Kuwa na UPENDO maana yake ni nini?

Kuwa na UPENDO maana yake ni nini?

nyumbani kwenu ulikuwa ukikosea unapelekwa mahakamani?

System ni ipi?

Na mtu akikosewa lazima asamehe? Msamaha ni nini?
Inawezekana kabisa nilikuwa napelekwa Mahakamani, Mahakama si jengo tu na hakimu lakini unapotuhumiwa hata nyumbani ina maana kuna consequences zake na mara nyingi hukumu zinatolewa, kuchapwa, kuzuiwa kucheza nk, na pia pale mtoto anapotendewa na wenziye lazima pia ilielekezwa some form ya lipizi.
Mara nyingi inasemwa binadamu ni mbinafsi kwa asili mi naona hapa kwenye msamaha ndio mahali pake kwenye ubinafsi wake binadamu asiposamehe uwa anaumia mwenyewe na anapata adhabu hasa kwahiyo msamaha ni kufanya amani na nafsi yako na wala hutaona uzito wa kumsamehe mwengine. Uwa tunahangaika sana kuwaona wengine wabaya kumbe kila suluhisho linapatikana kwenye nafsi zetu..
"System" inayoendesha Ulimwengu, labda hatuijui wala kuiona lakini ipo......
 
Hili ni kweli na namtaka Mtambuzi aje hapa anipe maelezo ya kutosha
Hawezi kutuambia eti uwepo wa Mungu unategemea uwepo wa alichokiumba [Shetani]


Kwenye hili inawezekana kuwa ni kweli lakini kuwepo kwa ugumu wa binadamu kuutenda upendo hakuwezi kuufanya usiwe na maana

Upendo hauna uongo bali kuna upendo na kisicho upendo

Kitendo cha mtu kukufanyia mambo fulani halafu akaja kukuacha au kukuumiza ukweli ni kuwa alikuwa ana pretend,kama alikuwa ana pretend huyo alikuwa hana upendo kwakuwa ukishamfanyia mtu jambo au kitu chochote kile kwasababu fulani huo sio upendo ni kitu kingine kabisa

Hivyo upendo hauna uongo bali upendo tu!

Ni kweli uliyoongea.Ni either upendo au Pretency/ unafiki
 
Last edited by a moderator:
kwa maelezo hayo, kuadhibu ni kazi yetu na systen ni sie wenyewe.

Ndio maana hata kwa ngazi ya familia mtu anaadhibiwa.

Na mtu akishaadhibiwa, inatosha mengine ni details tu.

Inawezekana kabisa nilikuwa napelekwa Mahakamani, Mahakama si jengo tu na hakimu lakini unapotuhumiwa hata nyumbani ina maana kuna consequences zake na mara nyingi hukumu zinatolewa, kuchapwa, kuzuiwa kucheza nk, na pia pale mtoto anapotendewa na wenziye lazima pia ilielekezwa some form ya lipizi.
Mara nyingi inasemwa binadamu ni mbinafsi kwa asili mi naona hapa kwenye msamaha ndio mahali pake kwenye ubinafsi wake binadamu asiposamehe uwa anaumia mwenyewe na anapata adhabu hasa kwahiyo msamaha ni kufanya amani na nafsi yako na wala hutaona uzito wa kumsamehe mwengine. Uwa tunahangaika sana kuwaona wengine wabaya kumbe kila suluhisho linapatikana kwenye nafsi zetu..
"System" inayoendesha Ulimwengu, labda hatuijui wala kuiona lakini ipo......
 
nikichitaka kuonyesha Lizzy ni kuwa, kuadhibu ni kazi yetu, kisasi ni kazi ya 'karma'. Ndio maana hata home tunaadhibiana bila hata kupelekana mahakamani.

Na system ni sisi wenyewe.

Kusamehe au kutosamehe kila mtu na tafsiri yake, mwingine anaweza kuona kasamehe lakini muda huo huo anamfanyia mabaya aliyemkosea, mfano tu kutangaza kwa watu fulani alifanya kile na kile. Kasamehe? May be yes, may be not. Kila mtu kwa mtizamo wake.

Mwingine unamkosea, anakuadhibu na mambo yanaishia pale pale.Kasamehe? May be yes, may be not.


