kwa babu loliondo video

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mamia ya watu wameendelea kumiminika Loliondo kufuata dawa ya babu mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile ambazo zinadaiwa kutibu magojwa sugu, wakati huo huo orijino komedi nao hawajakaa nyuma wametoa video kuhusiana na tiba ya babu ambayo imekuwa gumzo kubwa nchini.
Mamia ya watu wameendelea kwenda Loliondo kumuona babu ambaye bila kuchoka ameendelea kutoa dawa ambazo zimedaiwa kutibu magonjwa mbali mbali sugu kama Ukimwi, kisukari, shinikizo la damu na mengineyo.

Kuna foleni kubwa ya magari yanayoenda Loliondo kwa babu ambapo wagonjwa mbali mbali wengine wakiwa mahututi wamekuwa wakiwasili wakiwa wamebebwa na dugu zao.

Baadhi ya wagonjwa wamekimbia tiba walizokuwa wakipewa hospitalini na kukimbilia kwa babu wakiamini kikombe kimoja cha dawa za babu kitasaidia kuyaondosha magojwa waliyo nayo.

Angalia Video ya kipindi maalumu cha televisheni ITV kuhusiana na tiba ya babu mchungaji Mwasapile na Video ya pili ni Video ya kundi la kuvunja mbavu la Orijino Komedi ambalo nalo halijakaa kimya kutoa video kuhusiana na tiba ya babu ambayo imekuwa gumzo kubwa sana nchini.



ze comedy nao kwa babu yao Joti


 
Last edited by a moderator:
Umati huo waote wanatafuta uponyaji, kisha mjinga mjinga mmoja tena fisadi anasema dawa ya baubu haiponyi, Mungu anawapenda watu wake na wakati wa uponyaji ni huu, asiye amini basi na aendelee kuteketea.
 
tuombe mungu asimchukue babu mapema!

Haswa! maana hapa napanga nakupangua huyu mkoloni nimuageje.
Kila nikijaribu mbili haikai tatu haikai kizunguzungu kinanipata,
Hasa nikifikilia ile meli,
Isijefika kabla cjaenda huko
 
pole man na kwani likizo inaanza lini?subiri tu likizo maana ukienda kwa babu uhesabu na siku za kukaa kwenye foleni si unaona watu walivyo wengi!
Haswa! maana hapa napanga nakupangua huyu mkoloni nimuageje.
Kila nikijaribu mbili haikai tatu haikai kizunguzungu kinanipata,
Hasa nikifikilia ile meli,
Isijefika kabla cjaenda huko
 
Usijali foleni imeanza kupungua kuna ndugu yangu aliondoka Arusha jpili usiku saa 3 akafika saa 12 asubuhi jtatu mchana saa 7 akanywa dawa then saa 8 mchana wakaondoka jtatu hiyo then usiku wa manane wapo arusha washarudi na dawa wamekunywa wao gari yao ilikuwa ya 200 walipofika hiyo saa 12 asubuhi
 
Babu wala hana hata muda wa kubishana sijui eti na mwingira ..cijui kakobe..rosttamu...ye ni kazi tu..big up babu..may god bless you.:lol:
 
Unajua hawa wengine walishazoea kubishana sasa wanafikiri babu naye atafuata mkumbo kwanza kijijini kwake hakuna TV!!
 
Wanaodharau hiyo tiba na waendelee kwa nafsi zao. Watu wanaendelea kupona kwa hiyo miujiza na ni kupoteza muda kuwajadili akina RA na Mwgr kwa kuwa hawana mbadala wa hiyo miujiza
 
Babu hawezi bishana sababu sio mwanasiasa kama kina kakobe ambao wanasema ccm na tanesco mwogopeni mungu!
babu wala hana hata muda wa kubishana sijui eti na mwingira ..cijui kakobe..rosttamu...ye ni kazi tu..big up babu..may god bless you.:lol:
 
Back
Top Bottom