Kuweka ndani mtungi wa gas ya kupikia, inakuwaje?

HAKUNA

Senior Member
Mar 12, 2012
133
66
Wana Jamii, matumizi ya kupikia kwa gesi yamezidi kuongezeka; nimekuwa nikiona watu wengi wanaweka mitungi ya gas ndani, vipi hakuna hatari yeyote?, je hakuna sheria iliyoweka kwa watumiaji wa gas majumbani kwa ajili ya usalama?. Nimekuwa nikiona nchi nyingine mitungi ya gas ikijengewa nje.
 
Asante kwa kutukumbusha. Ni makosa makubwa kuweka mtungi wa gas ndani. We are not conscious of fire safety rules
 
Gesi ya siku hizi sio kama ya zamani, utashangaa unaweza fungua gesi kabula hujawasha na ukawasha kusiwe na tatizo, ni kama petrol ya zamani na ya siku hizi,

Kama kuweka ndani ni makosa vipi ILE MITUNGI YENYE JIKO HAPO HAPO? WATU WAWE WANAPIKIA NJE?

asante sana KOMANDOO kwa majibu mazuri

labda hatari inaweza kuwa ikivuja (leak) wakati wa usiku watu wamelala inaweza sababisha ugumu wa kupumua na watu waka suffocate
 
Gesi ya siku hizi sio kama ya zamani, utashangaa unaweza fungua gesi kabula hujawasha na ukawasha kusiwe na tatizo, ni kama petrol ya zamani na ya siku hizi,

Kama kuweka ndani ni makosa vipi ILE MITUNGI YENYE JIKO HAPO HAPO? WATU WAWE WANAPIKIA NJE?

Umenena vyema KOMANDOO
OTIS
 
Last edited by a moderator:
Gesi ya siku hizi sio kama ya zamani, utashangaa unaweza fungua gesi kabula hujawasha na ukawasha kusiwe na tatizo, ni kama petrol ya zamani na ya siku hizi,

Kama kuweka ndani ni makosa vipi ILE MITUNGI YENYE JIKO HAPO HAPO? WATU WAWE WANAPIKIA NJE?

Haya uliyonena yanatokana ta taaluma juu ya gesi au nadharia ya jumla, naomba ufafanuzi kwa anayefahamu.

KOMANDOO - Ulishawahi kufanya majaribio ya kufungulia gesi kwa muda halafu ukawasha kiberiti? Maana naona kama unazungumzia mambo ya kikomandoo zaidi kuliko uhalisia wenyewe.
 
hapo utakuwa unayatafuta matatizo wewe mwenyewe na wala haitakuwa ajali ... kila kitu kikitumika vibaya kina madhara ... hata chakula unavimbiwa
 
hapo utakuwa unayatafuta matatizo wewe mwenyewe na wala haitakuwa ajali ... kila kitu kikitumika vibaya kina madhara ... hata chakula unavimbiwa

LAT, ndio maana nilitaka kufahamu kama kuna jaribio ambalo limeshawahi kufanyika na kuthibitisha kwamba gesi ya siku hizi ni tofauti na zamani, kwamba hailipuki. Hapa ninachotaka kufahamu ni kama madhara yanaweza kuwepo, ikitokea kuvuja kwa gesi na je serikali kuna sheria yoyote imeweka juu ya matumizi ya gesi nyumbani au kuna chombo chochote cha uthibiti na kuhakiki kwamba watumiaji wa gesi nyumbani watakuwa salama kwa vipengele hivi na hivi au tunajiendea tu kama kondoo waliokosa mchungaji........!!!, watu tunatofautiana uelewa na mazingira tunayoishi, kwa sasa matumizi ya kupikia kwa gesi yamekuwa makubwa tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni kwa wachache tena wenye nazo.
 
Kwa vyovyote vile (nje au ndani) kuna hatari. Cha msingi ni hatari kiasi gani? Je hii hatari inabebeka? Kwa muundo wa mtungi wa gesi na matumizi ya nyumbani (domestic) kwa maoni yangu nitasema ni hatari ambayo inabebeka kwa sababu sio rahisi mtungi huo kupasuka.

Na kwa kweli hatari kubwa zaidi sio ya mtungi kupasuka bali ni zile valves au pipes kuvuja au watumiaji kuruhusu gesi kutoka (bila kuwasha jiko) kwa muda. Kwa hiyo hata kama mtungi upo nje lakini jiko unalopikia limo ndani na gesi inapita kwenye pipe kuja kwenye jiko la gesi bado hatari zipo palepale kwa kuwa ni rahisi zaidi kwa pipes hizo kuharibika/kuharibiwa na kuruhusu gesi kutoka.

Kama lengo ni kupunguza hatari zaidi, then inabidi hata kupikia (au matumizi mengine ya gesi) yafanyike nje ya nyumba.
 
cha msingi hapa ni elimu izidi kutolewa kuhusiana na matumizi ya gas. mtu anapofika maamuzi ya kununua cooking gas lazima atakuwa na uelwa kiasi fulani ambao ataupitisha kwa wanafamilia wake. mpaka sasa nyumba zinazoungua kwa hitilafu ya umeme ni nyingi kuliko zinazoungua kwa makosa ya kupikia gas

pili angalia issue ya wizi cylinder ya gas ikiwa imeja gasplus regurator inalala nje huku uswazi vibaka watatusalimisha kweli?
 