Ki usahihi utotoni ulipokuwa unakosewa ulitakiwa uambiwe kuwa unatakiwa usamehe,kijamii kuna makosa ya kumalizwa na nyie wenyewe hapo ndipo unaweza kusamehe lakini kuna mengine hayawahusu nyie

Mfano mtu ameua na ndugu wakamsamehe,hiyo haina maana serikali haitamchukulia hatua muuaji kwasababu ndugu wa marehemu wamemsamehe kwasababu usalama na uhai wa raia unalindwa na serikali kwa mujibu wa sheria hivyo ndugu wanapomsamehe watakuwa wamefanya jambo kwa faida ya nafsi yao na afya yao na serikali itafanya yake

Ndio

Kwasababu kukaa na kinyongo na kulipiza kisasi ni hasara kwa afya zetu na hakuna faida yoyote ile ya kisasi tofauti na ridhiko la kihisia tu na ni la muda mfupi

Unataka kwa tafsiri ipi?

Kidini au Kijamii?
 
Umeona eeh.

Au mtu anahubiri upendo nje, na hali hapatani hata na nduguze au mme/mkewe.

Upendo umejaa unafiki mno, ndio maana watu wanaumizana. Anamchekea mtu usoni moyoni anstamani achukue nafasi yake kazini.

Hata ukoloni uliingia hivi hivi, watu wanaleta dini na kuhubiri upendo hapo hapo wanataka rasilimali na watumwa juu.

Mie naona ni bora mtu aliyemkweli kwako, hakufeel anakuacha ufahamu ili usije kuwa victim bure.

Mnafiki ni mtu mbaya sana, ni heri ukutane na jambazi kuliko mtu mnafiki,nauogopa sana unafiki,heri mtu anionyeshe waziwazi kuwa hanipendi nitamvumilia kuliko nayedhani ananipenda kumbe moyoni mwake ananichukia.
 
Umeona eeh.

Hivi unadhani kwa nini mashosti wananyang'anyana hata waume? Ni unafiki huu huu, kuhubiri upendo in public, in private mtu anamnyesha sumu.

Ndio maana mienilisema maana ya upendo ni complex. Wengine hata unafiki wanaita kuwa 'civilized'.

Mnafiki ni mtu mbaya sana, ni heri ukutane na jambazi kuliko mtu mnafiki,nauogopa sana unafiki,heri mtu anionyeshe waziwazi kuwa hanipendi nitamvumilia kuliko nayedhani ananipenda kumbe moyoni mwake ananichukia.
 
Umeona eeh.

Hivi unadhani kwa nini mashosti wananyang'anyana hata waume? Ni unafiki huu huu, kuhubiri upendo in public, in private mtu anamnyesha sumu.

Ndio maana mienilisema maana ya upendo ni complex. Wengine hata unafiki wanaita kuwa 'civilized'.

Kweli upendo ni complex ,upendo ni Tabia tu ya mtu awe nayo na mtu anaweza kutii sheria za upendo iwapo mtu huyo ana hofu ya Mungu ndani yake.

Embu angalia mara ngapi binadamu anadhulumu haki ya mwenzake in the name of upendo? Mfano mtu ana mwanaye,huyo mwana let's say kambaka binti wa jirani yake,ni wazazi wachache sana ambao wanaweza kukubali sheria ifuate mkondo lakini wengi wao watapigana kufa na kupona mwanae awe huru na asionekane na hatia yoyote.
 
_41111356_13_beninpeeter.jpg


Ni vyema kuwa na upendo kama watoto wadogo maana hata sisi kama watu wazima tumezaliwa tukiwa na upendo ila katika makuzi yetu tunanyang'anywa huo upendo na na ndiyo maana tunaishi kwa chuki na visasi tofaui na watoto ambao hugombana lakini punde tu husahau na kucheza pamoja kwa furaha na amani wakiwa wamesahau tofauti zao......



