Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH) Featured | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH) Featured

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 15, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,605
  Trophy Points: 280
  KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE.jpg
  Tezi Dume (Prostate gland)


  KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE

  Tezi Dume (Prostate gland)

  Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

  Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.


  Kuvimba Tezi Dume (BPH)

  Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.
  Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
  Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.


  BPH husababishwa na nini?

  Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.

  Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

  Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.

  Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika

  damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye

  kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
  Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli: Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.

  Dalili za BPH
  Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote

  Hukojoa mkojo unaokatika katika
  Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  Husita kabla ya kuanza kukojoa
  Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
  Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
  Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
  hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
  Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH

  Madhara ya BPH
  BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na


  Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
  Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
  Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
  Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
  Madhara katika figo au kibofu
  Shinikizo la damu
  Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
  Maambukizi mbalimbali
  Nimonia (Pneumonia)
  Damu kuganda
  Uhanithi
  Vipimo na Uchunguzi

  Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na

  Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake
  kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
  Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.

  Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

  Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
  Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.
  Matibabu

  Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

  Matibabu kwa njia ya dawa
  Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na

  Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
  Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.

  Matibabu kwa njia ya Upasuaji
  Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)
  Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

  Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

  Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).
  Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume
  Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa


  Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo

  Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwaKula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.[Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.
  Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji

  Shida wakati wa kukojoa: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.

  Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. Hta

  hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji
  Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.


  Mdiso au kudindisha (Erections): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupa mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.Kutoa mbegu (Ejaculation):

  Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra

  karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia

  kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

  na Saratani ya Tezi Dume: Hakuna Uhusiano wa moja kwa mojaIngawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kila mwaka.

  UKITAKA DAWA YA KUTIBU HAYA MARADHI YA PROSTATE (TEZI DUME) KWA DAW ZA ASILI ZIPO UKITAKA DAWA NITAFUTE MIMI KWA WAKATI WAKO.

  Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
  Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,605
  Trophy Points: 280
  Prostatitis ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya vimelea vya bakteria katika tezi dume (prostate) kwa wanaume.
  Kuna aina kuu nne za ugonjwa huu wa prostatitis
  1.Maambukizi ya ghafla ya tezi dume (Acute bacterial prostatitis)
  2.Maambukizi sugu ya tezi dume (Chronic bacterial prostatitis)
  3.Chronic prostatitis without infection/Chronic pelvic pain syndrome/chronic non bacterial prostatitis
  4.Asymptomatic inflammatory prostatitis

  Tuangalie aina moja baada ya nyingine za ugonjwa huu

  Maambukizi ya ghafla ya tezi dume (Acute bacterial prostatitis)

  Ni maambukizi ya tezi dume yanayosababishwa na vimelea vya bakteria aina yaE.coli, Klebsiella, Proteus, Pseudomonas, Enterobacter, Staphylococcus aureus, Enterococcus, Serratia na vimelea vinavyosababisha magonjwa ya zinaa. Maambukizi haya yanaweza kufika katika tezi dume moja kwa moja kupitia kwenye damu, au kutoka kwenye kiungo kilicho na maambukizi karibu na tezi dume au huweza kufika kwenye tezi dume kutokana na athari za kufanyiwa kipimo cha kuchukua nyama ya tezi dume kuipeleka maabara kwa uangalizi zaidi au kwa lugha ya kitaalamu tunaita prostate biopsy.

  Dalili na viashiria vya maambukizi ya ghafla ya tezi dume
  Homa
  Kuhisi baridi
  Kutetemeka kutokana na baridi
  Maumivu chini ya mgongo
  Maumivu katika maeneo ya sehemu za siri
  Kupata haja ndogo /kukojoa mara kwa mara
  Kupata haja ndogo wakati wa usiku inayomfanya mtu kushindwa kuivumilia na hivyo kukimbia chooni
  Maumivu/kichomi wakati wa kukojoa/haja ndogo
  Maumivu ya mwili mzima

  Vipimo vya uchunguzi

  Complete blood count Kipimo cha damu kinachoonesha kuongezeka kwa kiwango cha chembechembe nyeupe za damu

  Kipimo cha damu ili kuangalia vimelea vya bakteria kwenye damu (blood cultures). Vimelea vya E-coli vina uwezo wa kupenya kwenye tishu za tezi dume, hivyo dawa za kudhibiti E-coli zinahitaji kutumiwa kamaE-coli ndio watagunduliwa

  Urine for microscope- Kipimo cha kuangalia chembechembe nyeupe za damu na bakteria kwenye mkojo

  Kipimo cha damu kuangalia kiwango cha Prostate Specific Antigen (PSA). Mara nyingi kiwango cha PSA huongezeka lakini ni kwa muda tu.