Ni hatari na makosa kuweka mtungi wa gas ya kupiki ndani ila serikali yetu haina sheria yoyote inayohusu matumizi ya gas na hiyo ni kwasababu kulikuwa na matumizi madogo sana ya gas siku za nyuma na hakujawahi kujitokeza hatari kubwa ya maafa kutokana na gas zinazotumika majumbani kutokana na kuvuja au kupasuka kwa mtungi. Ni vizuri mtungi wa gas ukawekwa nje ya nyumba kwa kujengewa kichumba chenye matundu mengi au au nondo na pipe zake zikatengenezewa kava ya ulinzi pia mpaka kwenye muunganiko na jiko. Gas inamadhara sio ya kuwasha moto tu bali pia haifai kuvutwa na mnyama wa aina yoyote endapo itatokea kuvuja.
 
Mimi naweka ndani lakini hii mada imenifungua zaidi. Nitakachcofanya ntanunua fire extinguisher kupunguza madhara pale yatakapotokea
 
Gesi ya siku hizi sio kama ya zamani, utashangaa unaweza fungua gesi kabula hujawasha na ukawasha kusiwe na tatizo, ni kama petrol ya zamani na ya siku hizi,

Kama kuweka ndani ni makosa vipi ILE MITUNGI YENYE JIKO HAPO HAPO? WATU WAWE WANAPIKIA NJE?
Mkuu acha kupotosha watu.
 
juzi nilikuwa naangalia matengenezo ya labaratory moja ya shule ya secondari nikapenda uwekaji wa gas yao mtungi upo nje na niamuuliza fundi kama inawezekana kufanya nyumbani akasema inawezekana kwa kweli ni salama zaidi. by the way kwa niaba ya serikali ya wadanganyika napenda kutoa shukrani zangu kwa nyinyi wenyewe kuliona hili na tutegemee sheria mpya kuhusiana na usalama majumbani itatekelezwa kwa kila mwenye gas awe na mtungi wa kuzimia moto halafu usipo kutwa nao fine na lazima ukanunue sehemu iliyothibitishwa na serikali hivyo tujiandae kulipa ada za ukaguzi kila mwaka pamoja na stika
 
Ni hatari na makosa kuweka mtungi wa gas ya kupiki ndani ila serikali yetu haina sheria yoyote inayohusu matumizi ya gas na hiyo ni kwasababu kulikuwa na matumizi madogo sana ya gas siku za nyuma na hakujawahi kujitokeza hatari kubwa ya maafa kutokana na gas zinazotumika majumbani kutokana na kuvuja au kupasuka kwa mtungi. Ni vizuri mtungi wa gas ukawekwa nje ya nyumba kwa kujengewa kichumba chenye matundu mengi au au nondo na pipe zake zikatengenezewa kava ya ulinzi pia mpaka kwenye muunganiko na jiko. Gas inamadhara sio ya kuwasha moto tu bali pia haifai kuvutwa na mnyama wa aina yoyote endapo itatokea kuvuja.

Mkuu umenena, kwa sababu hapoa awali watumiaji walikuwa wachache. Jamii yetu ni ignorant sana katika mambo ya msingi tunasubira mpaka madhara yatokee ndipo watu wanaanza kuzungumzia jambo husika; watu wanapenda majibu mepesi kwa maswali magumu, kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakiweka mtungi wa gesi ndani basi wanataka kuhalalisha kwamba kufanya hivo hakuna madhara. Nafikiri jamii na serikali inapaswa kuliangalia hili kwa makini kutokana na kuongezeka kwa watumiaji gesi, kwa mfano sasa hivi unaweza kukuta nyumba ya kupanga yenye vyumba takriban 8 na kila mmoja ameweka mtungi wa gesi ndani, unafikiri nini kitatokea endapo katika chumba kimojawapo kutatokea linkage ya gesi. Let us take it serious, something gonna happen...............!!!!!
 
Chance za mtungi kuleta madhara yoyote ukiwa ndani ni next to zero. Chance za kuleak hazitegemei mtungi uko nje au ndani, ili mradi jikoni kwako kuwe na ventilation ya kutosha (dirisha) sio rahisi gesi ikasababisha madhara yoyote makubwa. Pia gesi inawekwa harufu makusudi ili kukiwa na leak unaweza kujua mara moja.
 
Hata ukiweka nje kunaweza kukawa na leakage kwa ndani ya nyumba. Cha muhimu ni kuwa mwangalifu wakati wa kutumia. Siku hizi gas ina harufu ambayo ni rahisi kujua ikitokea kuvuja. Ventilation pia ni muhimu. Kubadilisha hose pipe mara kwa mara kama unatumia hose badala ya kopa.
Kama una nafasi na ulinzi kuweka nje ni vizuri zaidi.
 
lakini je tunajua maana ya namba zilizopo kwa juu ya mshikio wa mtungi mfano D12?
 
Back
Top Bottom