Kuuliza sio ujinga: Nina safari ya DSM, naombeni muongozo wenyeji

OnlineFinancial

Senior Member
Aug 23, 2017
117
96
Baada ya kusomeshwa namba mwaka mzima bila kazi tumeitwa kwenye usaili, na usaili utafanyika hapo dsm kwenye maktaba kuu utumishi wa uma (PSRS)!

Kwanza natarajia kushukia ubungo, pili naomba nielekezwe mambo haya wadau...

1. Je hii sehemu yaani maktaba kuu utumishi wa uma iko eneo gani hapo dsm?

2. Je naweza pata sehemu nzuri ya kulala iliyo karibu na maktaba kuu kwa bajeti ya 10000-15000 (isizidi elfu 20)?

Na hata pasipokua karibu na maktaba kuu basi pasiwe mbali na kituo cha magari au sehemu nnayoweza kutumia boda boda na kufika maktaba kuu au utumishi kwa haraka!

3. Je huu usafiri wa mwendo kasi ukoje? taratibu zake zikoje?

Karibuni kwa mawazo wadau...

MREJESHO:

Nilifanikiwa kufika, nilipata sehemu nzuri ya kulala na nilifanikiwa kuhudhuria usaili na zaidi ya yote nilifanikiwa kuwa kati ya wachache walioitwa kazini!!

Nawashukuruni wote kwa mawazo yenu!
 
Makataba kuu ipo karibu na chuo cha CBE juction ya kuelekea posta...!sehem ya kulala unaweza kutalala maeneo ya hapo ubungo jirani au ukalale magomen mapipa ndio hotel na guest za bajet hizo...na ka utalala ubungo au magomeni usafiri wa mwendo kasi unafika utashuka kituo cha akiba au DIT na nauli ni 650 tu na hufahamu kituo kilipo utaelekezwa na pia magari yanataja vituo ndani...na baada ya hapo kuelekea maktaba utatembea kama mita 200 kutoka kituoni ukiuliza watu hapo sio mbali
 
Manzese unaweza kupata gest hata za 2,000.

Maktaba iko posta, unapanda gari za posta unashukia kituo cha akiba(kilipo chuo cha CBE) kisba unatembea tu kwa miguu kama dakika 3 au 5 unafika.

Ukipanda gati za mwendokasi(kama umelala manzese au kimara au ubungo) unateremka kituo cha DIT kisha unatembea kwa miguu dakika 5 umefika. DIT na CBE ziko pamoja, chuo kimoja kiko nyuma ya kingine.

Maeneo rahisi ya wewe kulala ni manzese au kimara ambapo unaweza kupata gesti hadi za 1500. Elfu 20,000 manzese unapata full contained na mwanamke juu.
 
Makataba kuu ipo karibu na chuo cha CBE juction ya kuelekea posta...!sehem ya kulala unaweza kutalala maeneo ya hapo ubungo jirani au ukalale magomen mapima ndio hotel na guest za bajet hizo...na ka utalala ubungo au magomeni usafiri wa mwendo kasi unafika utashuka kituo cha akiba au DIT na nauli ni 650 tu na hufahamu kituo kilipo utaelekezwa na pia magari yanataja vituo ndani...na baada ya hapo kuelekea maktaba utatembea kama mita 200 kutoka kituoni ukiuliza watu hapo sio mbali
Shukrani kwa mwongozo mkuu
 
Manzese unaweza kupata gest hata za 2,000.

Maktaba iko posta, unapanda gari za posta unashukia kituo cha akiba(kilipo chuo cha CBE) kisba unatembea tu kwa miguu kama dakika 3 au 5 unafika.

Ukipanda gati za mwendokasi(kama umelala manzese au kimara au ubungo) unateremka kituo cha DIT kisha unatembea kwa miguu dakika 5 umefika. DIT na CBE ziko pamoja, chuo kimoja kiko nyuma ya kingine.

Maeneo rahisi ya wewe kulala ni manzese au kimara ambapo unaweza kupata gesti hadi za 1500. Elfu 20,000 manzese unapata full contained na mwanamke juu.
Na magomeni pakoje mdau?? ukilinganisha na kimara...interms of sehem za kulala na ukaribu wa kituo cha mwendo kasi
 
Baada ya kusomeshwa namba mwaka mzima bila kazi tumeitwa kwenye usaili, na usaili utafanyika hapo dsm kwenye maktaba kuu utumishi wa uma (PSRS)!

Kwanza natarajia kushukia ubungo, pili naomba nielekezwe mambo haya wadau...

1. Je hii sehemu yaani maktaba kuu utumishi wa uma iko eneo gani hapo dsm?

2. Je naweza pata sehemu nzuri ya kulala iliyo karibu na maktaba kuu kwa bajeti ya 10000-15000 (isizidi elfu 20)?

Na hata pasipokua karibu na maktaba kuu basi pasiwe mbali na kituo cha magari au sehemu nnayoweza kutumia boda boda na kufika maktaba kuu au utumishi kwa haraka!

