Kuwawezesha wabongo weusi! - Wazo hatari?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,694
40,720
Nimeona niandishe mada nyingine ambayo haihusiani hasa na viongozi lakini kwa namna fulani inatugusa. Huko Nyuma, Mzee Iddi Simba alikuja na hoja kuwa kama kweli Tanzania inataka ipige hatua kubwa ya maendeleo hatuna budi kuja na sera za kujali wazawa( akimaanisha Watanzania weusi...). CCM ilikataa maneno hayo kitu kilichochangia kuanguka kwa mzee Simba kwenye medani za kisiasa. Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na makala ya kiingereza iliyoandika na Adam Lusekelo wa Daily News kuhusu kuwapa nguvu watu weusi raia wa nchi yetu!! Makala yenyewe hii hapa:

_____________________________________________________________
HEARD our prez, Jack (I didn't know the nickname of Jakaya is Jack - Mwanakijiji) Mrisho, say that given the empowerment, Tanzanians are quite good at doing business and making their bones in life.

I agree. But I would have liked the prez to add what would have touched the other word which Tanzanian political establishment have shied away from - B - word. Black Tanzanians. Black empowerment!

Because we have seen the much-played around word of people of Bongo. Tanzanians. It seems that some Tanzanians are more equal than other Tanzanians and that is based on colour.

It is just like in the colonial times. White Tanzanians come tops in everything, finances and opportunities. They come even tops in meeting the big potatoes. Which is understandable, bearing the latent inferiority complex of most of our leaders.

Then come in Tanzanians of Indian descent. They have been holding most of the money. Some people, including some leaders, want some of the dosh to go to build silly looking mansions (call them pyramids) somewhere. Presumably they will be buried in the mansions.

Then comes in the scandalous poverty amongst the black Tanzanians. If the prez meant empowerment, he should then talk about Black Tanzanian empowerment.

In Sausi, they talk openly about Black empowerment in a country where the mass of the population has been brutalised and raped over decades. Why shouldn't we?

In Mchuchuma I hear funny names. In all the mines I hear funny names, never heard before in my life. When the figures of income derived from the mines are read out it's from wa-zungu Tanzanians. Can't Black Tanzanians read? Should the so-called investors be white or, as the press put it, Tanzanians of Asian origin only?

Because, really, this is insulting to us, Blacks. I once heard a remark by some clownish minister (he still is a minister. Sad) that Black Tanzanians were not trained to do business.

Some ministry of education idlers even removed subjects like commerce from the curricula.

You simply wonder if those guys had something from their necks upwards. In history, we learnt that many Mediterannean countries had what they called city-states. They were powerful and lived on commerce. Look at Zanzibar when the rule of Seyyid Said Bin Sultan started. But he empowered fellow Arabs.

The politicians have been pooh-pooing what Mzee Iddi Simba has been saying about 'Uzawa'. He was simply talking about Black empowerment. He is not wrong. We want to see Black Tanzanian businessmen and women. We want them being millionaires. Privatising should not be 'whitening' of public corporations in Bongo!

_____________________________________________________________

Mawazo yangu kwanza baada ya kusoma makala hiyo ni kuwa huyo Lusekelo aachie ngazi, hawezi kusema maneno aliyoyasema hapo juu bila ya kuonekana mbaguzi!! Sijui kama kuna ulazima wa sera ya namna hii, na ni jinsi gani sera kama hii inaweza kutekelezwa bila kuleta athari za ubaguzi!! Hata hivyo bado najaribu kufikiri kwa kufuata mfano wa Afrika ya Kusini na Marekani labda hoja yake ikiwekwa katika kusaidia Watanzania Maskini bila ya kujali rangi zao itakuwa na maana zaidi!!
 
