Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago!

Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago!

Kama walikuwa wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja na kukwepa Kodi hayo ndio matokeo na madhara yake mkuu. Suala la msingi pia inabidi uelewe ya kwamba sekta ya ujenzi haiko vizuri kwa sasa. Sababu mafisadi yamesimamisha ujenzi na majizi yako chini ya ulinzi.

wanaojenga inamaana ni mafisadi na majizi?.. kumchukia mwenye hela hakukufanyi wewe uwe tajiri..
 
Ni kweli, hili ndilo lilikuwa the biggest shop la Vifaa vya ujenzi along Old Bagamoyo Rd. Count jobloss, revenues loss, aftersale services loss, tenancy loss, quality products loss, etc, etc, Magufuli anaua!.
P
Alafu kuna mchumia tumbo yeye anataka aongezewe miaka
 
Hivi hii imani kwamba nchi hii ni wezi tu ndio walikuwa wanajenga na kufanya manunuzi yooote mnaitoa wapi? Zimbabwe imefika ilipofika kwa sababu Mugabe anawabana mafisadi? Magu akisoma comment kama yako nahisi anafurahi sana maana anaona ni rahisi kutuongoza
Usitake kulazimisha niwe na fikra Kama zako. Ninachoandika hapa kuhusu hawa jamaa nina hakika nacho. Wewe endelea na unachotaka kuamini wewe ni wajibu wako kikatiba.
 
kati ya posti zako zilizopita na mlengo wako wa leo siamini unachoandika! kumbe na wewe ni "msaliti" kama sie?? maajabu hayaishi Duniani

Sifa kubwa ya kuwa Great thinker ni kujadili Matukio sio kukariri kusifia au kukosoa

Ukiona kila Siku umekariri kumsifia Mtu au kikundi cha Watu au kukosoa tu kila Siku ujue Shingo yako imebeba tufe sio kichwa
 
Very true Siyabonga ila bavicha watakuja na porojo zao wakati hiyo iko wazi watu walizoea kufanya biashara bila kulipa kodi halali inayotakiwa what do you expect?????WAONDOKE
Huku wakitengeneza super profit mkuu.
 
Hilo nalo sio big deal, ingekua ni kiwanda hapo sawa, duka tu hata vichochoroni yamejaa au kuna mtu kakosa cement na misumari ya kujengea?
Hahahah mkuu umeongea lugha nyepesi anyway ngoja nikuache
 
Kama walikuwa wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja na kukwepa Kodi hayo ndio matokeo na madhara yake mkuu. Suala la msingi pia inabidi uelewe ya kwamba sekta ya ujenzi haiko vizuri kwa sasa. Sababu mafisadi yamesimamisha ujenzi na majizi yako chini ya ulinzi.
Uongo
 
Hivi hii imani kwamba nchi hii ni wezi tu ndio walikuwa wanajenga na kufanya manunuzi yooote mnaitoa wapi? Zimbabwe imefika ilipofika kwa sababu Mugabe anawabana mafisadi? Magu akisoma comment kama yako nahisi anafurahi sana maana anaona ni rahisi kutuongoza
Unaifananishaje Tanzania na Zimbabwe???
 
wanaojenga inamaana ni mafisadi na majizi?.. kumchukia mwenye hela hakukufanyi wewe uwe tajiri..
Kama ulizoea ujanja ujanja awamu hii hautoboi mkuu. Ndio maana huwezi kusikia muuza chips (just a metaphor) akilalamika, kwa kuwa asilimia kubwa wanafanya biashara kwa hali yao inavyoruhusu.
 
Hakuna anayependa kuweka hela yake mahala ambapo hapana usalama wa hela yake..

Hakuna International business yeyote duniani inafanyika pasipo watu kuiba, utaibiwa tu iwe kihalali au kibabe.

Dunia sio kijiji, huwezi kuwapangia watu wengine duniani namna ya kuishi huku akili huna na hauna msaada wowote kwa maendeleo ya dunia..

Wizi ni sehemu ya maisha duniani kwa sasa, kiachotofautisha ni aina ya wizi unaofanyika, wengine wanaiba bila kutumia akili na wengine wanaiba kwa kuhalalisha wizi wao, KULA ULIWE..

Akili ndio mtaji dunia ya sasa, Nguvu zilikuwa mtaji karne ya nne huko..
 
Ana haki hiyo Kidemokrasia Kama ulivyo Wewe kuona Miaka ibaki ile ile Mitano
Mnajifanya Mnapigania Demokrasia lakin mmeshindwa walau kuigiza kuvumilia mawazo ya wengine
Hapo umemaliza kila kitu mkuu. Kwa mwenye akili timamu atakuelewa.
 
Ana haki hiyo Kidemokrasia Kama ulivyo Wewe kuona Miaka ibaki ile ile Mitano
Mnajifanya Mnapigania Demokrasia lakin mmeshindwa walau kuigiza kuvumilia mawazo ya wengine
Mawazo yasiyo na mashiko huwa sio ya kuyavumilia hata siku moja
 
serikali sera zake sio makini, watendaji wa taasisi zake wanafunga tu biashara za watu hawajui walipoanza mpaka kufika hapo ,hawatoi elimu ya kutosha
ofisi moja vibali zaidi ya kumi TRA,NEMC,OSHA,LESENI,SERVICES LEVY,TIC,FIRE,LOCAL GOVT,BRELA,COSOTA,BARCODES,TFDA,TBS,CRB nk.......
hahahahahaha hii ndo nchi ya VIWONDER
 
Hawa maturuki bahili kumbe...hawana closing sale? Watabeba kila kitu kurudi navyo Uturuki?
 
Kama ulizoea ujanja ujanja awamu hii hautoboi mkuu. Ndio maana huwezi kusikia muuza chips (just a metaphor) akilalamika, kwa kuwa asilimia kubwa wanafanya biashara kwa hali yao inavyoruhusu.

Sio kosa lako, kosa lako ni kuishi kijijini na kutokuwa na exposure ya maisha. Roho mbaya ya kumchukia kila mwenye fedha na kumuona mwizi ni dalili mbaya aka UCHAWI.. kama umeshindwa kutafuta hela sio ndio na wengine washindwe kuzitafuta mkuu.. Hujui uhalisia wa mtaani huku ulivyo kwa wale wahangaikaji, bila shaka wewe mzee wa mwisho wa mwezi aka Muajiriwa.. Fanya uchunguzi acha mapenzi ya siasa, sio kila mtanzania anauza chips au unataka watanzania wote wawe wauza chips ndio iwe furaha yako???
 
Mtu anapofunga biashara hatutakiwi kushangilia, Ni vizuri tukakaa naye kuona ni vikwazo vipi vimepelekea apitie mapito hayo ili tujifunze na sio kuwa na majibu ya Jumla eti "MPIGA DILI",
 
Back
Top Bottom