kkarumekenge
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 1,708
- 1,026
Jamaa anataka picha siyo michoro. Hata hivyo atapataje picha huku tezi dume limeshaondolewa? Hapo sasa!
Salamu !
Chai moto ya choya inapunguza athari za magonjwa ya wazee,kama saratani inayosababishwa na ulawiti na ufiraji !
Pathogenesis tafadhali! !!!Salamu !
Chai moto ya choya inapunguza athari za magonjwa ya wazee,kama saratani inayosababishwa na ulawiti na ufiraji !
Naomba kujua tofauti ya mtu mwenye:
1.BUSHA.
2.TEZI DUME.
3.MSHIPA.
Ee Mola, tuepushe na magonjwa ya wazee wa Pwani !
Mimi nilfanyiwa hiyo ya ngiri maji, pumbu haikuvimba sana na wala mie mwenyewe sikujua kama nina tatizo hilo, ilikuwa ya kulia lkn wakati niko theatre dkr akaniambia hata kushoto nayo ina tatizo na nikakubali kufanyiwa zote...tatizo langu ni kwamba mrija wa upande wa kulia kuunganisha kwenye uume huwa unaiuma sana na huwa inasababisha maumivu kwenye korodani ya kulia na some times uvimba kidogo....NAOMBA USHAURI WENU WADAU NIFANYEJE KWANI NIMESHAENDA HSPTL WAKASEMA SINA NGIRI, NIMEZUNGUKA HOSPITAL NYINGI NA NIPO TAYARI KWA OPERATIONBusha (ngiri maji) ni maji yaliyotuama kwenye mfuko wa korodani (pumbu) kwasababu mbalimbali kama vile kuziba kwa mirija ya kusafirisha majitaka (lymphatics). Mishipa hii inaweza kuzibwa na minyoo midogo (filaria) inayoenezwa kwa kuumwa na mbu wa aina mbalimbali (Culex, ades, anopheles) na kusababisha matende na/au mabusha. Pia unaweza kupata busha kama ukiwa na hitilafu kwenye korodani (kupigwa, maambukizi kwenye korodani au kuzaliwa na hitilafu), mwanga wa tochi unapenya kwenye uvimbe wa busha. Mara nyingi hauna maumivu na unaweza kuzuia kwa kupambana na mazalia ya mbu, kulala kwenye chandarua na kunywa vidonge vya kuzuia mapusha na matende mara kwa mara. Upasuaji ndiyo matibabu ya busha lililozidi kiasi.
Mshipa/hernia (ngiri kavu) inasababishwa na kipande cha utumbo kushuka na kuelekea kwenye pumbu kupitia matundu (inguinal rings) yaliyotanuka kimakosa, hivyo kusababisha maumivu makali na uvimbe sehemu ya kinena. Uvimbe huu ni hatari sana unaweza kusababisha utumbo uonze kama ukibanwa sana. Uvimbe wa mshipa huwa unachezacheza (palsate) wakati wa kukohoa, na matibabu yake ni ya haraka (emergency) kwa njia ya upasuaji. Uvimbe wa hernia (mshipa) haupitishi mwanga wa tochi ukimulikwa. Sababu za mshipa ni kufanya kazi ngumu, mazoezi magumu, kubeba vitu vizito sana (mizigo, kunyanyua vyuma), kupata choo kigumu, kikohozi cha muda mrefu, kujisaidia bila kuchuchumaa au kuzaliwa ukiwa na hitilafu kwenye matundu ya inguinal.
Tezi dume linakaa kandokando ya njia ya kutolea mkojo (urethra) kutoka kwenye kibofu. Kazi yake ni kutoa majimaji yenye alikali ili kusafisha tindikali (acid) kwenye njia ya mkojo na ukeni ili kuzuia sperms zisiharibike zinapopita kwenye njia hizo. Pia inazibeba sperms kwenye maji hayo na kuzifanya zitoke kuelekea ukeni wakati wa kujamiana.
Busha (ngiri maji) ni maji yaliyotuama kwenye mfuko wa korodani (pumbu) kwasababu mbalimbali kama vile kuziba kwa mirija ya kusafirisha majitaka (lymphatics). Mishipa hii inaweza kuzibwa na minyoo midogo (filaria) inayoenezwa kwa kuumwa na mbu wa aina mbalimbali (Culex, ades, anopheles) na kusababisha matende na/au mabusha. Pia unaweza kupata busha kama ukiwa na hitilafu kwenye korodani (kupigwa, maambukizi kwenye korodani au kuzaliwa na hitilafu), mwanga wa tochi unapenya kwenye uvimbe wa busha. Mara nyingi hauna maumivu na unaweza kuzuia kwa kupambana na mazalia ya mbu, kulala kwenye chandarua na kunywa vidonge vya kuzuia mapusha na matende mara kwa mara. Upasuaji ndiyo matibabu ya busha lililozidi kiasi.
