Kuwa na UPENDO maana yake ni nini?

Kuwa na UPENDO maana yake ni nini?

1 Wakorintho 13: 1 – 9

  1. Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
  2. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
  3. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
  4. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
  5. haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
  6. haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
  7. huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
  8. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
  9. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;
Yeah nakubaliana na wewe kwa kurejea maandiko kwani hata Yesu alipoulizwa na wanafunzi wake kama sikosei kwamba ni amri ipi iliyo kuu alisema kwamba amri iliyo kuu ni upendo na akasisitiza kwamba mpende jirani yako kama unavyojipenda na alipoulizwa ni yupi huyo jirani yako....

Mnaojua maandiko malizieni...........
 
Halafu kuna sadist people hao wana justify hate kwa sababu za kijinga
Hata hizi dini za mapekeo pamoja na kuhubiri pendo, lakini kwa sababu ya kugombea waumini kwa sababu ya kuongeza pato la sadaka wamekuwa wakihubiri kinyume chake kwa kujenga chuki miongoni kwa waumni kwamba wao sio si wa Mungu sisi ndiyo wa Mungu.....

Halafu watu wanatarajia amani itawale hapa duniani, wengine hata wanakesha wakiomba amani itawale wakati mioyo yao imejaa chuki... Ajabu eh!
 
hiyo sio chuki, hicho.ni.kijicho. Na mtu wa aina hiyo ni kumpa za uso tu.

Maana ya upendo vs chuki ni subjective sana. Kuna mwingine anadhani ana upendo, kimya kimya anadhulumu hata yatima.

So ni kila mtu anavyoxhukulia.

wajua Kongosho chuki zingine zile Kwanini hivi yule na sio mimi, ukionyesha msimamo lazima usimame Kweli hapo, hapo ni kuvimbiana kimya kimya...
 
Last edited by a moderator:
umetoa mfano.mzuri, so unawapenda boko haram?

Huwachukii ili uonekane una fit kwenye hii definition.

Ndiyo maana kuna kampeni ya kuwausia watu wasambaze upendo, na kama watu wangekuwa wanasambaza upendo kusingekuwa na alshabaab wala Boko haram, si ndiyo eh Kongosho
 
Last edited by a moderator:
hiyo sio chuki, hicho.ni.kijicho. Na mtu wa aina hiyo ni kumpa za uso tu.

Maana ya upendo vs chuki ni subjective sana. Kuna mwingine anadhani ana upendo, kimya kimya anadhulumu hata yatima.

So ni kila mtu anavyoxhukulia.

Hilo eneo la mayatima lina wanafiki wengi kweli...
Ni eneo ambalo linatumiwa na wachache kujinufaisha, na ndiyo maana kila baa siku hizi ni mtaji kwa wachache, misiba siku hizi ni dili, ajali nazo ni dili yaani wanadamu wamekuwa kitu cha ajabu sana siku hizi...

Sambaza upendo
 
Sio upendo vs chuki Unaweza usimpende mtu na usimchukie...
 
umetoa mfano.mzuri, so unawapenda boko haram?
Huwachukii ili uonekane una fit kwenye hii definition.

Siwezi kuwachukia, bali nitawaonyesha upendo, huwezi kujua labda hawakuonyeshwa upendo na ndiyo sababu wakafikia kufanya hayo waliyoyafanya. Kongosho kumbuka tawala zetu nyingi ni za kidhalimu kuna watu hufikia mahali wakazalisha mawazo mabaya katika vichwa vyao na kufanya matendo ya kikatili kwa sababu ya kutotendewa haki, hawa ji watu ambao walifunyangwa katika malezi yaliyojaa chuki na visasi, na ndiyo maana nikamwambia The Boss kwamba ni vigumu kwa mtu aliyelelewa kwa kuambia tema mate tumchape kuwa na upendo, huyu amefundishwa kulipa visasi tangu utoto wake, unafikiri akifanyiwa jambo ambalo anahisi kwmaba ameonewa atachukua hatua gani.

Hizi dini zetu za mapokeo nazo, ingawa nisingependa kuzungumzia dini katika mada hii, zimetumika sana kuwajengea chuki waumini wake miongoni mwao, mahubiri ya siku hizi yamejaa chuki kupita kiasi, sasa unatarajia nini?
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh.

Au mtu anahubiri upendo nje, na hali hapatani hata na nduguze au mme/mkewe.

Upendo umejaa unafiki mno, ndio maana watu wanaumizana. Anamchekea mtu usoni moyoni anstamani achukue nafasi yake kazini.

Hata ukoloni uliingia hivi hivi, watu wanaleta dini na kuhubiri upendo hapo hapo wanataka rasilimali na watumwa juu.

Mie naona ni bora mtu aliyemkweli kwako, hakufeel anakuacha ufahamu ili usije kuwa victim bure.

