Swet-R
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 5,671
- 8,233
Kiukweli kutoka moyoni mwangu nawashauri vijana ambao hawajaoa. Kwa dunia ya sasa kuoa si lazima sana. Kuoa ni kuyafanya maisha yako yawe mafupi hapa duniani. Ndoa nyingi za kibongo ni utumwa.
Ukioa unakosa uhuru wako binafsi. Hata wanawake si lazima kuolewa,japo upande wa wanawake kwa huku kwetu,wanaweza kuwa waathirika kwa kukosa ndoa,ksbb wengi wana matarajio ya kuolewa. Inajulikana wapo wengi hawaridhiki na ndoa zao zinavyoendelea,ila wapo tu ksbb tayari walishakosea. Wengi wameoa ili kutimiza wajibu,ndio maana ndoa karibia 90% ziko tabani. Ndio maana wenzetu wazungu wamefika mbali wanaoa kwa mkataba. Wakiona bado wanahitajiana baada ya mkataba,wanaongeza. Au hata waliooana bila mikataba wakichokana hawana haja ya kuitiana pressure.
Wanaongea tu na kuachana kistaarabu kabisa. Sio kama huku kwetu mtu anang'ang'ania tu japo mapenzi hayapo ni kuendelea kujiua taratibu kabla ya muda. Wengi wataishangaa hii mada badala ya kufundisha watu waishije na ndoa zao,kitu walichokizoea wengi,lakini hakijawahi kupata tiba.
Mimi nakuambia bora usioe maisha yako yote na usiolewe maisha yako yote,na ni njema sana ukijitambua mapema kwamba hutaoa ama kuolewa. Utaishi bila pressure na maisha marefu duniani
Sent using Jamii Forums mobile app