Mshipa/hernia (ngiri kavu) inasababishwa na kipande cha utumbo kushuka na kuelekea kwenye pumbu kupitia matundu (inguinal rings) yaliyotanuka kimakosa, hivyo kusababisha maumivu makali na uvimbe sehemu ya kinena. Uvimbe huu ni hatari sana unaweza kusababisha utumbo uonze kama ukibanwa sana. Uvimbe wa mshipa huwa unachezacheza (palsate) wakati wa kukohoa, na matibabu yake ni ya haraka (emergency) kwa njia ya upasuaji. Uvimbe wa hernia (mshipa) haupitishi mwanga wa tochi ukimulikwa. Sababu za mshipa ni kufanya kazi ngumu, mazoezi magumu, kubeba vitu vizito sana (mizigo, kunyanyua vyuma), kupata choo kigumu, kikohozi cha muda mrefu, kujisaidia bila kuchuchumaa au kuzaliwa ukiwa na hitilafu kwenye matundu ya inguinal.
Tezi dume linakaa kandokando ya njia ya kutolea mkojo (urethra) kutoka kwenye kibofu. Kazi yake ni kutoa majimaji yenye alikali ili kusafisha tindikali (acid) kwenye njia ya mkojo na ukeni ili kuzuia sperms zisiharibike zinapopita kwenye njia hizo. Pia inazibeba sperms kwenye maji hayo na kuzifanya zitoke kuelekea ukeni wakati wa kujamiana.
Mimi nilfanyiwa hiyo ya ngiri maji, pumbu haikuvimba sana na wala mie mwenyewe sikujua kama nina tatizo hilo, ilikuwa ya kulia lkn wakati niko theatre dkr akaniambia hata kushoto nayo ina tatizo na nikakubali kufanyiwa zote...tatizo langu ni kwamba mrija wa upande wa kulia kuunganisha kwenye uume huwa unaiuma sana na huwa inasababisha maumivu kwenye korodani ya kulia na some times uvimba kidogo....NAOMBA USHAURI WENU WADAU NIFANYEJE KWANI NIMESHAENDA HSPTL WAKASEMA SINA NGIRI, NIMEZUNGUKA HOSPITAL NYINGI NA NIPO TAYARI KWA OPERATION
Asante sana kwa elimu hii! Naamini unautaalamu mkubwa na viungo vya uzazi vya mwanaume ndiomaana unatoa elimu hii, sorry, naomba unisaidie na hili: nina mdogo wangu (kwa sasa ana miaka 26) miaka kama mitatu iliyopita alikuwa akilalamika kuwa anaskia maumivu makali kwenye korodani zake hasa ya upande wa kushoto. Ilibidi twende hospitali kutafuta tiba. Baada ya kufanyiwa uchunguzi na wataalamu( kwa kuzigusagusa korodani zake hasa mishipa-hii ni kwa mujibu wa maelezo yake kuwa hakuna kifaa kilichotumika kumchunguza isipokuwa mikono ya daktari!).
Baada ya uchunguzi huo alishauriwa afanyiwe upasuaji mdogo kwenye korodani ya kushoto kwa maelezo kuwa kuna mishipa mingi imeota ambayo ilitakiwa kuondolewa. Madhara ya kutoitoa mishipa hiyo aliambiwa kuwa kwa baadae ingewezakumfanya asiwe na uwezo wa kumpa mimba mwanamke. Hivyo tulikubaliana afanye(ukizingatia daktari tulimuamini kwani ni specialist kutoka taasisi kubwa ya serikali hapa nchini). Sasa kilichonishangaza ni mara baada ya kupona kidonda cha oparesheni, korodani ilisinyaa na mpaka sasa imesinyaa(yaani ilikuwa ndogo sana kuliko ilivyokuwa mwanzo(SI KWAMBA MWANZO ILIVIMBA, ILIKUWA KAWAIDA TU) na pia si mara moja wala mara mbili namskia analalamika kuwa kuna kipindi anahisi maumivu kama yale yaliyosababisha afanyiwe opareshini japo yanakuja na kuondoka. Matatizo kama hayo yanasababishwa na nini? na kwanini korodani ilisinyaa baada ya oparesheni/ kuna uwezekano wowote wa kuwa iliharibiwa na oparesheni hivyohaiwezi kufanya kazi ten? Naomba msaada wako tafadhali.
mkuu ubarikiwe sana, nashukuru kwa ushauri wako inshaallah nitarudi hospitali wanicheck tena....lkn kama hutojali nikutafute kama upo DAR ili nipate ushauri zaidi, kama una hospitali basi nitafarijika zaidi, NASUBIRI KUSIKIA KUTOKA KWAKOPole sana, mara nyingi ngiri maji (busha) huwa haina maumivu, na hakuna sababu ya kufanyiwa upasuaji kama huna maumivu na uvimbe (mpira) ni mdogo tu, aliyekufanyia upasuaji alikusababishia majanga yasiyo ya lazima. Kutokana na maelezo yako nina wasiwasi kuwa ulikuwa huna busha (ngiri maji), vinginenyo ulihudumiwa na mtaalam asiye na ujuzi au uzoefu mkubwa wa kushuhulikia maradhi hayo. Mara nyingi Ngiri maji inahitaji upasuaji mdogo tu ili kuyamwaga maji na kupindua mfuko (tunica vaginalis) unaoruhusu maji kutuama kwenye pumbu. Labda wakati wa upasuaji mtaalamu alijeruhi au kufunga na viungo vingine visivyohusika na kusababisha shida yako unayojihisi. Rudi tena hospitali hata kama sio ile ile kitengo cha upasuaji (surgery) ukachunguzwe zaidi na kufaidika na utaalamu wa madaktari waliobobea na wenye uzoefu. Inshallah utapona. Tofautisha kati ya ngiri maji, ngiri kavu na shida nyingine za sehemu ya korodani kama uvimbe, maambukizi, na kuumia sehemu za mapumbu.
