Biashara ya ATM

Powell Gonzalez

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
622
1,276
Kuuliza si ujinga, walisema wahenga. Nami kwa kuheshimu methali hii naomba kuuliza bila uoga, hivi hizi ATM ni mtu yeyote mwenye mtaji anaweza kufungua ATM ? kama Kuna mtaalam basi afafanue na gharama kwa undani kidogo, kwenu wakuu.
 
hivi hizi ATM ni mtu yeyote mwenye mtaji anaweza kufungua ATM ?
NDIO, inawezekana.

ATM ni kama tu machine za kuhesabia fedha au zile machine za TRA zinazotoa Risit za EFD, mtu yeyote mwenye mtaji anaweza kuifanya hio Biashara.

Hata hapa Tanzania kuna baadhi ya Kampuni zinafanya hio Biashara ya kuuza Machine za ATM.
 
Kuuliza si ujinga, walisema wahenga. Nami kwa kuheshimu methali hii naomba kuuliza bila uoga, hivi hizi ATM ni mtu yeyote mwenye mtaji anaweza kufungua ATM ? kama Kuna mtaalam basi afafanue na gharama kwa undani kidogo, kwenu wakuu.
Lazima uwe na Benki Fungua kwanza benki kama wallivyopendekeza wadau
 
Nimegundua kuwa ATM inaweza kumilikiwa na mtu yeyote, kwa kuinunua mashine hiyo ambayo huuzwa kwa kati ya USD 2100 na kuendelea kisha utaweka pesa kuanzia USD 500 baada ya kufuata taratibu zote za kibiashara. Faida yake hupatikana kwa kulipwa kiasi Fulani Cha pesa kwa Kila transaction kama mmiliki was mashine hiyo.
 
Back
Top Bottom