Kuwashwa mwili ni tatizo jipya Dar es Salaam?

Mna uhakika maji ya bomba mnayokunywa ni salama?

Wengi wenu ni vipofu nyie, mtaanza kusema kuna VIRUS yuko angani anawabutua watoto na kuwatumbua mapele. 🤣

Angalieni maji ya bomba hayo kama hayajatiwa madawa fulani. Au chakula wanachokula.

Hakuna cha jotro wala nini. Jotro lipo miaka yote.
Maji ya kwenye chupa kama Uhai, Hill na Kilimanjaro ni salama kwa afya?
 
Nimeona kwa mdogo wangu kumbe ni tatizo limepata watu wengi. Sijaona kwingineko
 
Hizo ni Rashes za joto na unyevunyevu
(Hot and Humid weather). Zingatia kuoga kwa dettol mara mbili kwa usiku
Nafikiri nimekuelewa, wiki mbili zilizopita nilikua Dar, nikapata rushes sana mpaka usoni, ila nimeondoka naona zinaisha na baadhi ya sehemu nilipata muwasho pia vyote vinaisha..mikoa mingi, hali ya hewa ni rafiki sana.
 
Salaam wakuu.
Siku za hivi karibuni nimeona na kushuhudia wakazi wengi hapa Dar es salaam wametokwa na vipele na kuwashwa mwili.

Hasa watoto nimeona wengi pia wanawashwa na vipele mwili mzima. Hivyo nauliza, huu ni ugonjwa wa kawaida au Kuna tatizo lipo? Nauliza na nini cha kufanya ikiwa utapata shida Kama hiyo?

Wewe ni mgeni Dar?

Ni hali ya joto kali nyakati za usiku na kutokwa jasho kwa wingi ndio husababisha hivyo vipele vyenye kuwasha
 
Salaam wakuu.
Siku za hivi karibuni nimeona na kushuhudia wakazi wengi hapa Dar es salaam wametokwa na vipele na kuwashwa mwili.

Hasa watoto nimeona wengi pia wanawashwa na vipele mwili mzima. Hivyo nauliza, huu ni ugonjwa wa kawaida au Kuna tatizo lipo? Nauliza na nini cha kufanya ikiwa utapata shida Kama hiyo?
Kacheki FBP
 
Kuna uwezekano mkubwa ni measles/surua.

Dogo alipata vipele vya aina hiyo wiki iliyopita, vikawa vinamletea homa. Kwenda hospital akaambiwa amepata measles, japo hakuwa na dalili nyingine ambazo huambatana nayo.
 
Joto Kali na ukosefu wa maji ni janga kwa Dar es salaam kama huyu bibi akigombea 2025 na akashinda tuna miaka mitano Tena ya kutaabika kwa kuwashwa miili
Kumbe hili joto na vipele anasababisha huyu bibi??
Huyu ana uwezo wa kimungu twende tukampigie magoti aondoe joto nà vipele.
 
Kuna uwezekano mkubwa ni measles/surua.

Dogo alipata vipele vya aina hiyo wiki iliyopita, vikawa vinamletea homa. Kwenda hospital akaambiwa amepata measles, japo hakuwa na dalili nyingine ambazo huambatana nayo.
Tusubir wataalam
 
Back
Top Bottom