Mzee M,

Binafsi sijui kama nimekuelewa, isipokuwa nitasema kuhusu Idd Simba ni kwamba unapokuwa mwanachama wa CCM na tena kiongozi kama alivyokuwa yeye, ni lazima uwe mtekelezaji mzuri wa maadili ya chama,

Sasa Simba alikuwa anelewa wazi kwamba huwezi tu ukaibuka na dhana au sera zake bila ya kukubaliana na CCM kwani ni kukiuka miiko ya chama chako, as the results hata kama sera yako ni nzuri kwa taifa itaishia kukataliwa kwa sababu tu ya kukiuka miiko ya chama chako,

Simba alipaswa kuwafahamisha CCM katika vikao vyao kuhusu sera zake hizo mpya, kama wangelimkatalia basi angejitoa katika CCM, na kuanzisha chama chake chenye sera za uzawa, huo ndio moyo wa kulisaidia taifa lako, I mean the man kwanza sio mbongo, halafu ni mwanachama wa CCM ambao wanajua fika kuwa sio mbongo ila wanamlinda tu kwakuwa ni mwenzao, sasa tena na haya ya uzawa, please! Basi hata angempa hiyo sera Mtikila baada yakuona anashindwa kuwa convince CCM,

Kwa sababu no Question kwamba hii sera ikiwekwa vizuri sidhani kama kuna sera ya kuwaamsha wananchi usingizini kama hiyo, the matter of fact hii ndio iliyokuwa kiini cha mafanikio ya mzee Clinton kule US,

lakini Simba kwa maoni yangu alikuwa mbinafsi na arrogant mno, kiasi kwamba asingeweza kusikiliza la mtu yoyote yule, yeye alipewa uwaziri baada ya kuiongoza ile tume ya rais ya kufuatilia malalamiko ya Mrema kwamba Ben, Mbilinyi, na Mporogomyi walikuwa wamevuta shillingi millioni mia tano katika kuwaachia wavua samaki wakubwa huko Mwanza wasilipie kodi minofu hiyo ya samaki, yeye na Masilingi ndio waliokuwa viongozi wa hiyo tume, sasa cha ajabu ni kwamba baada ya uchunguzi wa miezi kama minne, wakagundua kuwa Mbilinyi na Mporogomyi aliyekuwa waziri mdogo wa fedha ni kweli walitia ndani pesa hizo, lakini wakasema kuwa mzee Ben hakuhusika, What a joke?

The next thing we know ni mawaziri, na anataka uzawa!
 
Mzee Es,

Shukrani sana kwa maelezo yako ambayo yamenipa mwanga mkubwa wa hii scandal ya samaki.
Kusema kweli, swala hili litaendelea kuwa hoja yangu kubwa ktk uongozi wetu na kwa maneno yako watu kama Idd Simba ni wasomi wazuri isipokuwa kosa lao kubwa - wasomi hawa ni Opportunistic.

Kwa maana hiyo hata hiyo sera ya Uzawa inabidi tuwaangalie sana watu hawa kwani wao ndio wa kwanza kufaidika na sera kama hiyo. Wanao uwezo na kila hali ya kuleta mabadiliko lakini wao sio viongozi wa kisiasa bali ni wafanyabiashara.

Sera ya Wazawa ni sera nzuri na dawa pekee ya umaskini wa mwafrika lakini haiwezi kuleta mabadiliko yoyote ikiwa viongozi wetu wataendelea kuruhusiwa pia kufanya biashara, hapa kila mmoja wao atakuwa na priorities zake.

Nikiwa kama Conservative, naamini kabisa kuwatajirisha wazawa kulingana na vipaji - elimu zao ktk mazingira yetu ndio njia pekee ya kuanza mabadiliko ya kiuchumi yenye sura halisi ya - nini maendeleo..
 
Mzee Es na Mkandara,
Kwa upande wangu mimi binafsi naona kuwa kwenye Taifa la watu wenye asili mbalimbali kutengeneza sera yenye kulenga rangi, kabila au dini ni kinyume na Katiba na ni kitendo hatari. Kutumia maneno Wazawa ni kuficha neno "Weusi". Binafsi sina tatizo na kuja na sera za kuwainua watanzania wote kiuchumi na kuwaleta kwenye mafanikio. Hata kam Simba angeweza kuwashawishi viongozi wa CCM sioni kama sera hiyo ingepata nafasi jinsi ilivyotolewa. Kuna tofauti kubwa kati ya Afrika ya Kusini, Marekani na Tanzania.

Kwa upande wa Marekani Kundi Kuu (weupe) ndo waliowanyanyasa na kuwakandamiza watu weusi kwa takribani miaka 400 na hata baada ya kutambua haki zao (weusi) kama raia miaka karibu 40 iliyopita bado kundi lile lile lina nguvu ya kiutawala. Kwa sababu hiyo basi, wao kuja na sera za kuwainua watu weusi ni jambo la kimantiki na ni kitendo cha kiutu kwani ni weupe waliofaidika na jasho la mtu mweusi. Lakini kwa jinsi wimbi la kisiasa na mafanikio ya kiuchumi yanavyoanza kuendelea sera hizo hatimaye zitajikuta zinatupwa nje na kuangalia uwezo, vipaji, na nafasi ya mtu badala ya rangi, na hivyo kuwalazimisha weusi kushindana na weupe katika uwanja sawa! Yameanza kutokea hayo kwenye elimu ya juu ambapo suala la rangi halitakiwi kuangaliwa kabisa!!!

Afrika ya Kusini ni tofauti (labda ni mfano mzuri kwetu), kundi la watu weupe lililowakandamiza watu weusi (Wengi) kwa karibu miaka 400 lilinufaika na jasho la watu weusi lakini hivi sasa halina uwezo wa kisiasa na nguvu ya kura hivyo limejikuta liko pembeni. Hata hivyo, kundi hilo la watu wachache haliwezi kufurahia matunda hayo ya ukandamizaji wakati lile kundi kuu likiendelea kusota katika umasikini uliokithiri. Ni kwa sababu hiyo basi, sera za "kuwawezesha watu weusi" zinahitajika na ni za lazima.

Kwa upande wetu Tanzania, weupe waliotutawala hawana nguvu yeyote ya kiuchumi au kisiasa, na waasia wachache walionufaika wakati wa ukoloni wana nguvu ya kiuchumi kuliko ya kisiasa. Kwa muda wa miaka karibu 45 Tanzania imetawaliwa na watu weusi na bila ya shaka itaendelea hivyo kwa muda mrefu ujao. Lakini ni chini ya viongozi weusi ndo umasikini umeongezeka na kukithiri!!! Hatuwezi kulalamikia wahindi wa leo kwa umasikini wetu! au wazungu waliopita kwa ufukara wa watu wetu!

Ni kwa sababu hiyo basi, kwa maoni yangu sera zenye kulenga umasikini wa watu wetu ndo sera zenye maana zaidi kuliko sera zenye kulenga rangi, kwani ukishaanzia kwenye rangi, tutajiuliza ni Kabila gani lenye watu masikini zaidi na tutafanye nini kuwawezesha watu wa kabila hilo? Na tusipoangalia tutaanza kuangalia (kama bado hatujaanza) ni dini gani yenye watu walionufaika zaidi na ni dini gani yenye watu masikini na tufanye nini kuwanufaisha watu hao. Hilo ni jambo la hatari. Ni kwa sababu hiyo sikubaliani kabisa na mantiki ya Adam Lusekelo kwani ndani yake imejaa ubaguzi, hisia ya ukuu, na haja ya kustahili!
 
Mwanakijiji,

Tunaweza kutafsiri hii issue kwa njia yeyote ile lakini ukweli utabaki kwamba UWAZA ndio njia pekee ambayo inaweza kumkomboa mwafrica. Swala la rangi limetumika CCM kutaka kuondoa maana kamili ya neno hili. Na kibaya zaidi ni kwamba walitumia neno weusi kuondoa uzito wa hoja nzima lakini mzawa ni yule mwenye asili ya sehemu hiyo tukiondoa kabila yake. Pwani na Dar-es Salaam kuna hesabu kubwa ya Wa manyema walizaliwa pale.

Salim anayo kila haki ya kujiita mzawa wa Pemba kama atakavyokuwa na haki mwarabu mwingine wa Singida, ama Idd Simba, Sykes na wengine waliokuja nchi kabla ya kupata uhuru wetu.

Swala la Marekani na ubaguzi halina usawa na kabisa na Uzawa wala hilo la South Afrika kwa sababu Muingereza pamoja weupe wake hana haki Marekani kama mweusi kisheria. Na wapo waingereza kibao wamerudishwa Uingereza kwa sababu hawana sheria ya kuhamia nchi hiyo.

