Kuwa na Marafiki wanaoeleweka

Miiku

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
3,842
2,000
Hello Guys,

Katika maisha ya sasa (sijui huko nyuma) kuwa na marafiki wanaoleweka namaanisha wenye uchumi wa kati na wajuu kama wewe ni hohe hahe ni ngumu sana kujoin na watu kama hawa, utaishia kuwa na wa level ya chini ambao nao ukipata changamoto ya kifedha e.a hawawezi kukusaidia zaidi ya kusikitika na wewe.

Kama huna hela jua na marafiki wa kueleweka huna automatcal.

Huku kubaguana kupo kuanzia kwenye jamii ya chini, siasani, kwenye misiba na sherehe hata huko Makanisani ni kawaida kuona waamini baada ya Ibada kuisha kujitenga tenga kwa makundi madogo madogo kujadili mambo mbalimbali. Inasikitisha. Na ukiwa kiherehere usiye na msaada ndio husikilizwi kabisa.
 
matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,025
2,000
Eleweka wewe kwanza. Kwenye maisha like attacts like
Ila ukija kwenye physics zetu sheria ya usumaku ni kinyume.
 
Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,905
2,000
Ukiwa na urafiki na mtu mwenye hela basi na wewe uwe nazo.

Kama huna,na una urafiki na mtu mwenye hela ujue basi una mawazo ya maana na kibiashara una akili mingi..friend with benefit.

Basi kama umebahatika kuwa na rafiki mwenye hela na bado ni marafiki na wewe huna,basi jua fika humtangazii injili ya shida na kulia lia hovyo kuhusu maisha magumu na kutaka akuje pesa🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️
 
Miiku

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
3,842
2,000
eleweka wewe kwanza.
kwenye maisha like attacts like
ila ukija kwenye physics zetu sheria ya usumaku ni kinyume.
Kweli usipoelewaka mipango yako na unavyovimiliki pesa, mali , akili na maarifa sahau watu kuja kwenye maisha yako.
 
Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
5,781
2,000
Hili ni Kweli na huwezi kuliona kama hujapitia moja wapo ya stage hapo. Ukiwa na hela utaona watu wenye ela ndio marafiki zako ukichange gafla wenye ela wanappotea halafu unaanza kukutana na wale ambao hawana ela mnaanza kuelezana namna hali iivyo ngumu.

Ni mambo ambayo yapo yanatokea kila siku.Halafu Wanaotunga sera za elimu wangeiangalia elimu itolewayo kwenye shule zetu na kuifanyia mageuzi tuweze kuwa na somo la maisha.Mahesabu ya kwenye karatasi ni rahisi kuandika ila ukija mtaani ni vitu viwili tofauti.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,707
2,000
Fanya hivi.

Kuwa na kitu kitakachowafanya wao watake kujiunga na wewe. Na si wewe kutaka kujiunga na wao tu.

Kuwa na ujuzi fulani hivi unaotakiwa nao. Hela yao haiwatatulii matatizo yao, wewe ukiweza ku add value katika maisha yao, watakutafuta wenyewe.

Sasa wewe hela huna, sawa.

Bado wanakufikiria na pengine kuna wenye moyo wa kukusaidia.

Ila watakusaidia vipi utoke kwenye kutaka kusaidiwa kila siku uweze si tu kusimama mwenyewe, bali pia hata na wewe kusaidia wengine?

Una ujuzi gani? Mipango gani? Vipaji gani? Unajua biashara gani? Mpaka sasa ushafanya nini? Umekwama wapi?Umeandika mipango yako? Una patent? Copyright? Trade Mark? Umesajili nini? Una elimu gani? Uzoefu gani? Unataka kufanya nini? Kwa nini usaidiwe wewe na si wengine maelfu kama wewe?

Ulimwengu wa sasa watu hawaaminiki na wengine hatutaki marafiki wa karibu wengi kuepusha mizozano na matatizo ya kiusalama, kwa nini mtu akufungulie wewe network yake ya urafiki? Atakuamini vipi wewe kirahisi tu?

Kuna mengi naweza kuandika nilivyosaidia watu, na nilivyofunzwa hivyo tangu awali kwenye nasaba yangu, lakini sitaki kuonekana najitapa na sipendi kuvunja maadili ya faragha zangu na niliowasaidia.
 
Miiku

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
3,842
2,000
Fanya hivi.

Kuwa na kitu kitakachowafanya wao watake ku join na wewe. Na si wewe kitaka ku join na wao tu.

Kuwa na skill fulani hivi inayotakiwa nao. Hela yao haiwatatulii matatizo yao, wewe ukiweza ku add value katika maisha yao, watakutafuta wenyewe.

Sasa wewe hela huna, sawa.

Bado wanakufikiria na pengine kuna wenye moyo wa kukusaidia.