3. Je huu usafiri wa mwendo kasi ukoje? taratibu zake zikoje?

Karibuni kwa mawazo wadau...
Maktaba/Utumishi iko alongside Bibi Titi Road, Kutembea kutoka Akiba kunaweza kua Mbali basi shukia Posta kabisa. Advantage ya Kushukia Posta ni kua Kutoka CBE/DIT/Akiba mpaka Posta kuna mahali kuna traffic lights ambako ndipo maktaba penyewe so waweza kuomba msaada hapo kama gari ikisimama kwenye traffic light.

Pa Kulala huko Manzese ulikoelekezwa mbali sana, lala Magomeni ndio karibu, na kama Mfuko unaruhusu basi lala hata kariakoo kwenye hotel. Ukiweza kua jasiri zaidi Nenda chuo CBE kakeshe hata darasani ukikamua, hutokosa pa kulala na pale kutembea ni karibu.

Yote ya yote Za kuambiwa, Changanya na zako....!!!!
 
na kama Mfuko unaruhusu basi lala hata kariakoo kwenye hotel.
Hhahaha vyuma vimekaza mkuu ndio tupo kwenye harakati za kupaka grisi japo inauzwa...

Naona kuna mdau kashauri magomeni mapipa hapo juu, nadhani hii sehemu itanifaa mkuu!!

Shukran kwa mawazo yako!!
 
Maktaba/Utumishi iko alongside Bibi Titi Road, Kutembea kutoka Akiba kunaweza kua Mbali basi shukia Posta kabisa. Advantage ya Kushukia Posta ni kua Kutoka CBE/DIT/Akiba mpaka Posta kuna mahali kuna traffic lights ambako ndipo maktaba penyewe so waweza kuomba msaada hapo kama gari ikisimama kwenye traffic light.

Pa Kulala huko Manzese ulikoelekezwa mbali sana, lala Magomeni ndio karibu, na kama Mfuko unaruhusu basi lala hata kariakoo kwenye hotel. Ukiweza kua jasiri zaidi Nenda chuo CBE kakeshe hata darasani ukikamua, hutokosa pa kulala na pale kutembea ni karibu.

Yote ya yote Za kuambiwa, Changanya na zako....!!!!
hahaha kukesha kusoma hakuiektiwi chief....atagongwa na mbu ashangaee
 
Manzese unaweza kupata gest hata za 2,000.

Maktaba iko posta, unapanda gari za posta unashukia kituo cha akiba(kilipo chuo cha CBE) kisba unatembea tu kwa miguu kama dakika 3 au 5 unafika.

Ukipanda gati za mwendokasi(kama umelala manzese au kimara au ubungo) unateremka kituo cha DIT kisha unatembea kwa miguu dakika 5 umefika. DIT na CBE ziko pamoja, chuo kimoja kiko nyuma ya kingine.

Maeneo rahisi ya wewe kulala ni manzese au kimara ambapo unaweza kupata gesti hadi za 1500. Elfu 20,000 manzese unapata full contained na mwanamke juu.
Manzese ajiandae kuibiwa chochote alichonacho, wakikosa valuable wanabeba hata vyeti.
Lazima kujiandaa psychological
 
Manzese unaweza kupata gest hata za 2,000.

Maktaba iko posta, unapanda gari za posta unashukia kituo cha akiba(kilipo chuo cha CBE) kisba unatembea tu kwa miguu kama dakika 3 au 5 unafika.

Ukipanda gati za mwendokasi(kama umelala manzese au kimara au ubungo) unateremka kituo cha DIT kisha unatembea kwa miguu dakika 5 umefika. DIT na CBE ziko pamoja, chuo kimoja kiko nyuma ya kingine.

Maeneo rahisi ya wewe kulala ni manzese au kimara ambapo unaweza kupata gesti hadi za 1500. Elfu 20,000 manzese unapata full contained na mwanamke juu.
Usilale manzese na mwanamke utaibiwa vyeti vyako vyote original na asubuhi utaamkia Mwananyamala hospitali ushalambishwa unga kupitia kulamba chuchu.
 
kama utakuwa una toka mbali sana na ikiwa utafika usiku, fika sehemu ya kulala wageni wanao wasili hapo ndani ubungo terminal ili kesho ujue uelekeo wako... pia asubuhi kuna huduma ya bafu utanunua maji ya kuswaki, sabuni ya kuogea na kuwa mpya kwa ajiri ya siku yako mpya... pia kama kibajeti kako kadogo una weza kurudi tena hapo siku ingine na kuzungumza na mgambo wa pale ili akupatie usingizi kwa mara ingine tena

NB:
Kama ukiwa msafiri umefika na una tiketi uta hudumiwa na una tiketi ila una taka kusafiri asubuhi sana watakuhudumia pia ktk hilo jumba bila malipo yoyote ila kama ndio magumashi ongea nao kiume walinzi na kuwapa buku ya maji au fegi wakupe hifadhi
 
Usilale manzese na mwanamke utaibiwa vyeti vyako vyote original na asubuhi utaamkia Mwananyamala hospitali ushalambishwa unga kupitia kulamba chuchu.
Hata hiyo hela ya kumpa huyo mwanamke nitaitolea wapi mdau?? na hata ningekua nayo nisingeweza fanya hivyo...
 
Back
Top Bottom