Hakuna mtu ama kampuni ya nje inayoruhusiwa kuwekesha Marekani ktk mradi mkubwa kwa aslimia zaidi ya ishirini bila kibali maalum ambacho kinamfunga mgeni huyo bila kujali rangi ama kabila yake.

Je, Uzawa ni ubaguzi?... yes naweza kukubali na wewe, so is kuwa na mipaka kati ya nchi mbili, lugha tofauti kati ya mataifa. Kuwepo kwa passport, na vilevile kuorodhesha vyama vinavyohusu gender n.k.

Yote haya yanategemea na jinsi tunavyotaka kutafsiri Uzawa. Tunaweza kuwaita waarabu wa Egypt kuwa waafrika kwa sababu ya Uzawa ama tukawaita waarabu kwa rangi na lugha yao kisha kuwatoa nje ya Uafrika hali kati yao kuna weusi wanaozungumza lugha moja tu nayo ni kiarabu. Na huyohuyo mwafrika mweusi kama wewe akasema yeye ni mwarabu sii mwafrika.

Lakini tukizingatia Uzawa wa- Egypt wote weusi kwa weupe, makabila kwa makabila ni wazawa wa nchi hiyo na wewe mweusi mbantu toka Tanzania ni mtu wa kuja. Huna haki ya nchi hiyo hata chembe zaidi ya kuwaona waafrika wenzako. Mbona hatupiganii hilo na miaka kwa karne zimepita?

Jamani let's make things easier for us to move forward. Haya maswala ya kuongezea maneno na tafsiri za kupotosha ndiyo yaliyosababisha binadamu tuwe wagumu kuamini imani ambazo malengo yake ni kuokoka!..
 
mhhhh haya

duuuh....GT kwa purukushani tu, hujambo!
Hata baada ya miaka mitatu ( 7th June 2006, 03:53 AM -Today, 11:46 AM)....lol
Ngoja nami nitibue moja yako iliyosahaulika... je, unaweza ku-guess itakuwa ipi mkuu?!!! Ukipatia nitakutundikia picha moja ya kilatino bomba kichizi hata Fikirini amei-endorse!!
 
kama asemavyo FMES,angempa mtikila 'wa kipindi kile', achana na mtikila huyu aliyechukua 'mkopo' Caspian Construction

Lakini kwa mtizamo wangu ADAM is right!ninasema hivyo kwasababu 'i feel the impact' PRACTICALLY.nipo bongo huku!naona.GT anaweza kushuhudia namna 'watanzania-waasia' walivyoishika serikali hasa katika miradi ya ujenzi.

Miradi yoote inayoendelea Dodoma,kampuni ya mzawa kwa maana ya mzawa ni ELERAI,na ELECTRIC INTERNATIONAL!the rest ni wachina na wahindi,lakini ni local contractors.

I think ni lazima kuwe na 'special considerations' kwa kampuni za wazawa
 
ahhh nishaijua lakini jama naona jana waliileta but without much impact

unajua threads mpya zishatuishia sasa si mbaya tukaleta blasts from the past
 
Ukienda Dubai kufanya biashara kama si Mzawa hupewi leseni pale. Wanacho fanya wanatumia majina ya wazawa na wewe mfanyabiashara unamlipa mzawa kwa kutumia jina lake ndo maana utawaona muda wote wapo kwenye gahawa lakini serikali yao imewaona na kuwathamini wazawa kwanza kwa hiyo wao wanatengeneza fwedha kwa mgongo wa wakuja.
 
ahhh nishaijua lakini jama naona jana waliileta but without much impact

unajua threads mpya zishatuishia sasa si mbaya tukaleta blasts from the past

...the computer says NOO!
...umenoa hapo mazee, nitakayo ifukua yaani kama ni fossil basi inatoa mafuta tayari!!
 
Bila kuwawezesha kwa dhati watu weusi, ambao ndio wengi ktk nchi, hakuna maendeleo ya kweli.
 