Hilo eneo la mayatima lina wanafiki wengi kweli...
Ni eneo ambalo linatumiwa na wachache kujinufaisha, na ndiyo maana kila baa siku hizi ni mtaji kwa wachache, misiba siku hizi ni dili, ajali nazo ni dili yaani wanadamu wamekuwa kitu cha ajabu sana siku hizi...

Sambaza upendo
 
Ok, is it even practical?

Uwakamate boko haram uanze kuwafundisha upendo badala ya kuwapeleka mahakani?

Mwizi amaingia kwako, unamshika na kuanza kumhubiri upendo badala ya kumpeleka polisi?

Unanitania.

Siwezi kuwachukia, bali nitawaonyesha upendo, huwezi kujua labda hawakuonyeshwa upendo na ndiyo sababu wakafikia kufanya hayo waliyoyafanya. Kongosho kumbuka tawala zetu nyingi ni za kidhalimu kuna watu hufikia mahali wakazalisha mawazo mabaya katika vichwa vyao na kufanya matendo ya kikatili kwa sababu ya kutotendewa haki, hawa ji watu ambao walifunyangwa katika malezi yaliyojaa chuki na visasi, na ndiyo maana nikamwambia The Boss kwamba ni vigumu kwa mtu aliyelelewa kwa kuambia tema mate tumchape kuwa na upendo, huyu amefundishwa kulipa visasi tangu utoto wake, unafikiri akifanyiwa jambo ambalo anahisi kwmaba ameonewa atachukua hatua gani.

Hizi dini zetu za mapokeo nazo, ingawa nisingependa kuzungumzia dini katika mada hii, zimetumika sana kuwajengea chuki waumini wake miongoni mwao, mahubiri ya siku hizi yamejaa chuki kupita kiasi, sasa unatarajia nini?
 
Last edited by a moderator:
hili somo wangekuzwa nalo watoto wetu.kesho yetu ingekua nzur
 
Tena dini ndio zimeleta.chuki kama nini. Yaani mtu anamchukia mwingine sababu tu anaamini tofauti na yeye.

Ndo maana nasema upendo vs chuki ni subjective kulingana na malezi.

Imagine kuua asiyeamini sawa na wewe ni jambo la thawabu, afu leo umwambie huyo mtu hana upendo, atakuelewa?

Hakuui sababu analuchukia ww mtambuzi,ni kuwa unachoamini wewe ndio adui yake, hapo anakuwa anapigana na adui yake.

Hata hizi dini za mapekeo pamoja na kuhubiri pendo, lakini kwa sababu ya kugombea waumini kwa sababu ya kuongeza pato la sadaka wamekuwa wakihubiri kinyume chake kwa kujenga chuki miongoni kwa waumni kwamba wao sio si wa Mungu sisi ndiyo wa Mungu.....

Halafu watu wanatarajia amani itawale hapa duniani, wengine hata wanakesha wakiomba amani itawale wakati mioyo yao imejaa chuki... Ajabu eh!
 
Ok, is it even practical?

Uwakamate boko haram uanze kuwafundisha upendo badala ya kuwapeleka mahakani?

Mwizi amaingia kwako, unamshika na kuanza kumhubiri upendo badala ya kumpeleka polisi?

Unanitania.

Swala la upendo halimaanishi kutompeleka muovu kwenye mkondo wa sheria akapate haki yake, mahakama ndipo mahali ambapo haki itapatikana na si kujichukulia sheria mkononi. Kila mtu lazima avune alichokipanda, kwa hiyo mwenye kuwaumiza wengine lazima hukumu impate na ndio maana hata dini inasema watenda mema wataenda peponi na watenda maovu wataenda motoni...
 
Unaji contradict, 'mwenye kuwaumiza wengine lazima apate adhabu yake'.

Ina tofauti gani na utotoni ila 'tema tumchape'?

Kwa nini tema tumchape unaiangalia kama kisasi na chuki halafu unasema mkosaji ni fair.akiadhibiwa?

Nilijua utasema boko haram wasamehewe na kuachiwa huru ili wajifunze maana halisi ya upendo.

Hili somo ni gumu sana kulihubiri kwetu binaadam japo halina ugumu wowote, tungalikuwa tunaelekeza focus zote na attention kwetu kabla ya kukabili wengine/walimwengu hali ingekuwa nzuri kweli. Unaambiwa usimtendee mwenziyo usivyotaka kutotendewa inamaanisha nini? Ni maneno rahisi kuyarusha hewani lakini practically yanaonekana magumu, njia bora kabisa ni kujigusa mwenyewe spiritually
 
Unaji contradict, 'mwenye kuwaumiza wengine lazima apate adhabu yake'.

Ina tofauti gani na utotoni ila 'tema tumchape'?

Kwa nini tema tumchape unaiangalia kama kisasi na chuki halafu unasema mkosaji ni fair.akiadhibiwa?

