Kuwa Mpinzani kisiasa ni mateso sana

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
9,517
12,813
Hasa ukiwa kwenye chama cha siasa ambacho ni dhaifu na kisicho na uelekeo, sera wala mipango itakayowavutia wananchi kukiamini, kukuunga mkono na kukichagua kuongoza.

Ni mateso kuishi na kufanya kazi ya siasa kwenye, Chama cha siasa cha upinzani ambacho hata viongozi wake waandamizi hawaaminiani bali wanaviziana kwa kuogopana badala ya kuambiana ukweli.

kwasababu ya mateso bila choyo upinzani, ndio maana hata wanaotoka chama Tawala na kuhamia au kujiunga upinzani, hawadumu kuishi kwenye mateso makali, ambayo hayana dalili za kupungua wala kwisha, huku matumaini ya kutwaa madaraka ndio hakuna kabisa.

Kazi ya upinzani ni rahisi sana. Si ni kupinga tu. Ila mateso yake ni msoto hasa yataka moyo kua upinzani usio na faida, hata hivyo that is the nature of politics.
 
Wapinzani wengine baada ya kuishiwa hoja wameanza kupandikiza chuki na ubaguzi ili wapate kura.lakini bado watanzania wameendelea kuwapuuza na kuwakataa .nimeamini chama kikikosa sera na ajenda za kuwashawishi watu kukipatia kura kinaweza kupanga na kuratibu hadi Vitendo vya kihaini kabisa.
 
hasa ukiwa kwenye chama cha siasa ambacho ni dhaifu na kisicho na uelekeo, sera wala mipango itakayowavutia wanainchi kukiamini, kukuunga mkono na kukichagua kuongoza...
Huku Wengine tukila Raha kwenye Chama Tuko Nacho mpaka Kituue hata wakisema Kinalea Mafisadi sawa tu..
Kinalea Machawa sawa tu
AddText_04-30-11.34.42.jpg
 
👊💪🔥 uko chonjo, uko rada uko mbele ya wakati mno comrade, umetisha sana 🤣👍🙏
Mkuu Hiki chama Nakipenda Sana Nina Muda nacho Nimekipigania Sana, Ninakidai Vingi sana..
Na chenyewe Kinanidai Vingi sana..
Kwahyo kukata Tamaa kizembe kwenye Chama changu Hapana 😅😅😅..

Hapa hakuna Kukata Tamaa Comrade 😅😅
 
Wapinzani wengine baada ya kuishiwa hoja wameanza kupandikiza chuki na ubaguzi ili wapate kura.lakini bado watanzania wameendelea kuwapuuza na kuwakataa .nimeamini chama kikikosa sera na ajenda za kuwashawishi watu kukipatia kura kinaweza kupanga na kuratibu hadi Vitendo vya kihaini kabisa.
Yes,
sure, uko sawa kabisa comrade, but tumejipanga balaa kuwakabili na kuwadhibiti vilivyo...
 
Upinzani huanzia kwa wananchi baada ya kuona watawala wanawatesa na kwamba kuna haja na uwezekano wa kuwabadilisha.

Chama ni jukwaa tu la kutimiza malengo hayo.

Kama wananchi hawajawa tayari vyama vya upinzani haviwezi kupata nguvu.
 
Mpinzani sio Adui yako chukua hoja zake kama sehem ya kiooo kujitazama.

Ukijifungia na kuhisi Uko salama ndani huduma muhimu zitazorota na kusababisha madhira kwa ndugu zetu wengine.

Don’t relax ,Play your card smart.
 
Shida Kubwa Wao Ni spika tu Maiki inatoka ndani ya Chama chetu..
Na hilo nimeliona..Wapinzani wanatumika Na Baadhi ya wanachama wasio na Nia njema
ka ukali flani hivi kanahitajika kwenye chama, kuwanyofoa hawa mamluki wachache, kwasabb hawawezi kuinjoy privileges za huku na kule...
 
ka ukali flani hivi kanahitajika kwenye chama, kuwanyofoa hawa mamluki wachache, kwasabb hawawezi kuinjoy privileges za huku na kule...
Shida hao wanaofanya hivyo wameshikilia Mizizi ya Chama Inabidi kuwaonya tu ndani ya Chama maana mpango wao kukipasua Chama kabla ya Uchaguzi 2025..
Tetesi tunazipata Na tunaziwasilisha Sehemu husika..
Wanamipango mibovu sana
 
Back
Top Bottom