  Kipimo cha prostate biopsy mara nyingi hakifanywi kutokana na dalili na viashiria vya maambukizi haya kuonyesha kuwa ni maambukizi ghafla ya tezi dume, lakini wakati wa kipimo hiki, chembechembe nyeupe aina ya neutrophils huonekana kwenye tezi dume.

  DRE- Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho

  mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari

  akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kisha kuzungusha zungusha ili

  kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni ngumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini. Katika maambukizi haya ya

  prostatitis,tezi dume huwa limevimba, lenye maumivu linapoguswa, lililokakamaa (firm), lenye jotojoto (warm) na kinga ambazo hazieleweki.

  Kipimo cha damu kuangalia aina ya protini inayojulikana kama C-Reactive protein ambayo huwa huongezeka kiwango chake pale panakuwa na maambukizi.

  Vipimo vya X-ray, Ultrasound na CT Scan vinaweza kutumika kulingana na hali ya mgonjwa itakavyokuwa au kama daktari anahisi chanzo cha maambukizi katika tezi dume kinatokana na maambukizi katika viungo vilivyokaribu na tezi dume au kuangalia viungo vilivyokaribu na tezi dume kama viko katika hali yake ya kawaida au la.

  Matibabu

  Matibabu ya aina hii ya prostatitis yanahusisha matumizi ya dawa aina za antibiotiki ambazo huponya maambukizi haya kwa haraka sana. Aina

  nyingine za dawa hizi huwa haziwezi kupenya hadi ndani ya tezi dume (mfano ciprofloxacilin) hivyo kufanya matibabu kuwa ya shida sana. Dawa za

  antiobiotiki zinazoweza kupenya kwa urahisi katika tezi dume ni dawa jamii ya co-trimoxazole, tetracyclins nk.

  Wagonjwa ambao wana upungufu wa kinga mwilini au wale wenye magonjwa sugu watahitaji kulazwa hospitali ili wawe chini ya uangalizi wa karibu wa daktari.

  Dawa za maumivu na za kulainisha choo pia hutolewa kwa mgonjwa mwenye maumivu au ambaye anapata choo kigumu.

  Mgonjwa ambaye amepata madhara ya maambukizi haya ya ghafla katika tezi dume kama kutoweza kupata haja ndogo/mkojo, atahitaji kuwekewa

  mpira wa kupitisha mkojo sehemu ya chini ya kitovu ili kumpunguzia maumivu na kurahisisha mkojo kutoka nje.

  Mgonjwa ambaye amepata matibabu ya antiobiotiki na hali yake haibadiliki kuwa nzuri atahitaji kufanyiwa kipimo cha Trans-urethral ultrasound ili kuangalia kama ana jipu ndani au la.

  Kinga ya maambukizi haya ni:
  Kuongeza hali ya usafi katika maeneo yako ya siri
  Hakikisha choo (toilet) chako ni kisafi hasa wale wanotumia vyoo vya kukaa
  Kutumia dawa za antiobiotiki kulingana na maelekezo ya daktari kwani dawa nyingine hupunguza kinga yako ya mwili kwa muda na hivyo kusababisha kupata maambukizi ya bakteria.
  Kama chanzo ni ugonjwa wa zinaa, ni vizuri kumueleza mwenza wako ukweli na kwenda hospitali ili kupata ushauri nasaha pamoja na tiba.

  Maambukizi sugu ya tezi dume (Chronic bacterial prostatitis)

  Aina hii ya prostatitis huonekana chini ya silimia 5 ya wagonjwa wote wa maambukizi ya tezi dume ambayo hayasababishwi na tatizo la uvimbe katika tezi dume.Maambukizi sugu ya tezi dume ni nadra sana kutokea na husababishwa na bakteria aina ya E-coli.Maambukizi haya hayana dalili wala viashiria vyovyote isipokuwa tu pale ambapo kutakuwa na kuenea kwa maambukizi kwenye kibofu cha mkojo.

  Vipimo vya uchunguzi

  Kipimo cha kuangalia vimelea vya bakteria katika mkojo (urine for culture and sensitivity)
  Kipimo cha kuangalia vimelea vya bakteria kutoka katika majimaji yanayotoka kwenye tezi dume (Expressed Prostatic Secretions au EPS).Majimaji haya hupatikana wakati wa kufanya kipimo cha DRE ambapo daktari atagandamiza kidole chake kwenye tezi dume ili majimaji haya yatoke.Pia majimaji haya yanaweza kupatikana baada ya daktari kufanya kipimo hiki cha DRE kama hapo awali daktari alishindwa kuyapata haya majimaji.
  Kipimo cha kuangalia kiwango cha PSA kwenye damu kama nilivyoeleza hapo awali.Kawaida kiwango cha PSA huwa juu.
  Semen analysis - Kipimo cha kuangalia shahawa za mwanamume.Katika kipimo hiki chembechembe za usaha (pus cells) zitaonekana kwa wingi kuliko kiwango cha shahawa, chembechembe za shahawa zinazoonekana hapa hazina uwezo (non motile semen) wa kusafiri kwenda sehemu nyingine yoyote.Pia seli aina yaepithelial huonekana hapa.

  Matibabu

  Matumizi ya dawa za antibiotiki kwa muda mrefu (wiki 4-8).
  Matumizi ya dawa aina za alpha blockers husaidia kwa wenye maambukizi sugu ambayo hayaishi
  Maambukizi ya mara kwa mara ya aina hii ya prostatitis huweza kusababishwa na kutoweza kukojoa mkojo wote wakati wa kutoa haja ndogo kutokana na sababu mbalimbali kama uvimbe kwenye tezi dume, neurogenic bladder nk Matatizo ya vijiwe kwenye tezi dume na maumbile yanayohifadhi vimelea vya bakteria pia ni chanzo cha kujirudia kwa maambukizi haya sugu mara kwa mara.
  Maambukizi ya Tezi Dume (Prostatitis) Sehemu ya Kwanza
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  thanx!
   
 4. mshihiri

  mshihiri Senior Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  jazakatulkher
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mkuu thanks!!
   
 6. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mkuu
  Ubarikiwe saana

  Hili tatizo limekuwa KUbwa saana hususani kwa waafrica lakini tatizo
  serekali zetu
  sidhani kama hata zinajua
  kwa west africa ndahni ni tatizo kubwa saana linalowauwa zazee kuanzia mika 48 na kuendelea
  hapa kwetu
  sidhani hata takwimu hakuna kabisa
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,605
  Trophy Points: 280
  Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH)


  Tezi Dume (Prostate gland)

  Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).


  Benign-prostatic-hypertrophy-BPH-.jpg


  Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.

  Kuvimba Tezi Dume (BPH)

  Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.

  Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.

  Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.

  BPH husababishwa na nini?

  Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao

  wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.
  Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

  1. Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.
  2. Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
  3. Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli: Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.

  Dalili za BPH

  Alama.png


  Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote

  1. Hukojoa mkojo unaokatika katika
  2. Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  3. Husita kabla ya kuanza kukojoa
  4. Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
  5. Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
  6. Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
  7. hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  8. Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
  9. Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH

  Madhara ya BPH

  BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na


  1. Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
  2. Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
  3. Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
  4. Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
  5. Madhara katika figo au kibofu
  6. Shinikizo la damu
  7. Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
  8. Maambukizi mbalimbali
  9. Nimonia (Pneumonia)
  10. Damu kuganda
  11. Uhanithi

  Vipimo na Uchunguzi


  uchunguzi.jpg

  Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na

  1. Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
  2. Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.
  3. Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.
  4. Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
  5. Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.

  Matibabu

  Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

  Matibabu kwa njia ya dawa

  Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na

  • Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
  • Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.

  Matibabu kwa njia ya Upasuaji
  Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)


  Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo ni

  • Tiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.
  • Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
  • Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

  Upasuaji mkubwa

  Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume (Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

  Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume
  Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa


  • Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo
  • Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwa
  • Kula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.
  • Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.
  • Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.

  Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji

  • Shida wakati wa kukojoa: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.
  • Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.
  • Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. Hta hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.

  Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji

  Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.

  • Mdiso au kudindisha (Erections): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupa mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.
  • Kutoa mbegu (Ejaculation): Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.
  • Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

  BPH na Saratani ya Tezi Dume: Hakuna Uhusiano wa moja kwa moja

  Ingawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kila mwaka.

  Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH)
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,605
  Trophy Points: 280
  Saratani ya Tezi Dume - Chanzo na Tiba  [​IMG]Tatizo jingine linaloathiri tezi dume ni saratani ya tezi dume. Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa wanaume wa umri mbalimbali duniani. Aidha ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, ni nadra sana kwa saratani hii kuwapata wanaume chini ya miaka 40.
  Nani yupo katika hatari ya kupata saratani ya tezi dume?


  Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:


  • Wanaume wenye asili ya Afrika (weusi) ikilinganishwa na wazungu
  • Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea
  • Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
  • Wanaume wanaokunywa pombe kupindukia
  • Wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi
  • Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali
  • Wanaofanya kazi katika viwanda vya utengenezaji matairi
  • Wachimbaji wa madini hususani aina ya cadmium
  • Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama
  Pamoja na kwamba, tatizo la kukua na kuongezeka kwa tezi dume yaani BPH hutokea kwa wanaume wengi, hali hiyo haiongezi uwezekano/hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
  Dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?

  Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na

  • Kupata shida unapoanza kukojoa
  • Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa
  • Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  • Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  • Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
  • Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
  • Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
  Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu za jirani ya mwili, mgonjwa anaweza kuwa na

  • Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni
  • Uume kushindwa kusimama (uhanithi)
  • Aidha, mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k
  Vipimo gani vitathibitisha kuwa nina saratani ya tezi dume?
  Utambuzi wa saratani ya tezi dume hujumuisha kufahamu historia ya mgonjwa pamoja na familia yake, kufahamu dalili alizo nazo mgonjwa pamoja na kufanya vipimo kadhaa. Vipimo vinavyoweza kufanywa ni pamoja na

  • Digital rectal exam: Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.
  • Kipimo cha damu kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA): PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati wa BPH, tezi dume inapopata uambukizi (prostitis) , na saratani ya tezi dume.
  DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au BPH. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa.

  • Prostate biopsy: Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua kipande cha nyama (tishu) kutoka tezi dume kwa ajili ya uchunguzi maabara.
  Kipimo kingine huitwa transrectal ultrasound ambacho husaidia kuonesha ukubwa na sura ya tezi dume lilivyo.
  Ili kutambua kama saratani imesambaa sehemu nyingine za mwili vipimo vya CT scan, MRI pamoja na PET navyo vyaweza kufanyika pia.
  Saratani ya tezi dume inatibika?
  Ndiyo! Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika.
  Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi, wakati kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri kumfuatilia mgonjwa kwa ukaribu bila kumfanyia upasuaji au bila kumpatia tiba ya mionzi.
  Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).
  Upasuaji

  Upasuaji hufanyika kwa wagonjwa walio katika hatua za awali za ugonjwa (stage I na stage II) ingawa pia hufanywa kwa baadhi ya wagonjwa walio katika hatua za mwisho za ugonjwa huu yaani stage III na stage IV. Upasuaji unaofanywa ni ule wa kuondoa tezi dume pamoja na baadhi ya tishu zinazozunguka tezi hiyo.
  Tiba ya Mionzi

  Hii ni aina ya tiba inayotumia mionzi kuua seli zenye saratani. Tiba ya mionzi hutumika kutibu saratani ya tezi dume ambayo haijasambaa kwenye sehemu nyingine za mwili. Aidha inaweza pia kutumika kuua masalia ya tishu zenye saratani mara baada ya kufanyika kwa upasuaji.
  Kwa wagonjwa walio katika hatua ya mwisho ya saratani yaani wale ambao saratani tayari imeshasambaa mwilini, mionzi hutumika kupunguza maumivu makali ya mifupa.
  Madhara anayoweza kupata mgonjwa kutokana na aina hii ya tiba ni pamoja na kushindwa kusimamisha uume au uhanithi, kukosa hamu ya kula, uchovu, ngozi kubabuka, kuharisha na kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
  Tiba ya Homoni

