Kuwepo vs Kutokuwepo

QUALIFIED

JF-Expert Member
Jun 13, 2012
773
115
Wakuu habari
Kuna maswali huwa sipati majibu nikayaona ni sahihi naomba tushilikiane kupata majibu tafadhali
1. Kama usingekuepo wewe nafasi yako ingechukuliwa na nani? Kama isingechukuliwa mambo ambayo umeyafanya yasingefanyika?

2. Kama usingekuepo ungekua wapi? Na huko ambako ungekua ungekua ukijisikia kama unavyojisikia sasa?

QUALIFIE said:
Wakuu habari
Kuna maswali huwa sipati majibu nikayaona ni sahihi naomba tushilikiane kupata majibu tafadhali
1. Kama usingekuepo wewe nafasi yako ingechukuliwa na nani? Kama isingechukuliwa mambo ambayo umeyafanya yasingefanyika?
Kama nisingekuwepo,na nafasi yangu isingekuwepo

Na kama nafasi yangu isingekuwepo,basi isingechukuliwa na mtu yoyote kwasababu haipo
2.Kama usingekuepo ungekua wapi?
Hili swali ni 'self defeating',lina jipinga lenyewe

Kama nisingekuwepo,nisingekuwa popote
Na huko ambako ungekua ungekua ukijisikia kama unavyojisikia sasa?
Hali ya 'kutokuwepo',ni sawa na kipindi ulichopitia kabla hujazaliwa

Kwani ww,kabla hujazaliwa ulikuwa unajisikiaje?
 
Kama nisingekuwepo,na nafasi yangu isingekuwepo

Na kama nafasi yangu isingekuwepo,basi isingechukuliwa na mtu yoyote kwasababu haipo

Hili swali ni 'self defeating',lina jipinga lenyewe

Kama nisingekuwepo,nisingekuwa popote

Hali ya 'kutokuwepo',ni sawa na kipindi ulichopitia kabla hujazaliwa

Kwani ww,kabla hujazaliwa ulikuwa unajisikiaje?
Huko 'kutokuwepo' ndio logic hapo mkuu.
Kusema usingekuepo basi usingekua popote that's so mean
Unafikili haya maswali hayana majibu? Ama wewe ndio hauna majibu
 
Mkuu kwema,..?

Hizo signature zako zinakera watu,.....ahahahahahaaaaaaaa
 
Tulikuwepo na tukifa tunabadili mwili tu na kuzaliwa upya .Kama ulikuwa mtenda maovu utazaliwa katika familia ambayo utapata mateso ya hapa duniani,Na kama unaishi mazingira magumu basi jua kuwa miaka216 nyuma ya mwaka wa kuzaliwa ulikuwepo na uliishi maisha mazuri ya anasa.
 
Uwepo(existence) maana yake ni uthibitisho wa hali au kitu katika hali au maada(matter) yoyote ile. Uwepo lazima uthibitishwe kwa namna yoyote aghalabu milango ya faham.
Kutokuwepo: ni hali kapa (null) inayowakilisha kinyume cha uwepo. Kutokuwepo ni hali pacha iliyojishikiza kwenye uwepo kwani kusingekuwa na uwepo basi hata neno hili lisingekuwepo.

Usingekuwepo ni nani angelichukua nafasi yako? Elewa kuwa mwanadam ni maada tata (complex matter) ambayo huhitaji nafasi (space) na mda (time) katika kuwepo kwake, hapo sasa unaona kuwa kama wewe ni maada (matter) unahitaji nafasi ili uwepo, nafasi hii ina ukomo (finite space) ambayo ukomo wake hudhihirishwa na mda (time). Kwa hiyo katika logic huwezi kuwepo bila kuwa na nafasi na mda.
Hakuna hoja yoyote itakayoidhinisha nafasi yako pamoja na mambo yako kuwa yangefanywa na mwingine kama Usingekuwepo. Ukiwepo wewe ndio nafasi yako ambayo baadae itaisha kwa sababu ya mda kwenda mbele ndipo utatoweka.
Kama usingekuwepo basi kusingekuwepo yoyote ambaye angeyafanya unayoyafanya kwa sababu haupo.
No alternative to such paradoxical propositions, if you weren't present, no one could have performed a duty of an absent subject.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom