Kuwa sehemu ya historia ya katiba mpya kwa kuweka maoni yako hapa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,646
698,169
Katiba mpya yaja na hili sio jambo geni wala la kubahatisha tena. Tumetoka mbali na tumepitia mengi mabaya na mazuri ya kushangaza na ya kuleta matumaini pia. MOJA LILILO WAZI ni kwamba KATIBA MPYA haizuiliki tena!

Jamii Forums ni mtandao tegemewa kwa mengi hapa Tanzania hasa linapokuja suala la mawazo mbadala yenye tija na chanzo kikubwa cha habari za kuaminika na kujenga.

Mawazo na makala nyingi za katiba mpya aina vinapitia hapa ama vinaanzia hapa
Viongozi wengi serikalini ni watumiaji wakubwa wa huu mtandao wa JF
Vyama vya kijamii, wananchi, waandishi mbalimbali, na watu wengine wote wa kaliba zote ni watumiaji mahiri wa JF

Kwa maana hiyo basi tunapoingia kwenye mchakato muhimu wa katiba mpya, Jamii Forums kupitia wewe inaweza kutoa mchango muhimu na mkubwa kwenye kupata katiba mpya Tanzania

Kuwa sehemu ya historia tukuka! Weka wazo/mawazo yako sasa kuhusu katiba mpya. Kumbuka kati ya mengi tutakayoyaandika hapa machache yataingia kwenye katiba mpya. Historia itakukumbuka, historia itatukumbuka. Jamii Forums itakumbukwa!

Unawaza nini kuhusu katiba mpya? Karibu sasa kama mzalendo na mhitaji wa katiba mpya kwa manufaa yetu sote na vizazi vyetu vijavyo!

Karibuni kwa furaha na moyo wa kujitoa kushiriki hili

Screenshot_20220118-142702.jpg
 
Yangu haya hapa
1.Bunge lisiwe la kudumu, wabunge wafike tu bungeni nyakati za vikao vya bunge na kulipwa posho za kujikimu za kawaida kwa viwango vya watumishi wa serikali.. Wabunge wawe ni watumishi wa sekta nyingine za serikali

2. Wabunge wawe ni wanataaluma waliobobea kwenye taaluma mbali mbali..na vikao vya bunge vizingatie mahitaji ya lazima ya taifa kama kipaumbele no 1

3.Thamani kubwa iliyowekwa kwenye siasa ibadilishwe na kuwekwa kwenye taaluma na wanataaluma ili kuchochea maendeleo

4. Mishahara na marupurupu ya wabunge visiwe tofauti na mapato ya wanataaluma kama walimu, mabwana afya shamba nk
 
Ni kwa jinsi gani tunaweza kupambana na maadui watano ujinga, maradhi, umasikini? Kutokana na matokeo ya Necta juzi ujinga bado ni tatizo. Bado hatujafikia kiwango cha kujikinga na maradhi tuko kwenye kiwango cha kutibu maradhi. Malaria, UTI na matumbo ya kuhara bado ni matatizo ya kila siku kwa wengi wetu.
Thamani kubwa iliyowekwa kwenye siasa ibadilishwe na kuwekwa kwenye taaluma na wanataaluma ili kuchochea maendeleo kwenye kila sekta
 
Yangu haya hapa
1.Bunge lisiwe la kudumu, wabunge wafike tu bungeni nyakati za vikao vya bunge na kulipwa posho za kujikimu za kawaida kwa viwango vya watumishi wa serikali.. Wabunge wawe ni watumishi wa sekta nyingine za serikali

2. Wabunge wawe ni wanataaluma waliobobea kwenye taaluma mbali mbali..na vikao vya bunge vizingatie mahitaji ya lazima ya taifa kama kipaumbele no 1

3.Thamani kubwa iliyowekwa kwenye siasa ibadilishwe na kuwekwa kwenye taaluma na wanataaluma ili kuchochea maendeleo

4. Mishahara na marupurupu ya wabunge visiwe tofauti na mapato ya wanataaluma kama walimu, mabwana afya shamba nk
Mawaziri wasiwe wabunge, na kama mbunge akiteuliwa kuwa waziri; jimbo lake litangazwe kuwa huru
 
1.Serikali tatu ni jambo la muhim yani tanganyika, Zanzibar na URT

2.Madaraka ya raisi yaangaliwe upya*

3.Nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya zipigiwe kura
 
Wakuu wa Mikoa na Wilaya wachaguliwe na wananch kama wanavyochaguliwa wabunge. Mikoa na Wilaya kuwe na mabaraza ya kuwawajibisha Wakuu hao wasipokuwa wawajibikaji.
Liwepo baraza la taifa lisilotokana na chama chochote cha siasa kwa ajili ya kusimamia miongozo yote ya nchi.. Uwepo utaratibu maalum wa kupata wajumbe wake
 
Vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya vifutwe kabisa,Wilaya ibaki na Katibu tawala tu kushughulika na Kero za wananchi hii itapunguza gharama za kuendesha nchi

Na huyu katibu Tawala iwe ni nafasi ya kuombwa na kufanyiwa usaili isiwe ya kuteuliwa.
 
Mchakato wa kupata katiba mpya:

Yeyote atakayeshiriki katika kuandaa na kupitisha katiba mpya ASIGOMBEE nafasi yoyote ya uongozi kwa miaka 20 ijayo ili kuondoa uwezekano wa waandaa katiba kujitafutia vyeo katika katiba. Hivyo kuna umuhimu wa kubadili sheria ya katiba mpya na kama Rais atakuwa ndiye atapitisha katiba mpya, basi asigombee tena hadi miaka 20 ipite. Mjumbe wa bunge la katiba vile vile asiruhusiwe kugombea nafasi yeyote kwa muda wa miaka 20.
 
Hili gap kati ya wapiga kura na wapigiwa tiba yake ni kuondoa utukufu kwenye siasa.. Hili ni hitaji kubwa mno
FB_IMG_1642497743898.jpg
 
Madaraka ya Raisi ni makubwa katiba tuliyo nayo inamfanya Raisi kuwa Mungu.
Tupunguze Madara ya Raisi na akiboronga Mambo kwenye utawala wake awajibike.

Tuwe na katiba ambayo Kila mtu yupo chini ya sheria kuepusha haya tunayoyaona Sasa.
 
Tuwe na katiba ambayo Kila mtu yupo chini ya sheria kuepusha haya tunayoyaona Sasa
 
Kenya wameandika katiba mpya nzuri baada ya vita wakati wa uchaguzi, Marekani waliandika katiba mpa baada ya vita ya kiraia " Civil War".
Ktk mazingira ya Tanzania ambapo walioko madarakani hawataki katiba mpya kwa kuhofia kupoteza madaraka, katiba mpya haitopatikana.
Inatakiwa kutengenezwe mazingira ambayo kila upande utapata kiu kubwa ya katiba mpya ili hali fulani isije kutokea tena.
 
Back
Top Bottom