana
Dah...kwa mwanaume ndoa ni kuondoa Uhuru wako kwa 75% ...kuongeza matumizi kwa 100%...bora uoe ukifika 60yrs....Ni mtizamo tu..[emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Acha upotoshaji ndoa ni muhimu kwa kuishi maisha marefu na yenye furaha. Kitu kikubwa ni unamchaguaje mume atakayekuoa au mke utakeyemuoa ili muishi kwa furaha. Kulingana na nyakati hizi wengi wanakata tamaa lakini hawajui kipindi kijacho kitakuwaje. Upo tayari uondoke bila kuacha copy duniani? upo radhi ukifika uzeeni ukose hata watoto wa kuongea nao au mume/mke wa kukujali katika hali ya uajuza au ukikongwe ulionao. Acha kuangalia karibu ndoa ilitengenezwa ili maisha yarahisike sie wenyewe tunaifanya inakuwa ngumu. Kama hujui unampataje mchumba bora ili aje kuwa mume au mke mtakayedumu naye karibu PM tukufunde.
Dah...umechanganya...kuwa na ndoa...na kuwa na watoto ...Ni vitu tofauti [emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
We jamaa kama una matatizo yako ya kimwili, kimtazamo kiafya, pambana na hali yako ila usipotoshe watu.
  1. Kwa wale waumini tumeambiwa kuwa enendeni duniania mkaijaze nchi, hii ni agizo la muumba
  2. Ukifika uzeeni kama huna mtoto unategemea utasaidiwa na nani kwa kazi za hapa na pale
  3. Hakuna furaha kama kuishi na kundi la watu ambao ni kizazi chako, kuna nyakati za furah na huzuni
  4. Ndoa zenye shida na karaha husababishwa na wepenzi wenyewe na si kusudi la Mungu
  5. Tendo la ndoa ni sehemu yenye kuleta furaha na msisimko wa kiakili, ndoa ndiyo gurantee pekee na sio kwa machangudoa
  6. Watu waliooa na kufuata misingi ya ndoa, ndo sehemu pekee ya kuepuka risk ya magojwa ya zinaaa na Ukimwi
Hope haya machache yatakusaidia
Hakuna mahala nilipopotosha watu. Hii ni mada fikirishi. Halafu kama mliambiwa zaeni mkaijaze dunia mimi hakuna mahala nimeongea msizae,hiyo ni mada nyingine. Utajua wewe utazaa kwa kuoa ama kuolewa. Ila mimi nimesema USIOE AU KUOLEWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom