100%Unaweza kushinda ndani kama jini nani sijui!, Halafu ukitoka nje dakika mbili tu unatamani tena kurudi ndani.. mbaya mbovu introvert tunaujinga huu.
Naweza nikawa nataka kutoka na wewe umekaa sehemu nayotaka kupita naweza nikasubiri mpaka utoke ndo namimi nipite!, mitabia myengine sijui ya wapi tu!..
Huku mitandaoni tumejazana maana ndo sehemu tunaweza hata kumtishia mtu kumdunda!, ila huku ana kwa ana hata kutukana tu ni kasheshe!.
Ndo viumbe pekee vinakaa mji fulani ila vinajua mitaa michache sana maana kutembeatembea sio pendeleo sana kwao!.
Mzazi mwenye mtoto wa aina hii usimsokote sana mwanao kumlazimisha achanganyikane na watu!, wakati wake ukifika atachanganyika na atachagua wakuchanganyika nao!.
pili mfatilie ila usimfatilie sana mpaka ukaziba uhuru wake ambao ni amani yake!, utamkosesha kujiamini hata akiwa peke yako atakuwa anaona kama unamuangalia 24/7.
Usiruhusu mtu mwengine ambae hazijui hulka za mwanao amsumbue hovyohovyo bila sababu za msingi.
Jua vitu anavyovipenda ukiweza mpatie kadri uwezavyo kwa vipimo vya wastani, usimzidishie.
Introvert wengi wana hulka ya uoga na akikuwa hiyo hulka ikakomaa ndo inamvaa na kumsababishia "anxiety".
Hivyo hakikisha akiwa bado mdogo mpe kazi ambazo zitaongeza ujasiri wake, sanasana hakikisha anakuwa anafanya zile kazi ngumu kiasi na pia uwe unampa maneno ya kumtia moyo ya kwamba anaweza!. jitahidi kumsoma hali zake maana ni mabingwa wa kuficha!, hivi ndo viumbe vinaweza kutunza siri mpaka kufa!.
Mwisho kuwa makini na namna unavyoenenda nae maana anaweza akawa anakushinda hata utafakari!, usimtake ajielezee sana bali kama ni kitu cha kufanya muache afanye!, maana huwa si wazuri sana kwenye kujieleza ila kutenda wapo smart sana!.
kweli wengine ni mixer na wengine wanashida fulani...Kuna muda unaweza sema mtu ni introvert ila ukijaribu ku dig deeper unakuta chanzo cha kutochanganyikana na watu ni childhood traumas alizopitia ..sasa zinakuja kumu affect kwenye utu uzima
Marafiki atawapata tu tena akizoeana nao unaweza kusema sio yeye!.. ila itakuwa vyema sana kama atapata rafiki wakuchangamka nao.Kuna Mwanangu yuko form 2 ana tabia hizo,ndio yupo form,akirudi shule ni ndani,kuna baadhi ya majirani uwa wanamuona mtaani akiwa anaenda au kurudi shule lakini hawajui kama ni Mwanangu coz dogo hajulikani anakaa wapi,pale home ni ndani tu,kuna kipindi alidai anataka kunifundisha forex maana nilimpa kipc changu kibovu kibovu na home kuna wifi ya voda ya mchongo,ila sasa upande wa shuleni si mzuri sana,mtaani hana rafiki coz sijawahi kumuona kucheza na wenzake,kuna kipindi nilimfuatilia shuleni kwao nikagundua kule pia hana marafiki,wakati wa kutoka kuelekea stendi uwa namuona yuko peke yake,ajichanganyi na wenzie
Yeah ukifanya mabadiriko kiasi inapendeza, ila ni ngumu kubadili tabia zote!.Nafikiri ilikua wazo zuri kwangu kujitoa taratibu kwenye hilo group na kua Ambivert ( Extrovert + Introvert )
Circumstances za kimaisha zinafanya baadhi ya watu kuwa hivi either upo katiba upbringing ya udini sana au mazingira sio rafiki ya changanyikeni, effects from parenting na socialization.
Kuna kipindi namaliza O'level na A'level nasubiri matokeo kazi kugombana na mshua tu maana anakufuata room mbona hutoki nje wewe? Mida tunaonana ni ile naenda kuchukua chakula au natoka kununua matumizi ya nyumbani (Gengeni, Dukani) au nipo jikoni na saidia kuandaa chakula cha wote.
JF ilikua relief kwa kipindi fulani ila now nimekua mtu mwepesi sana kumzoea mtu na nimekua na limit ya nani nimzoee!
Kabisa hii pia ni faida kubwa sana hasa ukiwa unaishi changanikeni.Na kuna wengine wanakuogopa mpk akiwa anajambo anataka kulifikisha kwako anajiuliza aanzie wapi...🤣
Kwa nini umesema hivyo mkuu?Bila shaka wewe ni andunje.