Mzee Es na Mkandara,
Kwa upande wangu mimi binafsi naona kuwa kwenye Taifa la watu wenye asili mbalimbali kutengeneza sera yenye kulenga rangi, kabila au dini ni kinyume na Katiba na ni kitendo hatari. Kutumia maneno Wazawa ni kuficha neno "Weusi". Binafsi sina tatizo na kuja na sera za kuwainua watanzania wote kiuchumi na kuwaleta kwenye mafanikio. Hata kam Simba angeweza kuwashawishi viongozi wa CCM sioni kama sera hiyo ingepata nafasi jinsi ilivyotolewa. Kuna tofauti kubwa kati ya Afrika ya Kusini, Marekani na Tanzania.

Kwa upande wa Marekani Kundi Kuu (weupe) ndo waliowanyanyasa na kuwakandamiza watu weusi kwa takribani miaka 400 na hata baada ya kutambua haki zao (weusi) kama raia miaka karibu 40 iliyopita bado kundi lile lile lina nguvu ya kiutawala. Kwa sababu hiyo basi, wao kuja na sera za kuwainua watu weusi ni jambo la kimantiki na ni kitendo cha kiutu kwani ni weupe waliofaidika na jasho la mtu mweusi. Lakini kwa jinsi wimbi la kisiasa na mafanikio ya kiuchumi yanavyoanza kuendelea sera hizo hatimaye zitajikuta zinatupwa nje na kuangalia uwezo, vipaji, na nafasi ya mtu badala ya rangi, na hivyo kuwalazimisha weusi kushindana na weupe katika uwanja sawa! Yameanza kutokea hayo kwenye elimu ya juu ambapo suala la rangi halitakiwi kuangaliwa kabisa!!!

Afrika ya Kusini ni tofauti (labda ni mfano mzuri kwetu), kundi la watu weupe lililowakandamiza watu weusi (Wengi) kwa karibu miaka 400 lilinufaika na jasho la watu weusi lakini hivi sasa halina uwezo wa kisiasa na nguvu ya kura hivyo limejikuta liko pembeni. Hata hivyo, kundi hilo la watu wachache haliwezi kufurahia matunda hayo ya ukandamizaji wakati lile kundi kuu likiendelea kusota katika umasikini uliokithiri. Ni kwa sababu hiyo basi, sera za "kuwawezesha watu weusi" zinahitajika na ni za lazima.

Kwa upande wetu Tanzania, weupe waliotutawala hawana nguvu yeyote ya kiuchumi au kisiasa, na waasia wachache walionufaika wakati wa ukoloni wana nguvu ya kiuchumi kuliko ya kisiasa. Kwa muda wa miaka karibu 45 Tanzania imetawaliwa na watu weusi na bila ya shaka itaendelea hivyo kwa muda mrefu ujao. Lakini ni chini ya viongozi weusi ndo umasikini umeongezeka na kukithiri!!! Hatuwezi kulalamikia wahindi wa leo kwa umasikini wetu! au wazungu waliopita kwa ufukara wa watu wetu!

Ni kwa sababu hiyo basi, kwa maoni yangu sera zenye kulenga umasikini wa watu wetu ndo sera zenye maana zaidi kuliko sera zenye kulenga rangi, kwani ukishaanzia kwenye rangi, tutajiuliza ni Kabila gani lenye watu masikini zaidi na tutafanye nini kuwawezesha watu wa kabila hilo? Na tusipoangalia tutaanza kuangalia (kama bado hatujaanza) ni dini gani yenye watu walionufaika zaidi na ni dini gani yenye watu masikini na tufanye nini kuwanufaisha watu hao. Hilo ni jambo la hatari. Ni kwa sababu hiyo sikubaliani kabisa na mantiki ya Adam Lusekelo kwani ndani yake imejaa ubaguzi, hisia ya ukuu, na haja ya kustahili!
Mwkjj..

kuna sera tayari (national economic empowerment policy) na chombo cha kusimamia utekelezaji wa sera kipooo...

hebu visit NEEC- Home-.

tuna safari ndefu kuimarika kiuchumi kwa UKOSEFU WA UTASHI KISIASA katika kutendaaaaa...
 
