Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Shakir

JF-Expert Member
Jul 31, 2012
1,602
1,819
Wakuu Kwema?

Mimi kwa kiasi fulani ni mdau wa mafuta, kwani hapo kabla miaka ya nyuma nilishawahi kufanya kazi katika kampuni ya mafuta Kwa kama miaka kadhaa Hivi

Hivi karibuni Mbunge wa Gairo Bw. Ahmed Abdallah Shabiby amependekeza kua ili Bei ya mafuta iweze kushuka basi Serikali iruhusu Wafanyabiashara binafsi waagize mafuta hayo.

Napenda kuweka taarifa sawa tu kua Utaratibu huu anaoupendekeza Bw. Shabiby utumike ndio uliokuwepo hapo awali. Serikali ilikuja kuubadilisha huu utaratibu kutokana na sababu au mapumgufu yake kadhaa, na chache nitazitaja hapa chini.

Kwanza ni ku avoid "Transfer Pricing". Yaani kampuni A iliyopo Tanzania ni tawi la Kampuni B iliyopo labda S.A. Sasa kampuni B ndio inayonunua mafuta inakokujua kisha inaiuzia kampuni A ya hapa nchini kwa bei kubwa kuliko bei ya soko.

Sasa kampuni A ya hapa katika hesabu zake za kodi ya faida 30%x (Mapato - Matumizi) inajikuta inalipa kodi kidogo sababu gharama za uendeshaji zimekua kubwa kutokana na gharama kubwa za manunuzi ya mzigo. Kwa mtindo huu kampuni zingine hufikia hata kuandika wamepata hasara (Manunuzi + Gharama zingine vimezidi Mapato). Kifupi kampuni hukwepa kodi kwa kusingizia gharama kubwa za manunuzi kumbe humo humo anapomlipa Kampuni Mama na faida au dividend anasafirishia hapo hapo kinyemela.

Sababu ya pili Mpaka Serikali ikaondoa utaratibu huu ni kufaidi "Discount on Bulk Purchases". Yaani kampuni 10 zikinunua labda lita million 10 kila moja ni tofauti na kampuni moja ikinunua lita 10mil x 10 = Lita 100mil. Huyu anaenunua lita nyingi ni rahisi ku bargain na kupewa Discount kubwa tofauti na yule anaenunua kidogo. Discount hiyo hupelekea unafuu wa bei Mwishowe kwa finale user.

Tatu ni kua na records za mafuta yaliyoko nchini. Yaani soko likiwa holela kila mtu anaagiza mnaweza kushindwa kujua hata mahitaji ya nchi kwa kipindi husika ni kiasi gani. Hii pia huwezesha Serikali kukadiria (bajeti) Kodi itakayokusanywa kutokana na mafuta haya.

Nne ni kupata bidhaa iliyo bora na standard. Kutokana na Bei mbalimbali zinazosababishwa na ubora mbalimbali basi wengine wanaweza kuchukua au kuagiza hata yale yenye ubora wa chini sababu tu ya unafuu wa bei bila kujali athari zake kwenye matumizi yake. Standard hapa ni viwango vifanane kati ya kampuni moja na ingine. Kusiwe na tofauti kati ya anaejazia BP/Puma au yule anaejazia Oilcom (Ceteris Peribus).

Tano ni kuondoa mafuta ya magendo kwenye soko. Since Mnunuzi wa kutoka nje atakua ni mmoja tu na ndie atakaewasambazia Makampuni ya ndani then kunapunguza uwezekano wa mafuta mengine yasiyolipiwa ushuru kuingia kwenye soko.

Sita, Kwa kuagiza pamoja kunaleta uniformity kwenye Bei. Ingawa Labor na Other Overhead Expenses zaweza kua tofauti lakini bei ya kununulia bidhaa ambayo ndio huchukua sehemu kubwa ikiwa sawa basi Bei hazitapishana sana. Ingawa bei Hupangwa na Ewura lakini kipindi hicho huu utaratibu unawekwa ni Makampuni yenyewe yalikua yanajipangia Bei baada ya kukukokotoa Gharama mbalimbali za kuanzia Manunuzi na Undeshaji pia.

Saba, Kuzuia kuficha mafuta. Kampuni zingeweza kusema hazina mafuta (lower supplies) ili kutengeneza Demand kubwa then bei zipande. Lakini since uagizaji na/kisha ugawaji wa mafuta hufanywa Kwa pamoja then ni rahisi kujua stock ya kila kampuni. Hivyo si rahisi kwa Kampuni husika kuficha taarifa za mafuta iliyo nayo.

Sababu zilikuwa nyingi, nimejaribu kukumbuka chache. Inawezekana mazingira ya wakati ule yangechochea tuhamie kwenye uagizaji wa pamoja labda sababu hizo sio valid anymore so turudi tu kule kule tena. Nimeona kama (nilieliekua) mdau wa mafuta basi nisikae kimya watu wafikiri kua hatujawahi kua katika huo utaratibu alioupendekeza Bwana Shabiby.

Muwe na Siku njema.
 
Sasa ndugu mdau hebu tueleze . juzi tumeambiwa mafuta yapo ya kutufikisha siku 27. Lakini juzi ewura wametangaza bei mpya na zimeanza kutumika hapohapo , kwanini isingesubiriwa hizo siku 27 ziishe Ndo bei zibadilike?
 
Serikali itafute njia ya kuwabana kwenye mapato sio kuongeza gharama zisizo za lazima kwa watumiaji mafuta.

Shabiby amesema pia mita ya mafuta bandarini imeharibika mara nyingi zaidi baada ya kuingia mfumo wa BPS kuliko kabla haujawepo!
Tafuta Bei za 2011 kurudi nyuma, anachosema shabiby ni kweli Ila serikali ilikua inashindwa kuwabana kwenye mapato.
 
sasa kama serikali ya tozo inategemea kuvuna hela humo humo kwenye mafuta unategemea waruhusu watu binafsi kujiagizia wenyewe? haya mambo hayahitaji digirii kujua tatizo lilipo, nilishawahi kusema mtu kama mwigulu anakuaje waziri w fedha, for God sake how?
 
Hao akina Shabiby ndio walisababisha bei ya kerosine ikawa juu hadi leo kwa sababu ya mambo yao ya " kuchakachua" mafuta.

Usidanganyike kirahisi rahisi bwashee!

Kwa nini kuandikia mate? Shabiby anaahidi bei kupungua chini ya 50%?

Kwanini asipewe nafasi kama Masudi Kipanya ku prove gari lake la umeme?
 
Back
Top Bottom