Pasipo kupoteza muda!
Kumekuwepo na malalamiko mengi sana juu ya jeshi la polisi kitengo cha traffic kwamba wananyanyasa sana wenye magari barabarani!
Kuna watu wamefikia hatua hadi kuwaita Trafiki kwamba sasa NI WAKUSANYA KODI!
Mambo hayo yalinifanya nianze kuchunguza tatizo ni nini hadi tumefikia hapa! Nimejiuliza je; kama ni kweli, ina maana polisi wanapata wapi ujasiri Wa kubambikia makosa? Nikawaza tena, hao madreva wanakubali vipi kubambikiwa kosa? Je sheria zikoje? Madreva wanaouelewa Wa sheria barabarani?
Hizo leseni wanazipaje? Je madreva wanafuzu kweli mafunzo vyuoni?
Majibu ya maswali hayo ndiyo yamenifanya nijiulize sana! Niliamua kutembelea kituo kimoja cha polisi ili nipate kujua mambo haya, nikajibiwa watu hawazingatii usalama barabarani na wengi hawafahamu sheria na kuzizingatia, na bahati nzuri polisi mmoja akaniomba niambatane nae site ( tukaelekea barabarani nijionee). Ni kweli niligundua mambo mengi sana, nilijionea watu wakiendesha speed kubwa zaidi katika makazi (tochi), niligundua watu magari yao mengi ni mabovu, pia niligundua wale ambao sheria wanazijua na kuzizingatiwa walikaguliwa na kuruhusiwa waende!
Laikini kilicho nishangaza zaidi ni pale kila aliyekamatwa hakukosa sababu ya kujitetea, kuna watu walijitetea Kwa kudai wanaharaka, kuna wengine waliwapigia ndugu zao, wengine walilia machozi, wapo walikimbia n.k
Ingawa niligundua; miongoni mwa waliokamatwa wanawake ndiyo walionyesha kukubali kosa na kuandikiwa haraka kuliko wanaume;
NAOMBA TUJADILI JE; TATIZO NI TRAFIKI AU SHERIA NI MBOVU? KARIBUNI