  Hii ni aina ya tiba inayotumia dawa zinazopunguza kiwango au ufanyakazi wa homoni ya testosterone mwilini. Testosterone ni homoni ya kiume inayochochea ukuaji wa tezi dume, hivyo basi matumizi ya dawa hizi husaidia kupunguza ukuaji huu na kusambaa kwa seli za saratani.
  Tiba ya homoni hutolewa kwa wanaume walio katika hatua za mwisho za ugonjwa huu kwa nia ya kupunguza maumivu na kutibu dalili za ugonjwa. Dawa zinazotumika kwa tiba ya aina hii zimegawanyika katika makundi mawili, zile zinazochagiza uzalishaji wa homoni ya luteinizing (luteinizing hormone-releasing hormones, LH-RH) kwa mfano goserelin, nafarelin na leprolide; na zile zinazozuia ufanyaji kazi wa homoni yaandrogen kwa mfano flutamide, bicalutamide na nilutamide.Madhara yanayoweza kusababishwa na utumiaji wa dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, upungufu wa damu, kuongezeka uzito, uhanithi na kukosa hamu ya tendo la ngono, matatizo katika ini na matiti kuwa makubwa.
  Baadhi ya madaktari hutumia upasuaji wa kuondoa korodani kama njia ya kupunguza kiwango cha homoni za kiume mwilini kwa kigezo kwamba kiwango kikubwa cha homoni hizi huzalishwa kwenye korodani. Hata hivyo tiba hii haifanyiki mara kwa mara.
  Baada ya matibabu?

  Baada ya matibabu, mgonjwa wa saratani ya tezi dume hufuatiliwa kwa ukaribu kuhakikisha kuwa saratani haisambai sehemu nyingine za mwili. Ufuatiliaji hujumuisha mgonjwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara pamoja na kupima PSA kwa kipindi cha miezi mitatu mitatu mpaka mwaka mmoja.

  Saratani ya Tezi Dume - Chanzo na Tiba
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,605
  Trophy Points: 280
  MAAMBUKIZI YA TEZI DUME (PROSTATITIS) SEHEMU YA PILI

  Maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria (Chronic non-bacterial prostatitis)

  Kama jina lake linavyoeleza, maambukizi ya aina hii kwenye tezi dume husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo katika vichocheo vya mwili (homoni) na hata matatizo katika mfumo mzima wa neva.Pia kumekuwepo na dhana ya kwamba maambukizi ya aina hii huchangiwa na kuwepo kwa

  maumivu ya kibofu cha mkojo yanayotokana na maambukizi katika kibofu hicho (Cystitis)au hali ya hewa hususan baridi ambayo huongeza maumivu ya tezi dume na hali ya joto ambayo hupunguza maumivu hayo. Baridi pia huchangia kujirudia kwa dalili na viashria vya maambukizi haya.

  Katika utafiti uliofanyika kaskazini mwa nchi ya Finland (nchi ambayo ina majira ya baridi kali sana),umeonyesha ya kuwepo kwa maambukizi ya aina hii yanayoambatana na dalili na viashiria vyake kali sana kuliko sehemu yoyote duniani.
  Maambukizi haya ya tezi dume bila uwepo wa bakteria hutokea kwa wanaume walio katika umri wa miaka 35-45 na inakisiwa kutokea kwa asilimia 90-95 ya maambukizi yote ya tezi dume .

  Kuna aina mbili kuu za maambukizi haya ambazo ni:
  1.Maambukizi haya yanayoambatana na mcharuko (Inflammatory Chronic Prostatitis/Chronic Pelvic Pain Syndrome)
  2.Maambukizi yasiyokuwa na mcharuko (Non-infalmmatory chronic prostatitis, CP/Chronic Pelvic Pain Syndrome au CPPS)


  Nini hasa hutokea wakati wa maambukizi haya?

