ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,230
- 40,753
KUZAMA SIYO KWENYE MAJI TU
Tunaposema mtu amezama, mara nyingi tunafikiria amezama kwenye mto au bahari
Lakini katika maisha, kuna kuzama kwa aina nyingi
Wengine husema, Nimezama kwenye penzi
Lakini pia kuna watu waliozama kwenye maovu na tabia ambazo zinawatesa kila siku
Kuna kuzama kwenye kamari
Kuna kuzama kwenye pombe
Kuna kuzama kwenye dawa za kulevya
Kuna kuzama kwenye rushwa
Kuna kuzama kwenye uzinzi au umalaya
Kuna kuzama kwenye marafiki wabaya
Kuna kuzama kwenye madeni, uongo, au hata tamaa ya pesa za haraka
Kinachoumiza zaidi ni kwamba wengi wanaozama huko si kwamba hawajui
Wanajitambua kabisa
Wanajua wanachokifanya si sahihi Wanajua wanapoteza muda, kipato, familia, afya na heshima
Lakini wanashindwa kujinasua
Ni kama mtu anayezama majini Anaona kila kitu, anapambana kwa nguvu zote, lakini kadiri anavyojitahidi ndivyo anavyozidi kuzama 😔
Anatamani kutoka, lakini haoni njia 😟
Ninaamini sababu mojawapo inayowafanya watu washindwe kuacha tabia mbaya ni mazingira wanayoishi
Ni vigumu kuacha pombe ukiwa kila siku upo kwenye vijiwe vya pombe
Ni vigumu kuacha kamari ukiwa umezungukwa na marafiki wanaokushawishi kucheza kila siku
(Wadau wa betting wanaelewa)
Wakati mwingine mazingira humshinda hata mtu mwenye nia ya kubadilika 💯
Lakini je, mazingira ndiyo sababu pekee?
Au kuna mambo mengine kama , kuiga, marafiki, msongo wa mawazo, au kukata tamaa, kujilinganisha , sifa na kutokukinahi?
Karibuuunii wana JF
Je, umewahi kuzama kwenye tabia fulani ukashindwa kutoka, ingawa ulitamani kuiacha?
Ni kitu gani kilikufanya ushindwe kujinasua?
Kama uliweza kuacha, ni mbinu gani ilikusaidia?
- Umewahi kumsaidia mtu kuacha tabia mbaya?
Je ukifanyaje🤔
Ukiweka comment hapa anaweza akapona mtu hata kama asiposema karibuuni guys
Chombezo : umewasha mshumaa au kibatari?
ShesRise_1🤚