Nilijua utasema boko haram wasamehewe na kuachiwa huru ili wajifunze maana halisi ya upendo.
Sio kazi yetu kuadhibu kuna system in place inayopelekea watu hao kupata adhabu. Waathirika wanaweza kusamehe na kusahau lakini so long "system" ina operate utafanyaje?
 
Kumbuka pia kwamba, bila Ibilisi hakuna Mungu (najua utabisha, lakini kubisha kwako hakutabadili ukweli, ukweli utabaki kuwa ukweli) Kuna watu huwa wanaomba Ibilisi aangamie, nimesikia maombi haya tangu nikiwa mdogo na mpaka leo yanaendelea lakini Ibilisi haangamii, ukweli ni kwamba haitatokea akaangamia, na kama itatokea akaangamia, hata Mungu naye ataangamia au atakosa maana. Watu wanamuabudu Mungu kwa sababu ya Ibilisi, kama ikitokea Ibilisi akaangamia kuna haja gani ya kumwabudu Mungu?

Mkuu mada yako ni nzuri lakini imetiwa doa na hii kauli yako

Hivi mkuu hujui kuwa Mungu alikuwepo kabla ya kila kitu ikiwemo na huo ubaya?

Nkuu naona nikurudishw madrasa maana inaonekana umesahau kabisa elimu ahera

CC: kahtaan , FaizaFoxy , Karucee , Ishmael , Basluma Original , Mwana Mtoka Pabaya Ntuzu . . . . . . . .!
 
Last edited by a moderator:
nyumbani kwenu ulikuwa ukikosea unapelekwa mahakamani?

System ni ipi?

Na mtu akikosewa lazima asamehe? Msamaha ni nini?

Sio kazi yetu kuadhibu kuna system in place inayopelekea watu hao kupata adhabu. Waathirika wanaweza kusamehe na kusahau lakini so long "system" ina operate utafanyaje?
 
Mkuu mada yako ni nzuri lakini imetiwa doa na hii kauli yako

Hivi mkuu hujui kuwa Mungu alikuwepo kabla ya kila kitu ikiwemo na huo ubaya?

Nkuu naona nikurudishw madrasa maana inaonekana umesahau kabisa elimu ahera

CC: kahtaan , FaizaFoxy , Karucee , Ishmael , Basluma Original , Mwana Mtoka Pabaya Ntuzu . . . . . . . .!

Nakubaliana na wewe.Hapo mwisho kaharibu.
Upendo kuuhubiri ni rahisi lakini kuutenda ndio issue.Binadamu tuna ubinafsi sana.Ni wachache sana wanafanikiwa kuwa na upendo wa kweli
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe.Hapo mwisho kaharibu.
Hili ni kweli na namtaka Mtambuzi aje hapa anipe maelezo ya kutosha
Hawezi kutuambia eti uwepo wa Mungu unategemea uwepo wa alichokiumba [Shetani]
Upendo kuuhubiri ni rahisi lakini kuutenda ndio issue.Binadamu tuna ubinafsi sana.Ni wachache sana wanafanikiwa kuwa na upendo wa kweli

Kwenye hili inawezekana kuwa ni kweli lakini kuwepo kwa ugumu wa binadamu kuutenda upendo hakuwezi kuufanya usiwe na maana

Upendo hauna uongo bali kuna upendo na kisicho upendo

Kitendo cha mtu kukufanyia mambo fulani halafu akaja kukuacha au kukuumiza ukweli ni kuwa alikuwa ana pretend,kama alikuwa ana pretend huyo alikuwa hana upendo kwakuwa ukishamfanyia mtu jambo au kitu chochote kile kwasababu fulani huo sio upendo ni kitu kingine kabisa

Hivyo upendo hauna uongo bali upendo tu!
 
Last edited by a moderator:
nyumbani kwenu ulikuwa ukikosea unapelekwa mahakamani?

System ni ipi?
Ki usahihi utotoni ulipokuwa unakosewa ulitakiwa uambiwe kuwa unatakiwa usamehe,kijamii kuna makosa ya kumalizwa na nyie wenyewe hapo ndipo unaweza kusamehe lakini kuna mengine hayawahusu nyie

Mfano mtu ameua na ndugu wakamsamehe,hiyo haina maana serikali haitamchukulia hatua muuaji kwasababu ndugu wa marehemu wamemsamehe kwasababu usalama na uhai wa raia unalindwa na serikali kwa mujibu wa sheria hivyo ndugu wanapomsamehe watakuwa wamefanya jambo kwa faida ya nafsi yao na afya yao na serikali itafanya yake
Na mtu akikosewa lazima asamehe?
Ndio

Kwasababu kukaa na kinyongo na kulipiza kisasi ni hasara kwa afya zetu na hakuna faida yoyote ile ya kisasi tofauti na ridhiko la kihisia tu na ni la muda mfupi
Msamaha ni nini?
Unataka kwa tafsiri ipi?

Kidini au Kijamii?
 
Back
Top Bottom