Kuumwa kwa wastara; Bongo movie watoa lawama za kutopewa taarifa

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
268,184
1,095,288
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba, amelaumu kitendo cha msaniii mwenzao Wastara Juma kulalamika mitandaoni kuwa anaumwa na kuhitaji msaada, bila kutaarifu uongozi wake ili waweze kumsaidia. .

Akizungumza na EATV Mwakifwamba amesema ingawa wanafahamu kwamba Wastara ni mgonjwa, lakini taarifa za sasa hivi hajazipeleka kwao rasmi, na hivyo wameziona mitandaoni kama wasanii wengine walivyoona. .

Mwakifwamba ameendelea kwa kusema kuwa kitendo hicho si kizuri kwani inaonekana kama wamemtupa kitu ambacho sio kweli, kwani hata alipokuwa na matatizo kwa mara ya kwanza wao ndio walisimama mstari wa mbele kumsaidia, hata kabla mume wake Sajuki hajafariki. .

Licha ya hayo Mwakifwamba amesema wao kama shirikisho wameshaanza utaratibu wa kuweza kusaidia tatizo la Wastara ili aweze kupata matibabu.

Wiki iliyopita Wastara alitoa taarifa mitandaoni kuwa ana hali mbaya kwani mguu wake ambao ulishakatwa unazidi kumsumbua, na kuomba msaada kwa jamii kwa kumchangia chochote ili aweze kupatiwa matibabu. .

Hata hivyo, mapema January 2016 Wastara alitangaza mitandaoni kuwa na Hali mbaya ya mguu wake akisema anahitajika kwenda India na pesa hana, baadhi ya wasanii wenzake baada ya kusikia hilo walianza kuchangishana apate pesa za matibabu lakini usiku wa siku hiyo baadhi ya wasanii wenzake walishangaa Wastara akifunga ndoa na Sadifa iliyotajwa kuwa ya ghafla.

TAFF walikiri kushangaa waliyeambiwa ni mgonjwa anahitaji msaada akifunga ndoa kwa mujibu wa habari zilizochapishwa .
 
Tatizo huyu Dada analialia sana!! Yaani huwa anadhani yeye ndio mtanzania pekee mwenye matatizo hivyo anataka akiinua mdomo tu basi nchi itikisike na ijishughulishe na yeye!! .. Yaani huwa hataki kbs kuikubali hali yake ambayo watu wengi tu wanayo!! Sijui huwa anadhani mungu hampendi hivyo anataka watu wamtetee asiendelee kuonewa ama VP? Hopeless!
 
jini.PNG
 
Hii hali ya maisha ya awamu hii itawatesa sana hawa wadada waliozoea kuishi maisha ya kudanda danda,bado wanafikiria kuishi kwa kuigiza ni suluhisho la maisha yao,someni alama za nyakati,this is another season..
 
Back
Top Bottom