Ukienda Dubai kufanya biashara kama si Mzawa hupewi leseni pale. Wanacho fanya wanatumia majina ya wazawa na wewe mfanyabiashara unamlipa mzawa kwa kutumia jina lake ndo maana utawaona muda wote wapo kwenye gahawa lakini serikali yao imewaona na kuwathamini wazawa kwanza kwa hiyo wao wanatengeneza fwedha kwa mgongo wa wakuja.

Hatuwezi kujilinganisha na hao. Hao ni wabaguzi wa wazi, na jamii yao haina minority ambao wameshika uchumi, kutokana na uzembe wa wenyeji. Hapa Tanzania ukitaka kutekeleza sera kama hiyo inabidi uwe makini na uwe mkweli. Usiwe unalenga tu kupata kura unapotaka kula. Sina hakika kama Idi Simba alikuwa na lengo la kweli la kumnemeesha mtanzania, sioni kama sera zilizopo zinamminya mzawa na kumpendelea asiyemzawa, ni weakness ya wazawa ndio inawapa advantage wasio wazawa. Let us address our weaknesses first then we can see what we can do.
 
Hivi waliopinga sera ya Uzawa ilipotolewa na Mzee Idi Simba wakati huo na kuibadilisha kuwa uwezeshaji si ndio hao wamejitajirisha through Meremeta, Tangold,Deep Green Finance, na Kagoda Ltd.Kwa kweli wananchi wengi kipindi kile walihadaika kwa wanasiasa wachache kukataa sera ya uzawa.

Ukweli ni kwamba ni sera hii ya uzawa ndio inaweza kumkomboa mtanzania.Lakini sera hii inapigwa vita na baadhi ya wafanya biashara wa kiasia ili fedha zinazokusanywa na serikali zeweze kuibwa kwa urahisi.Mafisadi papa wametumia mwanya huu kupora fedha ambazo kama zingetumika vizuri zingewainua wazawa kiuchumi mifano halisi tunayo.

Kwa mtazamo wangu mimi sidhani kama sera hii itapata msukumo unaostahili kutoka serikali inayooongozwa na CCM.Na hili ni dhahiri kashfa zote kubwa na ndogo za rushwa zinadhibitisha hilo.Wapo watu wachache ndani ya CCM wanaoshirikiana na wafanya biashara wachache wa kiasia kupora na kumiliki uchumi wa nchii hii.Na hili pia ni dhahiri kwani wanajulikana ni kina nani na wanafanya nini.

Ili ukombozi halisi wa kiuchumi kwa mtanzania uweze kupatikana ni lazima kuwe na sera madhubuti,mkakati maalum ukiambatana na utashi wa kisiasa wa kumuwezesha mtanzania mzawa kumiliki rasilimali zilizopo nchini pamoja na kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za kuchangia uchumi wa taifa hili.Kinyume na hapo ni kiini macho.
 
Tena Lusekela hajasema vya kutosha. Dunia nzima, hususan mataifa yaliyoendelea, ni kosa kubwa sana kwa serikali kuonyesha kupendelea tabaka fulani la watu, hususan walio wachache na wageni kwa asili. Hii italeta fujo tu nchini leo, kesho au siku za usoni.

Uchumi lazima ushikwe na wengi na lazima kuwe na juhudi za dhati sana kuponya majeraha ya wengi walioumizwa wakati wa ukoloni: hawakupewa elimu bora ya kutosha, waliajiriwa kwa ujira wa kinyonyaji, walibaguliwa, wakatengwa bila huduma bora za kijamii. Waliibiwa rasilimali zao za asili. Watu wetu waliuzwa utumwani kama mbuzi! Kwa ujumla walinyonywa sana. Haya na mengine mengi yanahitaji tiba maalum.

Twahitaji kuwezeshwa, hasa kupewa fursa sawa. Tutawezeshwa vipi? Majibu yapo mengi na twayajua. Mfano:

Elimu: Elimu bora kwa kila mtanzania. Ni kosa kubwa kuwagawa watu kupitia elimu. Wengine kayumba, wengine academy. Serikali inashindwa kusimamia ubora? Tena kuna shule za wahindi tu siku hizi kama ilivyokuwa enzi za mkoloni. Mweusi ananyimwa nafasi, na akipewa atabaguliwa mpaka aondoke!