Ila watakusaidia vipi utoke kwenye kutaka kusaidiwa kila siku uweze si tu kusimama mwenyewe, bali pia hata na wewe kusaidia wengine?

Una ujuzi gani? Mipango gani? Vipaji gani? Unajua biashara gani? Mpaka sasa ushafanya nini? Umekwama wapi?Umeandika mipango yako? Una patent? Copyright? Trade Mark? Umesajili nini? Una elimu gani? Uzoefu gani? Unataka kufanya nini? Kwa nini usaidiwe wewe na si wengine maelfu kama wewe?

Ulimwengu wa sasa watu hawaaminiki na wengine hatutaki marafiki wa karibu wengi kuepusha mizozano na matatizo ya kiusalama, kwa nini mtu akufungulie wewe network yake ya urafiki? Atakuamini vipi wewe kirahisi tu?

Kuna mengi naweza kuandika nilivyosaidia watu, na nilivyofunzwa hivyo tangu awali kwenye nasaba yangu, lakini sitaki kuonekana najitapa na sipendi kuvunja maadili ya faragha zangu na niliowasaidia.
@kiranga wewe ni writter mzuri endelea kuandika mkuu najua una maarifa mengi na kuyagawa na hasa kwa kuandika humu ni Hobby yako. Comment zako huwa wengi tunazisoma na hizo zimekupa upekee na wengine humu.
 
yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,595
2,000
Ukiwa na urafiki na mtu mwenye hela basi na wewe uwe nazo.

Kama huna,na una urafiki na mtu mwenye hela ujue basi una mawazo ya maana na kibiashara una akili mingi..friend with benefit.

Basi kama umebahatika kuwa na rafiki mwenye hela na bado ni marafiki na wewe huna,basi jua fika humtangazii injili ya shida na kulia lia hovyo kuhusu maisha magumu na kutaka akuje pesa
mkuu we upo kundi gani?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,707
2,000
@kiranga wewe ni writter mzuri endelea kuandika mkuu najua una maarifa mengi na kuyagawa na hasa kwa kuandika humu ni Hobby yako. Comment zako huwa wengi tunazisoma na hizo zimekupa upekee na wengine humu.
Nakushukuru sana.

Kila mtu ana upekee wake. Ndiyo maana namuelezea mtoa mada autafute upekee wake na autumie huo.

Asifikiri tu kuwa yeye ndiye anawahitaji wengine, aweze kujua wengine watakachoweza kuhitaji kutoka kwake na kukipalilia hicho kipaji chake mpaka kimletee heshima na mafanikio katika jamii.

Kila mtu ana nafasi ya kuchangia. Mara nyingi tatizo ni kujua nafasi hiyo iko wapi, kipaji chako ni kipi, wapi utapata watu wa kuku mentor na kukuendeleza, nini cha kufanya, kwa wakati gani, na kadhalika.
 
Misako

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
1,157
2,000
Fanya hivi.

Kuwa na kitu kitakachowafanya wao watake kujiunga na wewe. Na si wewe kutaka kujiunga na wao tu.

Kuwa na ujuzi fulani hivi unaotakiwa nao. Hela yao haiwatatulii matatizo yao, wewe ukiweza ku add value katika maisha yao, watakutafuta wenyewe.

Sasa wewe hela huna, sawa.

Bado wanakufikiria na pengine kuna wenye moyo wa kukusaidia.

Ila watakusaidia vipi utoke kwenye kutaka kusaidiwa kila siku uweze si tu kusimama mwenyewe, bali pia hata na wewe kusaidia wengine?

Una ujuzi gani? Mipango gani? Vipaji gani? Unajua biashara gani? Mpaka sasa ushafanya nini? Umekwama wapi?Umeandika mipango yako? Una patent? Copyright? Trade Mark? Umesajili nini? Una elimu gani? Uzoefu gani? Unataka kufanya nini? Kwa nini usaidiwe wewe na si wengine maelfu kama wewe?

Ulimwengu wa sasa watu hawaaminiki na wengine hatutaki marafiki wa karibu wengi kuepusha mizozano na matatizo ya kiusalama, kwa nini mtu akufungulie wewe network yake ya urafiki? Atakuamini vipi wewe kirahisi tu?

Kuna mengi naweza kuandika nilivyosaidia watu, na nilivyofunzwa hivyo tangu awali kwenye nasaba yangu, lakini sitaki kuonekana najitapa na sipendi kuvunja maadili ya faragha zangu na niliowasaidia.
Fact
 
troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
15,798
2,000
Kutokuwa na pesa na kipimo cha ufinyu wa kufikiri.
Ukweli mchungu. Wenye pesa hawapendi kuwa karibu na watu ambao anajua fika hakuna atachomuongezea.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom