Kuwakemea Viongozi wa Dini, Magufuli Ameweka Rekodi Mpya

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Nimemsikiliza Rais Magufuli, akihutubia taifa baada ya kumwapisha Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba. Kuna mengi aliyoongea JPM ambayo yanavutia mjadala. Mimi nijikite kujadili kwa kifupi alichosema Rais kuhusu Imani, Biblia na Viongozi wa Dini.

Nianze kwa kumtahadharisha Rais wangu Magufuli, awe na Subra katika mambo ya Imani za watu. Mpaka sasa, Rais Magufuli ameonesha ujasiri wa kipekee wa kuongelea mambo ambayo watangulizi wake hawakuthubutu.

Hili la kuwashambulia viongozi wa dini, na hapa niongelee Kanisa Katoliki ambalo nalifahamu vizuri, eti kwa sababu tu wamefanya maamuzi yasiyompendeza, ni jambo la hatari sana, hata kwa wale aliowasifia, hapa namuongelea Baba Askofu Nyaisonga, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, Askofu wa Jimbo anayo mamlaka kamili katika Jimbo lake, kwa habari ya mambo ya Imani na Dini, na hawezi kuingiliwa na kiongozi mwingine, hata Rais wa Baraza la Maaskofu.

Bahati nzuri Baba Askofu Severin NiweMugizi, ambaye ni Askofu anayemkasirisha sana Rais Magufuli, kiasi kwamba hapo nyuma aliwahi mnyang'anya Paspoti kwa madai siyo raia, ni Canonist, yaani bingwa wa sheria za Kanisa. Pia kwa kutazama rekodi ya utendaji wake, ni Mtumishi wa Mungu mwenye msimamo usioyumba. Hivyo inaaminika Baba Askofu anajua fika anachokifanya, kwa mujibu wa sheria na miongozo ya kanisa.

Hivi karibuni, kwa kutumia mamlaka aliyonayo, ametoa amri ya katazo la ibada ya Misa katika Jimbo lake, kama tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid19. Tukumbuke pia kwamba Baba Askofu huyu ndiye pia Askofu wa Magufuli, yaani Chato ni sehemu ndani ya Jimbo lake, kama sijakosea.

Sasa kwa kitendo hicho Baba Askofu Severin amekwenda kinyume na mkakati wa Rais Magufuli, wa kutaka kuionesha dunia kwamba maambukizi ya virusi vya Corona hapa nchini yapo kiwango cha chini, na kwamba Ibada kanisani na misikitini zinaendelea kama kawaida.

Kitendo hicho cha Baba Askofu Severin inaaonekana kimemkasirisha sana Rais Magufuli, hadi akatoa karipio kali kwa "Viongozi" wa dini. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, viongozi aina ya Baba Askofu Severin, wanakimbia mateso, wanaogopa kuwa "Mashahidi" wa imani. Ametoa mifano kadhaa kutoka Biblia, ya manabii waliokuwa tayari kutoa uhai wao ili kulinda imani yao.

Hapa tujiulize swali. Askofu anakuwaje Shahidi kwa kuacha kuzuia Ibada za Misa? Kama kweli anakuwa Shahidi, basi ndio kusema kitendo cha kukusanyika kanisani kinahatarisha uhai kwa waumini na padre au Askofu wao? Ndio maana anaweza kuwa shahidi? Kama ndivyo basi tishio la Corona ni la kweli?

Swali la pili. Mtu anaweza kuwa Shahidi kwa kuchagua kutoa uhai wake tu, na sio uhai wa mtu mwingine. Askofu anaweza kuwa shahidi kwa kuchagua kutoa uhai wake kutetea imani yake, na siyo kuteketeza uhai wa wengine ambao wala hawajui kwamba maisha yao yapo hatarini, ila wamehakikishiwa na Rais Magufuli kwamba kanisani ni salama na nchi yao ipo salama. Kama hivyo ndivyo, inakuwaje Magufuli anawataka Maaskofu wawe mashahidi kwa kuwatoa muhanga waumini wao? Hapo kuna tatizo.

Ni vema pia kutambua kwamba mtu anakuwa Shahidi kwa Neema ya Mungu anayemvutia huko, na si kwa maelekezo ya mtu mwingine.

Kuna hii hoja kwamba kipi ni sahihi, kuendelea kukusanyika kanisani kumwomba Mungu atunusuru na Corona? Au tusiende kanisani, kuepuka misongamano, lakini tuendelee kusali? Mimi naamini kwamba hili ni Swali gumu na linahitaji Neema ya Mungu. jambo la kwanza kiongozi wa dini asali na kufunga ili kupata mapenzi ya Mungu katika hili ni yapi? Ibilisi aliwahi kumjaribuYesu, alipomwambia ajitupe toka ncha mnara wa Hekalu, kwamba imeandikwa Mungu atatuma Malaika wake wamchukue asiangukie mawe. Ni kweli imeandikwa, lakini kama alivyomjibu Yesu, huko ni kumjaribu Mungu. Ni sawa na mtu anayekataa kwenda Hospitali akidai aponywe na Mungu moja kwa moja. Kwa maneno mengine, anadai muujiza.

Lakini Mungu huruhusu muujiza kama ishara, ili watu waamini. Haina maana kwamba daima tutaishi kwa miujiza. Mungu ameruhusu maendeleo ya sayansi ili binadamu waweze kutatua shida zao. Ni juu ya viongozi wa dini kutuongoza kwa kutumia miongozo ya kiroho, na siyo miongozo ya kisiasa.

Rais Magufuli amepewa maono na Mungu awakemee viongozi wa Dini?

Anadiriki kutamka kwamba viongozi wa dini wasiomtii Magufuli, wanaongozwa na Shetani!

Hii ni jeuri iliyopitiliza viwango vyote!!
Vipi kuhusu Magufuli aliyeua watu wengi wanaompinga? Vipi mauaji ya Kibiti? Ambayo IGP mpaka sasa anajutia? Vipi mauaji katika bomoabomoa? Ni lini Magufuli ametubu kwa uporaji katika sanduku la kura?
Uporaji wa fedha za kodi za mafukara, kujenga mambo ya kifahari Chato, ikiwemo uwanja wa ndege, gharama zake hazikupita bungeni?

Magufuli huyu ndio anadiriki kutamka viongozi wa Dini wanaompinga wanaongozwa na Shetani?

Kwa Maaskofu wanaomtii Rais Magufuli, akiwemo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, TEC, Baba Askofu Nyaisonga, ambaye Magufuli kamtaja kwa jina na kumshukuru kwa UTIIFU wake kwa Rais Magufuli, ni vema watambue kwamba imewapasa kumtii Mungu, na siyo wanadamu, na hakika si viongozi wa siasa.

Nakumbuka katika ibada, nadhani ya miaka 150 ya umisionari kule Bagamoyo, miaka michache iliyopita, Baba Askofu Nyaisonga aliomba Maaskofu wakutane na Rais ili wawasilishe "maombi" yao. Nilijisikia aibu sana, Baba Askofu alivyolidhalilisha kanisa, na yeye mwenyewe, kwa kuwa ombaomba kwa viongozi wa siasa. Askofu atambue kwamba daima wanasiasa hutumia Dini kukidhi mahitaji yao, na hawana Shukrani.
 
kumuagiza Mwigulu akachek maabara kuna tatizo gani nyie haijawashangaza watanzania wenzangu?
Wanaidhalilisha sayansi ili siasa ndiyo ibaki ya kuaminika. Kwa kauli ya Mwigulu majuzi kule Bungeni, ilikuwa ni sweet music kwa a crazy and frustrated president. Kamzawadia uwaziri na atamtumia kuvunja authority ya Medical science, ili authority ibaki kwa Magufuli. Yuko juu ya viongozi wa dini pia.

Hata Trump wa USA anatumia " Ushirikina" huo, japo kule wataalamu wanampinga hadharani, na takwimu kule huwezi kuzipika kirahisi. Hapa kwetu nani atadiriki kumpasha Magufuli za uso? Alikuwa Tundu Lissu tu. Ona kilichompata
 
Mindi

Nimeipenda sana no 2

Amebaki kwenye biblia na akasahahu historia ya kanisa lake hasa kanisa la mwanzo
Waamin walijitenga kwa siri na waliongoza wenzao kwa alama ambazo leo zinatumika kuashiria kusanyiko la kumega ambazo kwa urahisi zipo kwenye mavazi ya mapadri ili wakutane kuumega wasiuawe na askari ya wakirumi waliokuwa wanawadhulumu.

Je, walipaswa kusali hadharani wauawe na kusiwepo kutaniko la kristu, mahubiri na kuendeleza imani ya kikristo? Na leo imani angeipataje? Na je kanisa la mwanzo hawamo watakatifu?


Nashauri, maaskofu kuunga mkono hilo, hapo Dar wanakutana jumanne ni vema maparoko wasajesti hilo na kwingineko maaskofu watumie busara na kufunga
Aulize vip vatican waamuni wanakutana?
Roma has spoken, obey

Papa alishatoa waraka wa kuruhusu na kutuombea msamaha kwa Mungu dhidi ya amri ya tatu
 
Back
Top Bottom