Miundombinu: Juhudi kubwa za nchi lazima zielekezwe huku ili raia wote wapate mazingira bora ya kufanya shughuli zao za kiuchumi na ziwalipe accordindly. Sio kuboresha miundombinu kuwalenga baadhi ya watu wakati wengine wakisahauliwa! Hii ni aibu na ujinga mkubwa.

Huduma nyingine za jamii: Zimfikie kila Mtanzania kwa usawa na haki.

Sheria/Fursa sawa kwa wote: Iwekwe mikakati makusudi ya kufikiria UWIANO MAALUM wa makundi yote ya kitabaka: rangi (race), jinsia, ulemavu, umri, maeneo ya nchi, n.k. Ajira zitolewe kwa kuzingatia hili. Mikopo benki, mgawanyo wa rasilimali zetu n.k. Haiingii akilini matajiri wakawa wahindi tu. Wakaa maeneo jirani na huduma za kijamii wao tu. Wanaosoma shule bora wao tu. Matajiri wao tu.

Mikakati Maalum: Hii ilenge katika kuleta usawa wa kijamii. Asante Nyerere.

Jamani kudai haki ni mapambano na tusipopambana hili kundi dogo la watawala hawatatujali, watafanya watakalo. Watatuibia sana na kutupeleka kwa hovyo kabisa!
 
Last edited:
kama asemavyo FMES,angempa mtikila 'wa kipindi kile', achana na mtikila huyu aliyechukua 'mkopo' Caspian Construction

Lakini kwa mtizamo wangu ADAM is right!ninasema hivyo kwasababu 'i feel the impact' PRACTICALLY.nipo bongo huku!naona.GT anaweza kushuhudia namna 'watanzania-waasia' walivyoishika serikali hasa katika miradi ya ujenzi.

Miradi yoote inayoendelea Dodoma,kampuni ya mzawa kwa maana ya mzawa ni ELERAI,na ELECTRIC INTERNATIONAL!the rest ni wachina na wahindi,lakini ni local contractors.

I think ni lazima kuwe na 'special considerations' kwa kampuni za wazawa
Wakati kumpendelea mtz mweusi kwa hila itakuwa ni jambo baya, imefika mahali sasa ili mbele ya safari tusijejiingiza kwenye migogoro, kuwe na upendeleo maalumu wa kuwasukuma watz weusi ili nao wawe players katika uchumi wetu. Mfano, kazi nyingi za ujenzi zinataka mitaji mikubwa ambayo kampuni nyingi za wazawa hazinao. Badala ya kuwapa kila kazi ya ujenzi kampuni za watz wa kiasia/kizungu kama estim, daikin,barkeley electric,caspian etc kwasababu wana mitaji, kuwe na namna ambayo kampuni nyingine ndogo zinapewa guarantee za mitaji zinapopata kazi kama hizo kutoka kwa mabank na institution nyingine za fedha. Hilo kwa sasa halipo.
Halafu hawa watz wa kiasia na kizungu faida kubwa huwa inapelekwa nje wanakokuona ni safe. Pengine wasiwasi unatokana na sababu kuwa walio wengi ambao ni weusi hawana...itakuwaje wakiwabadilikia mbele ya safari!!
 
Ukienda Dubai kufanya biashara kama si Mzawa hupewi leseni pale. Wanacho fanya wanatumia majina ya wazawa na wewe mfanyabiashara unamlipa mzawa kwa kutumia jina lake ndo maana utawaona muda wote wapo kwenye gahawa lakini serikali yao imewaona na kuwathamini wazawa kwanza kwa hiyo wao wanatengeneza fwedha kwa mgongo wa wakuja.

Haswa. Na mnaona uchumi wa Dubai unavyoyumba baada ya wageni kukitoa? Mnachotaka ni kupewa na si kuwezeshwa!Mnataka mgao ili mkakae barazani kunywa ghahawa badala ya kushiriki kikamilifu katika kuinua uchumi wenu. Mawazo kama haya hayatatufikisha mbali. Badala ya kuangalia Dubai angalia Mauritius na Singapore ili ujue maana ya kuwezeshwa. Elimu, elimu, elimu na hamna njia ya mkato!

Amandla........
 
Back
Top Bottom