Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,935
- 6,844
Wakati kumpendelea mtz mweusi kwa hila itakuwa ni jambo baya, imefika mahali sasa ili mbele ya safari tusijejiingiza kwenye migogoro, kuwe na upendeleo maalumu wa kuwasukuma watz weusi ili nao wawe players katika uchumi wetu. Mfano, kazi nyingi za ujenzi zinataka mitaji mikubwa ambayo kampuni nyingi za wazawa hazinao. Badala ya kuwapa kila kazi ya ujenzi kampuni za watz wa kiasia/kizungu kama estim, daikin,barkeley electric,caspian etc kwasababu wana mitaji, kuwe na namna ambayo kampuni nyingine ndogo zinapewa guarantee za mitaji zinapopata kazi kama hizo kutoka kwa mabank na institution nyingine za fedha. Hilo kwa sasa halipo.
Halafu hawa watz wa kiasia na kizungu faida kubwa huwa inapelekwa nje wanakokuona ni safe. Pengine wasiwasi unatokana na sababu kuwa walio wengi ambao ni weusi hawana...itakuwaje wakiwabadilikia mbele ya safari!!
Tusisahau tuliwanyang'anya hao tunaowaita wageni kila kitu tukapeana wazawa! Kuanzia mashamba ya wagiriki, mabenki, nyumba za kupanga, makampuni binafsi etc etc. Tukachukua, tukayafilisi halafu tukataka kuwarudishia wageni. Makandarasi wazawa wengi walipewa kandarasi, wakashindwa. Mahoteli vile vile tukawapa wazawa kwa bei ya kutupa, nayo wameyafilisi! Sasa tunataka tuwezeshwe vipi?
Ukweli ni kuwa hakuna njia ya mkato katika maendeleo ya dhati. Tujifunge mikanda, tusikimbie umande n.k. na siku moja tutafika.
Amandla.........