Kuvaa nguo ya ndani ya mpenzi wako

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,390
1,225

Je, unaweza kuvaa nguo ya ndani ya mpenzi wako?soma hii.

nguo ya ndani inayoweza kuvaliwa na watu wa jinsia zote sasa imeanza kuuzwa madukani nchini Marekani.

Hii ni baada ya kampuni moja nchini humo kuanza kutengeza nguo za ndani kwa lengo la kuhakikisha kuwa wapenzi wanaweza kutumia nguo moja bila tatizo lolote.

Kulingana na gazeti la the telegraph,nguo hizo kwa jina Play out zinazotengezwa na kampuni ya Abby Sugar na Sylvie Lardeux pia zinashirikisha suruali fupi zenye rangi ya kung'aa.

nguo hizo zimetengezwa kama za kiume lakini hazina zipu swala linalozifanya kuweza kuvaliwa na jinsia zote,ijapokuwa wengine wanaweza kulalama kwamba haziwapi faraja.

''Tunataka watu wajisike vizuri na wawe wenye raha wakati wanapovalia nguo hizi,lakini sio kuvaa ili kuwafurahisha watu wengine'', alisema bi Sugar ambaye amekuwa na uhusiano na Bi Lardeux kwa kipindi cha miaka mitano iliopita.

Wanasema kuwa waliamua kutengeza nguo hizo kwa kuwa wanaona mtindo wa chupi za wanaume kama zinazofurahisha na kuvutia.

Source:BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/11/141126_chupi_unisex
 

Attachments

Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,799
2,000
Watu wanavaliana bukta,fulana,snickers.....hata kyupi..ni suala la muda tu....
 

suregirl

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
6,077
1,225
Nguo za ndani za mume wangu sivai hata kwa magongo bora unambie tshirt ntavaa boxer!!!! Sivai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom