SoC04 Kuwekeza kwenye Teknolojia kwa kutumia vyuo vyetu kuyasogelea kwa Karibu Mapinduzi ya Nne ya Viwanda

Tanzania Tuitakayo competition threads

Benjamin9911

Member
Mar 8, 2018
6
10
Tanzania kama tunavyojiita kuwa ni moja ya Nchi zinazoendelea, hatuwezi kukwepa kujiingiza moja kwa moja kwenye MAPINDUZI YA NNE ya viwanda.

Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, ni mapinduzi makubwa ya kiteknolojia ambayo yanaendelea hivi sasa, na yana athari kubwa kwa biashara na jamii kote ulimwenguni, ndipo uchumi wa Dunia ulipo kwa sasa. Mapinduzi ya Nne ya Viwanda inajulikana kwa kujumuisha teknolojia kadhaa tofauti, ikiwa ni pamoja na akili bandia (Artificial Intelligence), roboti (Robotics), Mtandao wa Vitu (Internet of Things), na data kubwa (Big Data). Teknolojia hizi zinabadilisha jinsi tunavyoishi, kufanya kazi, nakuingiliana na ulimwengu unaotuzunguka.

Hivyo kama nchi tukitaka kukimbia mbio pamoja na dunia katika mapinduzi haya, yatupasa kuweka mipango madhubuti kwenye mitaala ya Sayansi kuanzia shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ufundi, Vyuo vya kati na Vyuo vikuu, ili watu wetu waelewe ni wapi tunapaswa kwenda. Ikiwa ni pamoja na kujifunza kwa vitendo zaidi na kufanya uhalisia wa vitendo kwa kutengeneza Mifumo, Sakiti na vifaa mbalimbali vya kiteknolojia, ikiendana na kuwapa kipaumbele na kuruhusu teknolojia nyingi zinazobuniwa na wanafunzi vyuoni, mathalani TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM, CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA na Vyuo vyote vinavyotoa kozi za ufundi na Teknolojia.

Iwe ni lazima mwanafunzi kufanya Bunifu zenye tija ambazo zitasaidia kutatua changamoto iliyopo kwenye jamii yetu, ili Bunifu hiyo kweli iingie kwenye soko baada ya mwanafunzi husika kuifanya na kuwa ndio ajira yake.

Kuna Bunifu nyingi zenye kutatua changamoto halisi ambazo wanafunzi wameshazifanyia kazi yaani wametengeneza Mifumo, Sakiti au Vifaa mbalimbali kwa aidha kifaa halisi au "Prototype" lakini kwa bahati mbaya zimewekwa kwenye stoo za vyuo bila kuendelezwa, hali hii inawavunja moyo wanafunzi na hata walimu. Na hivyo kupelekea baadhi ya wanafunzi kufanya Bunifu ili kutimiza takwa la chuo kuweza kupata Cheti na kurudi mtaani kusaka kuajiriwa.

Baadhi ya bunifu ambazo Mapinduzi ya Nne ya Viwanda yametupa ni Akili Bandia kwenye uzalishaji viwandani, Kilimo, Biashara Mtandaoni, hivi sasa unaweza agiza kitu China ukiwa Ruangwa, Lindi na kikafika eneo ulipo kwa uharaka zaidi ni pesa yako tu. Kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu. Hayo ni baadhi ya mambo chanya kwenye Mapinduzi haya ya viwanda. Pia Mapinduzi haya yamekuja na changamoto hasi ikiwemo baadhi ya ajira kutoweka, kuporomoka kwa maadili n.k.

Ushauri kwa Serikali na wadau wa sekta ya Sayansi na Teknolojia, kuwekeza zaidi kwa Bunifu zinazofanyika kwenye vyuo vyetu ili kuziendeleza pamoja na kumuendeleza Mbunifu wa teknolojia husika aifanye teknolojia aliyobuni kuwa Ajira yake ya kudumu. Pia Wizara husika, ione sasa ulazima wa kurekebisha mitaala ili tuweze kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia, tuondoke kule kwenye elimu ya kizamani ya kukariri, sasa twende kwenye kujenga uelewa kwa vijana wetu waweze kupambanua mambo na kufikia majawabu kwa kutumia mazingira yetu halisi. Tumfanye kijana wa kitanzania akimaliza chuo atoke pale anajua anakwenda kufanya nini mtaani na sio kuanza kuzunguka na bahasha, mwisho wa siku wanaishia kucheza kamari, madawa ya kulevya na mambo mengine mabaya. Ambayo yanasababishwa na msongo wa mawazo wa kutokuwepo kwa ajira. Pia tusisahau kwenye mitaala yetu kukazania somo la Maadili, Nidhamu na Uwajibikaji.