upendo- maana yake ni kujipenda+kupenda+kupendwa (soma maelezo hapo juu). Lakini kumbuka kwamba ili upendo ukamilike ni lazima uzungukwe na chuki, upendo bila chuki haufai kuitwa upendo, chuki hukamilisha upendo, huufanya upendo uwe na maana. Mwanamume bila mwanamke hajakamilika, kumbuka kila jambo lina pande mbili, na pande hizi hazipingani, ila zinakamilishana. Kumbuka pia kwamba, bila Ibilisi hakuna Mungu (najua utabisha, lakini kubisha kwako hakutabadili ukweli, ukweli utabaki kuwa ukweli) Kuna watu huwa wanaomba Ibilisi aangamie, nimesikia maombi haya tangu nikiwa mdogo na mpaka leo yanaendelea lakini Ibilisi haangamii, ukweli ni kwamba haitatokea akaangamia, na kama itatokea akaangamia, hata Mungu naye ataangamia au atakosa maana. Watu wanamuabudu Mungu kwa sababu ya Ibilisi, kama ikitokea Ibilisi akaangamia kuna haja gani ya kumwabudu Mungu?
Jibu maswali yafuatayo:

1. Unaweza kufafanua “upendo halisi” jinsi gani? ․․․․․

2. Unaweza kufafanua “upendo wa kupumbazika” jinsi gani? ․․․․․

3. Kwa maoni yako, kuna tofauti gani kati ya taarifa hizo mbili? ․․․․․

 
Mfano wa Upendo Halisi​
Masimulizi ya Biblia kuhusu Yakobo na Raheli yanaonyesha waziwazi upendo halisi. Walikutana kwenye kisima, ambapo Raheli alikuwa ameenda kuwanywesha maji kondoo wa baba yake. Mara moja Yakobo akavutiwa naye. Kwa nini? Kwanza, alikuwa "na umbo zuri na sura nzuri."-Mwanzo 29:17.

Hata hivyo, kumbuka kwamba upendo halisi hautegemei sura ya nje tu. Mbali na sura nzuri, Yakobo alitambua mengi kumhusu Raheli. Biblia inasema kwamba baada ya muda, Yakobo hakuvutiwa tu naye. "Alimpenda Raheli."-Mwanzo 29:18.

Huo ulikuwa mwisho wa hadithi ya kimahaba? Hapana-kwa kuwa hadithi hiyo haikuishia hapo. Baba ya Raheli alimwomba Yakobo asubiri miaka saba kabla ya kumuoa Raheli. Iwe ilikuwa haki au si haki, upendo wa Yakobo ulitahiniwa. Kama ungekuwa upendo wa kupumbazika tu, Yakobo hangemngojea. Ni upendo halisi tu unaoweza kuvumilia. Ikawa namna gani? Biblia inasema: "Yakobo akatumikia miaka saba kwa ajili ya Raheli, lakini machoni pake hiyo ikawa kama siku chache kwa sababu alimpenda."-Mwanzo 29:20.

Unaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Yakobo na Raheli? Kwamba upendo halisi unaweza kuvumilia. Pia, hautegemei tu sura ya nje. Kwa kweli, mtu atakayekuwa mwenzi wako wa ndoa huenda asiwe mwenye kuvutia sana unapomwona kwa mara ya kwanza. Kwa mfano, Barbara, alifahamiana na kijana mmoja ambaye Barbara hakuvutiwa sana naye mwanzoni. Anasema: "Lakini nilipopata kumjua vizuri, mambo yakabadilika. Niliona jinsi Stephen anavyowahangaikia watu na jinsi nyakati zote anavyotanguliza masilahi ya wengine. Hizo ni sifa ambazo nilijua mume mzuri anapaswa kuwa nazo. Nikavutiwa na nikaanza kumpenda." Matokeo yakawa, ndoa yenye msingi mzuri.

Ukiwa mtu mzima anayeweza kuwa na urafiki wa kimapenzi, ukiwa na lengo la kufunga ndoa, utajua jinsi gani kwamba umempata mtu unayempenda kikweli? Moyo wako unaweza kukuongoza, lakini tegemea kanuni za Biblia. Usitegemee sura ya nje tu. Chukua muda kusitawisha uhusiano huo. Kumbuka, upendo wa kupumbazika hufifia baada ya muda mfupi. Upendo wa kweli huimarika kadiri wakati unavyopita na kuwa "kifungo kikamilifu cha muungano."-Wakolosai 3:14.

Uwe na hakika kwamba unaweza kupata upendo wa aina hiyo, ikiwa utajifunza mengi zaidi ya mambo unayoona na kuhisi.
 
Back
Top Bottom