  Kukosekana kwa udhibiti wa mfumo wa neva mwilini kutokana na kuwepo kumbukumbu za maumivu yoyote (past trauma), maambukizi kwenye tezi dume, mrundikano wa kemikali tofauti tofauti na kuwepo kwa hali ya kuvutika kwa neva za kwenye nyonga husababisha mcharuko (inflammation)

  katika tezi dume unaosababishwa na kutolewa kwa wingi kwa kemikali aina ya substance P(kutoka kwenye msihipa ya neva) ambayo ndio husababishwa kutolewa chembechembe zinazosababisha mcharuko mwili (mast cells) kwa wingi na matokeo yake ni kuathiri tezi dume pamoja na viungo vilivyokaribu yake kama kibofu cha mkojo, mpira wa kupitisha mkojo (urethra),korodani nk.

  Dalili na viashiria vya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
  •Maumivu makali ya kwenye sehemu za siri au kwenye nyonga kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu bila kuwepo kwa maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI)
  •Maumivu haya makali yanaweza kuenea hadi kwenye mgongo kwa chini, kwenye puru (rectum) na kumfanya mgonjwa kushindwa kukaa chini/ kwenye kiti.

  •Maumivu wakati wa kukojoa
  •Maumivu katika jointi za mifupa
  •Maumivu ya misuli (myalgia)
  •Maumivu ya tumbo
  •Uchovu usioelezeka
  •Kichomi kwenye uume/dhakari (constant burning pain in the penis)
  •Maumivu ya mara kwa mara kwenye nyonga, korodani au kwenye puru (rectum) bila uwepo wa maambukizi kwenye kibofu cha mkojo

  •Maumivu wakati wa kutoa shahawa (wakati wa kujamiana)
  •Kukojoa mara kwa mara
  •Maumivu baada ya kutoa shahawa (baada ya kujamiana) ni dalili kubwa ya maambukizi haya
  •Kupungua hamu ya kufanya mapenzi
  •Kushindwa kujamiana vizuri (sexual dysfunction)
  •Kushindwa kusimika/kudisa (jogoo kushindwa kupanda mtungi)- Erectile dysfuction


  Vipimo vya uchunguzi
  Hakuna kipimo maalum cha kuchunguza maambukizi haya ya tezi dume.

  Vipimo vinavyoweza kusaidia katika uchunguzi wa maambukizi haya ni pamoja na
  •kipimo cha kuangalia shahawa (semen analysis)
  •kipimo cha kuangalia wingi wa cytokines kutoka kwenye majimaji ya tezi dume
  •Vipimo vya kuangalia viashiria vya mcharuko(inflammation) kama cytokines,myeloperoxidases na chemokines
  Inflammatory CP/CPPS huambatana na kuwepo kwa seli za usaha (pus cells) kwenye mkojo, shahawa na kwenye majimaji ya tezi dume wakati Non inflammatory CP/CPPS haina seli hizi za usaha kwenye mkojo, shahawa na majimaji ya tezi dume.Kielezo hiki si kigezo cha kutumika kama kipimo cha kuchunguza maambukizi haya.

  Seli za usaha (pus cells) huwa ni chembechembe za damu nyeupe zilizokufa.

  Matibabu ya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
  Maambukizi haya sio rahisi kutibu kwani hakuna tiba maalum inayokubalika na wataalamu wa afya.
  Lengo kuu la matibabu ya maambukizi haya ni kupunguza mvutano unaosababishwa na kuvutika kwa misuli ya nyonga na ya kwenye puru ,

  kupunguza msongo wa mawazo na vichangizi vya msongo huu wa mawazo.
  Miongoni wa matibabu yanaweza kusaidia ni pamoja na:
  •Kujua chanzo cha msongo wa mawazo/wasiwasi(panic disorder) au taharuki na kumsaidia mgonjwa kuepuka vichagizi hivi
  •Ushauri nasaha pamoja na kumhakikishia mgonjwa ya kwamba hali yake itatengemaa
  •Kumuona daktari wa magonjwa ya akili
  •Kufanya mazoezi ya yoga ili kufanya nyoga pamoja na mishipa ya neva ya nyoga na misuli kuwa katika hali tulivu(relaxation)
  •Massage ya tezi dume (Digital prostate massage)
  •Mazoezi ya viungo kwa wale ambao bado hawajafikia hatua ya kupata maumivu makali (Chronic Fatigue Syndrome)

  •Dawa za kupunguza msongo wa mawazo kama antidepressants, benzodiazipines nk.
  •Dawa za antibiotiki na alpha blockers hazijatoa matokeo ya kuridhisha katika uponyaji wa maambukizi haya
  •Tiba ya acupuncture imeonyesha kuwapa unafuu baadhi ya wagonjwa

  Wanaume wenye maambukizi haya ya tezi dume wako kwenye hatari ya kupata tatizo la maumivu makali sana (Chronic fatigue syndrome) na ugonjwa wa Irritable Bowel Syndrome( unaoambatana na maumivu ya tumbo, tumbo kuwa kubwa, kuharisha mara kwa mara au kutopata haja kubwa, msongo wa mawazo, wasiwasi, kuharisha damu na nk).

   
 10. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,740
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Thanks Mkuu!!
   
 11. S

  SHADRACK LUTOBECK Senior Member

  #11
  Mar 9, 2014
  Joined: Sep 29, 2013
  Messages: 141
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Prostate glands(matatzo ya kibofu cha mkojo) imekuwa ikisumbua wanaume wengi sana.Baadhi ya tiba zake ni TIBA YA HOMONI,UPASUAJI N.K.Madhara yanayo mpata mtu kwa upasuaji ni,kupoteza damu nyingisana,mwili kuwa dhaifu kwa mda,kutolewa tezi,kupungua kwa nguvu za kiume,pia husababisha kifo kwa watu walio na presha.Kiukweli unapofanyiwa upasuaji wa tezi unakuwa unapoteza kiungo mhimu katika mwili,maana kazi ya tezi ni kutengeneza majamaji yanayobeba shahawa.je tezi zikitolewa mtu huyo anakuwa na haligani kwa upande wa kizaz???Nina dawa inayotibu matatzo hayo ya tezi,ni dawa nzurisana ya mitishamba kwa aliye na tatyo hili anitafuta kama anaitaji tiba.iwe mkojo unatoka kidogokidogo,mfululizo,hata kama mgonjwa anacatheta miaka mingapi atapona.kama kuna mtu alisha fanyiwa upasuaji na tatzo likajirudia tena mwambie askate tamaa dawa zipo na zinatibu.kwa meng zaid ntafute.0759217720
   
 12. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2014
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Wadau !
  Habari zenyu .
  Kiukweli kiswahili cha kibaolojia hakijawahi kuwa na urafiki nami .
  Sielewi TEZI DUME ni tezi gani .

  Aidha sielewi linahusika kuwepo pande ipi ya mwili wa Binadamu .
  Naomba kuelimishwa.

  ===========================================================


  Chanzo: Mwananchi
   
 13. O

  Omarymbwambo1980 Member

  #13
  Nov 10, 2014
  Joined: Oct 28, 2014
  Messages: 48
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Yap swali zuri
   
 14. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2014
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Wanalazimisha lugha kwa kuipeleka kwa kasi bila utafiti wa kisayansi. What are the etimological origin of these words. nami huwa sipati ladha yake hata kidogo
   
 15. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2014
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,982
  Likes Received: 1,637
  Trophy Points: 280
  Wewe hujui tezi dume? Ni litezi linatokea mkono wa kulia halafu linavimba sana na maumivu makali.

  Tezi jike hutokea mkono wa kushoto, uvimbe huwa mdogo na maumivu kidogo.

  Hayo ndo matezi dume na jike. Usikonsoe.....
   
 16. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2014
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Kiongozi mwanawao , asante kwa elimisho .
  But hujanikidhisha kuelewa.
  Tezi mkono wa kushoto (kama usemavyo)
  Sasa mkono wa kushoto kwapani? Kiwikoni ?
  Kiganjani ?
  Vidoleni ?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2014
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145

  CHUAKACHARA kimsingi una maono kama yangu .
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. p

  princemwachipindi Member

  #18
  Nov 10, 2014
  Joined: Nov 2, 2014
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tezi dume ni aina ya uvimbe katika korodani ya mwanaume
   
 19. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2014
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mushi92

  Mushi92 JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2014
  Joined: Oct 5, 2013
  Messages: 2,765
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  I think it is prosterial gland
   
Loading...