Pia sekta binafsi zitoe nafasi ya kujifunza kwa wanafunzi kwenye maeneo yao ya uzalishaji, ambako huko sasa wanafunzi watakutana na hali halisi ya Teknolojia iliyopo Duniani kwa eneo analisomea. Hapo sasa mwanafunzi akiunganisha yale aliyofundishwa chuoni kwa vitendo na akafaulu vizuri na kile alichojifunza kwenye maeneo ya uzalishaji, basi lazima kijana huyu atakuja na wazo la kibunifu zuri na lenye tija kwa jamii.

Hapo tutakuwa tumemaliza matatizo ya Ajira na pia tutakimbia mbio kwa kasi ambayo dunia inakimbia, na Uchumi wa Tanzania yetu utakuwa kwa kasi ya 6G (100gbps).​
 
Nice topic mkuu, bado Tanzania haijajua ku harness maarifa yanayotokana na research, hii ndio changamoto kubwa. Mimi nahisi kukiwa na body specific ya serikali inayo deal na bunifu za vyuo vikuu pennine itasaidia. Bodi itoe prizes kwa research nzuri na isaidie kutoa changamoto za matatizo tunayoface ili wanafunzi waje na solutions kupitia research. Nimependa pia ushauri wako wa kutoka kwenye elimu ya kukariri iende kwenye uelewa zaidi, ila hili linahitaji msingi kuanzia huku chini watoto wafundishwe kuongeza maarifa kwa kusoma vitabu vingi tangia wadogo. Nimekupa vote mkuu.
 
Nice topic mkuu, bado Tanzania haijajua ku harness maarifa yanayotokana na research, hii ndio changamoto kubwa. Mimi nahisi kukiwa na body specific ya serikali inayo deal na bunifu za vyuo vikuu pennine itasaidia. Bodi itoe prizes kwa research nzuri na isaidie kutoa changamoto za matatizo tunayoface ili wanafunzi waje na solutions kupitia research. Nimependa pia ushauri wako wa kutoka kwenye elimu ya kukariri iende kwenye uelewa zaidi, ila hili linahitaji msingi kuanzia huku chini watoto wafundishwe kuongeza maarifa kwa kusoma vitabu vingi tangia wadogo. Nimekupa vote mkuu.
Nashukuru sana, ndio maana nimeshauri Wizara husika na wadau wa elimu tuanze kufanya maboresho kuanzia chini ili kutengeneza watu wenye uelewa mpana wa kuyapatia majawabu ya changamoto tulizonazo kama taifa.
 
Mapinduzi ya Nne ya Viwanda inajulikana kwa kujumuisha teknolojia kadhaa tofauti, ikiwa ni pamoja na akili bandia (Artificial Intelligence), roboti (Robotics), Mtandao wa Vitu (Internet of Things), na data kubwa (Big Data). Teknolojia hizi zinabadilisha jinsi tunavyoishi, kufanya kazi, nakuingiliana na ulimwengu unaotuzunguka.
Hivi tupo tayari kweli kwa hizi vitu. Mmmmh Mungu atusaidie.

ni lazima mwanafunzi kufanya Bunifu zenye tija ambazo zitasaidia kutatua changamoto iliyopo kwenye jamii yetu, ili Bunifu hiyo kweli iingie kwenye soko baada ya mwanafunzi husika kuifanya na kuwa ndio ajira yake.
Hivi ndivyo tunajenga taifa pamoja. Bunifu zenye matunda moja kwa moja.

Hapo tutakuwa tumemaliza matatizo ya Ajira na pia tutakimbia mbio kwa kasi ambayo dunia inakimbia, na Uchumi wa Tanzania yetu utakuwa kwa kasi ya 6G (100gbps)
Hii ni kali asee 100gbpee second!!!.
Nisaidie na elimu kidogo je 3g ni gani 4g ni gani na 5g ni ngapi kwa hesabu hizo za gbps... samahani nje ya mada kidogo lakini ndio tunajifu za hivyo
 
Hivi tupo tayari kweli kwa hizi vitu. Mmmmh Mungu atusaidie.


Hivi ndivyo tunajenga taifa pamoja. Bunifu zenye matunda moja kwa moja.


Hii ni kali asee 100gbpee second!!!.
Nisaidie na elimu kidogo je 3g ni gani 4g ni gani na 5g ni ngapi kwa hesabu hizo za gbps... samahani nje ya mada kidogo lakini ndio tunajifu za hivyo
Pamoja sana Kaka. 2G ni 64Kbps, 3G HSPA+ ni 8Mbps, 4G LTE ni 50Mbps na 5G ni 10Gbps. Hiyo 6G bado wako kwenye stage ya Prototype na ndio kasi yake wametest 100Gbps. Asante. JIFUNZE ZAIDI HAPA https://www.rantcell.com/comparison... packet switching, the,bandwidth of 15-20 MHz.
 
Back
Top Bottom