Kuuliza si ujinga,nahitaji kufika sea cliff ila sipajui...

Chukua daladala hadi dar halafu Chukua Taxi umwambie akupeleke unakotaka kwenda,yaani hivyo man!
 
Daaaahhh umenikumbusha mbali sana mkuu viwanje hvyo hatari sana. Mkuu kanyaga mafuta mpaka coco beach halafu muulize mtu yoyote, kutoke coco beach ni karibu mnoo. Ni kilometer 3.4 tu kutokea coco beach. Kanyaga mafuta mkuu ama lile gari umeuza sasa unatumia matatu?
 
Mkuu fuata maelekezo ya uzi namba 6,ukitoka Coco Beach unanyoosha ile barabara inayoelekea Golden Tulip straight to Sea Cliff village,one of the very best place to stay and do expenditure in Dar Es Salaam....go enjoy it!
 
Chukua daladala hadi Mbezi.
Kisha chukua daladala mpaka Mawasiliano(simu 2000).
Hapo panda daladala za kwenda Masaki.
Shuka Masaki kisha tafuta bodaboda au taxi au uber.
Nyongeza asishuke mwisho,kuna kituo kinaitwa bakhresa kipo karibu anaweza tembea hata kwa mguu
 
Panda daladala la Temeke. Teremkia Sugar Ray. Panda daladala la Buguruni. Unganisha na daladala la Muhimbili. Ukifika faya teremka. Panda mwendo kasi hadi Shekilango. Teremka Shekilango. Chukua daladala la shule ya uhuru kupitia Kigogo. Teremkia kwa mkuu wa mkoa. Panda daladala la Msadani. Teremkia ubalozi wa Marekani. Chukua pikipiki hadi kilima nyege. Teremka hapo chukua bajaj ya buku hadi police officers mess. Geukia kulia utaiona kwa mbali kidogo. Then chukua uber ni buku 2 tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom