Kuvaa nguo ya CCM ni dhambi?

Kuvaa nguo ya CCM ni dhambi?

Karume havai,we nani kwenye chama hadi uvae?
 
mkuu nguo za chama huwa navaa ila sijawahi tinga nazo mwanza mjini kwani mimi ninaishi USAGARA kama unaenda busisi.
Embu na we jaribu kuvaa labda wamenionea tu hao watu walionizomea,nimechukia kweli leo

Inaelekea hata katika hali ya kawaida hufanyi utafiti kabla ya kufanya jambo..Ulivaa ukitegemea kusifiwa?
Pole ndio ujue hapa tulipo kila mtu amechoka,Kinachohitajika ni mabadiliko na sio vingine.
 
Awali ya yote niwasalimieni nyote.

Nilikuwa na safari ya kutoka sokoni hapa mwanza mjini na niliitaji kwenda hadi Kilimahewa nikaona nipite Makoroboi ili nipande hiace pale karibu na mataa.

Nimekutana na dhahama na kunyanyapaliwa kusiko na mfano mara niitwe teja,fisadi wengine wananisukuma bila sababu kisa nimevaa tisherti ya Ccm,kosa langu ni lipi hadi kufikia hata wenye hiace wanakataa nisipande gari yao?

Nimepatwa na hasira sana!

Wanakunyanyapaa kwa sababu unaongozwa na bangi kuvaa nguo za uchaguzi pasipo na uchaguzi. Pili unasapoti mafisadi, majangili na wezi wa raslimali za nchi.
 
Back
Top Bottom