LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
Personal Fınance,

Hili ni somo muhimu sana ambalo kila mwanadamu angeweza kuliishi basi tungekua tumefanikiwa kuwa na uhuru wa kifedha kwa asilimia kubwa sana.



Personal Finance ni uwezo wa mwanadamu kutenga pesa kwaajili ya matumizi yake ya sasa na ya baadae.



Tunashauri mtu afate njia ya 50%, 30% 20%

Inamaanisha kipato chako unachokipata either ni kwenye biashara au mshahara ukigawe kufata hizo asilimia.

50% ya kipato ni ya kufanyia matumizi muhimu kama kulipa kodi ya nyumba, kodi ya jengo la biashara, nauli ya kukufikisha kazini au sehemu ya biashara nk



30% hii ni kama emergency fund ambayo utatumia mfano imetokea harusi ama msiba utahitajika kuchangia, laptop yako imeharibika, simu imepotea, umeamua kuji zawadia kwa zawadi nzuri, umeamua kuhonga nk



20% hii ndio unayotakiwa kuitunza, usahau kama hii pesa ni yako, sasa kwa waTanzania wengi hii sehemu ni ngumu.

ni ngumu kujisahaulisha kama una pesa na unajua unayo, ni ngumu upatwe na changamoto na usiiguse.

ushauri:

20%

1.fungua fixed account iweke huko kuanzia mwaka mzima na zaidi,

2.Fungua account ya UTT Amis au nenda DSE ulizia ni kampuni gani inafanya vizuri wekeza huko.

3.Nunua line ya simu ambayo unaweza ukampa mtu mwengine akushikie unayemuamini, weka pesa huko tunza kwenye m koba kibubu, au airtel money kibubu, au tig pesa kibubu utafaidika na gawio.

4. Kanunue ardhi (shamba ama kiwanja)



mimi nashauri 50% 20% 20% 10%

ambayo asilimia 50 inaendana na hio hapo juu,

20% iendane na 30%

20% nyengine iendane na 20%

alafu 10% ya mwisho ni mpya..

hii iwe ile pesa ambayo upo teari ku take risk nayo,

namaanisha hii iweke kwenye biashara.

kama genge, kuuza maji officini, kuuza juice, kuuza ma T shirt , wallet nk

biashara ambayo haigharimu mtaji mkubwa.

karibuni sana, ningependa kupata comment zenu.Asanteni sana.

#personalfinance #comment #money #DSE #UTTAMIS #stocks #risktaking #budgeting #elimu #biashara #lovintah
personal-finance.png
 
Sasa 50 matumizi
30 Dharula
20 Saving

Mtaji hapo upo wap? Au hizo ni faida?
 
Sasa 50 matumizi
30 Dharula
20 Saving

Mtaji hapo upo wap? Au hizo ni faida?
Hii kitu tunaongelea kwamba teari biashara imeshaanza, kwaio kwenye 50% ni zile gharama za uendeshaji wa biashara kama kulipa kodi, marekebisho, kuongeza stock nk

Ila kwa mtu ambae anafanya kazi na hana biashara ndio 20% ya saving itamfanya apate mtaji wake anaouhitaji kuanzisha biashara kwa miaka ya badae.
 
Back
Top Bottom