Salamu !
Chai moto ya choya inapunguza athari za magonjwa ya wazee,kama saratani inayosababishwa na ulawiti na ufiraji !
Pole sana, mara nyingi ngiri maji (busha) huwa haina maumivu, na hakuna sababu ya kufanyiwa upasuaji kama huna maumivu na uvimbe (mpira) ni mdogo tu, aliyekufanyia upasuaji alikusababishia majanga yasiyo ya lazima. Kutokana na maelezo yako nina wasiwasi kuwa ulikuwa huna busha (ngiri maji), vinginenyo ulihudumiwa na mtaalam asiye na ujuzi au uzoefu mkubwa wa kushuhulikia maradhi hayo. Mara nyingi Ngiri maji inahitaji upasuaji mdogo tu ili kuyamwaga maji na kupindua mfuko (tunica vaginalis) unaoruhusu maji kutuama kwenye pumbu. Labda wakati wa upasuaji mtaalamu alijeruhi au kufunga na viungo vingine visivyohusika na kusababisha shida yako unayojihisi. Rudi tena hospitali hata kama sio ile ile kitengo cha upasuaji (surgery) ukachunguzwe zaidi na kufaidika na utaalamu wa madaktari waliobobea na wenye uzoefu. Inshallah utapona. Tofautisha kati ya ngiri maji, ngiri kavu na shida nyingine za sehemu ya korodani kama uvimbe, maambukizi, na kuumia sehemu za mapumbu.
mpe pole mdogo wako, unajua nini!, pumbu ni mfuko mdogo sana kati kati ya mapaja lakini umeshindliliwa viungo vingi sana ndani yake. Kwenye kamfuko haka kuna tissues, korodani mbili, mirija (epididymis) mirefu sana zaidi ya mita 6 urefu na mirija mingine muhimu kwa uzazi. Ndani ya kamfuko haka pia kuna blood vessels, mishipa ya fahamu (nerves) mingi sana, mirija ya majitaka (lymphatic vessels) na kamba (spermatic cords) zinazozishikilia na kuzining'iniza korodani kutoka tumboni. Kazi ya viungo vyote hivi ni kuzipa korodani (testes) afya na mazingira mazuri ya kutengeneza sperms na kuzalisha homoni za kiume (androgens) hasa ile ya testosterone inayomfanya mwanaume awe mwanaume. Hii inapelekea korodani ziwe miongoni mwa viungo nyeti (sensitive) sana kwa mwanaume.
Hivyo basi, kitu chochote kwenye mapumbu kama vile upasuaji (operation), ajali, kupigwa, kukandamiza (kama vile kupanda baiskeli, kuendesha magari ya safari ndefu na madaladala mchana kutwa), joto kali, kuminya, kuvuta, kuvaa nguo zinazobana sana mapumbu, au maambukizi kwenye mapumbu kunaweza kusababisha hasara kubwa kwa mwanaume kwa urahisi.
Tatizo la kijana: Kutokana na wingi wa viungo ndani ya mfuko wa korodani inawezekana daktari kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji huo alikata nerves na blood vessels zinazo-supply korodani husika, hivyo kusababisha kododani iparalize na kukosa damu ya kutosha inayopeleka virutubisho na hewa kwenye korodani husika, hivyo kusababisha korodani isinyae (dystrophy) kwa sababu ya kukatwa kwa mishipa hiyo muhimu. Hii ni kawaida kwa kiungo chochote kama kikiparalize huwa kinasinyaa iwe mkono au mguu.
Kuwa na subira: Mishipa ya damu na fahamu ina tabia ya kujitengeneza upya baada ya muda kupita, korodani inaweza kupata vyanzo vingine vya mishipa kutoka matawi (branches) mengine na kurejea hali yake baadaye.
Habari njema: Hata hiyo korodani moja nzima inaweza kumtosha kwa kazi za uzazi na uzalishaji wa homoni, aitunze vizuri isiudhulike. Hiyo korodani iliyosinyaa inawezekana nayo bado inafanya kazi. Mtu anaweza kubaki na kokwa moja tu bila kupungukiwa zaidi na kitu chochote.
Haya maumivu: Mpeleke hospitali akaripoti hayo maumivu ili apatiwe usaidizi, daktari atamchunguza, kufanyia vipimo (ultra sound), kumpa dawa, kurudia upasuaji au kuiondoa kabisa korodani yenye hitilafu kutokana na atakavyoona inafaa.