Tetesi: Kuwa na mashaka ya jambo fulani ukitoa taarifa kwa vyombo dola kufuatilia na kukuta taarifa sio ya kweli pia ni uzalendo kwa taifa letu

tusipotoshane

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
733
1,000
Juzi asubuhi wakati nipo maeneo ya Kibamba Chama Jijini Dar,huku watu/abiria wakisubiri daladala kuelekea maeneo mbalimbali ya Jiji kwa mihangaiko yao,baadhi tulikuwa kijiweni kwa shughuli zetu za bodaboda walionekana vijana 5 au 6 hivi wenye umri kati ya miaka 10-13 wakiwa na vindoo/visinia vilivyojaa vitumbua/maandazi wakielekea maeneo ya Mbezi Mwisho na kwingineko kwa ajili ya kuuza.Ndipo jamaa wa vijiweni walipoanza kumwaga umbea kuwa vijana hao wanalelewa(wanaishi) kwa mama mmoja wa hapo Kibamba Chama na anajua alikowatoa. Muda wanaotoka kwenda kuuza bidhaa zao ni kuanzia SAA 11 au 12 kasoro asubuhi.Wadau hao wa kijiweni walitanaabaisha kuwa vijana hao hawajui Kiswahili au huzuga kwa maneno mawli au matatu hivi ya Kiswahili na muda mwingi kwenye mizunguko yao huwa kimya ili kutofahamika wao ni akina nani,wanatoka wapi,wanaishi wapi na kwa nani.Wambea hao wa Kijweni walisema inavyoonekana wanatoka mojawapo ya nchi za Afrika mashariki kama vile Rwanda,Burundi,Congo n.k.

Kwa tetesi hii,tunaomba uhamiaji waende maeneo ya Kituo cha Kibamba Chama kuanzia SAA 11 asubuhi na kubaini kama kuna watoto wa aina hiyo ili kuwakamata na kuwahoji kupata ukweli wa umbea huo wa wana vijiwe wa Kibamba Chama kwani ulinzi na usalama ni jukumu la kila Mtanzania.Lisemwalo lipo,kama halipo laja liko njiani.

Wasalaamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilele9

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
1,165
2,000

Umetumia njia ndefu.
 
cabo

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
2,653
2,000
Mbona kuna watoto wengine wa mikoani huko hata kiswahili hawajui labda ungesema kuhusu umri na mda huo walitakiwa kuwapo shuleni hapo sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tusipotoshane

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
733
1,000
Ndio maana nimesema ni tetesi,kwani vyombo husika vikifuatilia na kujiridhisha kuna tatizo?Kwani kwenda hapo kuna gharama yoyote kama kwenda Nanjilinji?Ndio maana ya neno ulinzi shirikishi.Kama siyo raia ,basi hao watoto wanatakiwa kupata haki yao ya elimu.Gharama za kusoma awamu hii ya tano ni ndogo sana kama sio hakuna kabisa.Pia kumbuka kuna Elimu Bure/Bila Malipo.

Nilimaanisha njia ndefu kuwafikia walengwa/wahusika. Wengi wa wafanyakazi ndio hao unaowatuhumu kwa uvivu wa kusoma.
Nimekusoma Mkuu wangu Kilele9 kama sio Kilele Cha Kibo au Mawenzi vya Mlima Kilimanjaro.Wavivu wa kusoma sio wafanyakazi wao walisoma vitabu kwa hiyo sio wavivu tofauti na vijana wa sasa hivi wanapenda kitonga/vitonga (summarised materials),sawa na matamanio ya mtu(kijana) kwamba leo ni maskini kesho anataka kuwa na pesa 'mingi' ya kula bata kwa short cut bila kuvuja jasho la kwapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom