tusipotoshane
JF-Expert Member
- Jul 19, 2018
- 730
- 693
Juzi asubuhi wakati nipo maeneo ya Kibamba Chama Jijini Dar,huku watu/abiria wakisubiri daladala kuelekea maeneo mbalimbali ya Jiji kwa mihangaiko yao,baadhi tulikuwa kijiweni kwa shughuli zetu za bodaboda walionekana vijana 5 au 6 hivi wenye umri kati ya miaka 10-13 wakiwa na vindoo/visinia vilivyojaa vitumbua/maandazi wakielekea maeneo ya Mbezi Mwisho na kwingineko kwa ajili ya kuuza.Ndipo jamaa wa vijiweni walipoanza kumwaga umbea kuwa vijana hao wanalelewa(wanaishi) kwa mama mmoja wa hapo Kibamba Chama na anajua alikowatoa. Muda wanaotoka kwenda kuuza bidhaa zao ni kuanzia SAA 11 au 12 kasoro asubuhi.Wadau hao wa kijiweni walitanaabaisha kuwa vijana hao hawajui Kiswahili au huzuga kwa maneno mawli au matatu hivi ya Kiswahili na muda mwingi kwenye mizunguko yao huwa kimya ili kutofahamika wao ni akina nani,wanatoka wapi,wanaishi wapi na kwa nani.Wambea hao wa Kijweni walisema inavyoonekana wanatoka mojawapo ya nchi za Afrika mashariki kama vile Rwanda,Burundi,Congo n.k.
Kwa tetesi hii,tunaomba uhamiaji waende maeneo ya Kituo cha Kibamba Chama kuanzia SAA 11 asubuhi na kubaini kama kuna watoto wa aina hiyo ili kuwakamata na kuwahoji kupata ukweli wa umbea huo wa wana vijiwe wa Kibamba Chama kwani ulinzi na usalama ni jukumu la kila Mtanzania.Lisemwalo lipo,kama halipo laja liko njiani.
Wasalaamu.
Sent using Jamii Forums mobile app