Wazazi wangu wananipenda kuliko Watoto wengine

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
659
1,074
Tumsifu yesu kristu.Bwana Asifiwe.

Tumezaliwa Watoto wengi kidogo ni zaidi ya 10. Hii imeanza nikiwa Bado mdogo inshort sijajielewa kivile majirani na hata wanazengo walikuwa wakiyasema haya bayana kuwa waguse Watoto wote lakini usiguze huyo kijana! Nilichukulia utani wa watu tu lakini kadiri nilivyo zidi kujielewa zaidi nikawa nagundua hili.

Wazazi wetu sio kwamba hawapendi Watoto wengine lahasha wanawapenda sana na hakuna hata mmoja anaye sema Mimi wazazi hawanipendi.

Nimeligundua hili baada ya ndg zangu kaka na dada wakubwa wakiwa na jambo Kwa mzee au mama lazima waniambie live kuwa mwambie mzee kuhusu hili na hili maana wewe ndiwe anakuelewa na kukusikia sana kiuchumi Mimi Bado najitafta japo uhakika wa kula na kunywa bia2-5 sio wa kuuliza daily kama nikiamaua ila wakubwa zagu wapo vizuri sana wamejenga na Wana usafiri wote.

Hii imenifanya niwaze na kujisikia vibaya kidogo kuwa kama wamefikia hatua hii ya Mimi kunitumia kufikisha ujumbe Kwa mzee Ili Hali wao ndo wakubwa naona hii ni shida Kwa mtazamo wangu!

Mzee au mama anaweza kuja kwangu akakaa hata siku2-3 (na nimepanga tu) bila kwenda Kwa dada yng mkubwa na kaka ambae tupo sehemu Moja na anakupa angalizo usiwaambie akitaka kuondoka ndo anawaambia
Nilikuwa hapa Kwa Fulani na Leo narudi. Naona hii si sawa!

Pia mzee hawezi maliza siku 1 bila kunipigia simu! Issue yoyote ya familia lazima aniambie Mimi niwaambie !!

Ni vitu vya kawaida sana navyo fanya Kwa wazazi

Mfano kukiwa na shida ya mhimu hata ya kawaida Huwa naenda chap sana kuwaona
Zawadi Watoto wote Huwa wanawapa lkn Mimi nikinunua hata shati litavaliwa Kila sehem ya mhimu nk Hadi ndg walalamike Hilo shati mzee unatutia aibu wee hubadirishi.

Kuna kitu nilikipinga Mimi mzee alikuwa amekubali hapo kabula ila nilipopinga nayeye akabadiri GIA angani na kukataa pia.

Ni mengi lakini Sasa nahitaji niwaambie wazazi ila nashindwa nianze vipi pengine wanaweza kuhisi sipendi wawe wanakuja kwangu.

Kama Kuna mtu nae ilimtokea anipe mawili matatu ya kuwaeleza Ili nijitoe kwenye hili sio kwamba siwapendi no nawapenda sana hata wife alishaniambia mara kibao kuwa wazee wanakupenda sana kuliko wengine.
Mwisho.

Mvua zinanyesha Sasa tupandeni miti ya matunda Kwa faida ya Afya zetu si Kila kitu ununue tu sio poa.

Ahsante
 
Attachments

  • IMG_20231107_091321_613.jpg
    IMG_20231107_091321_613.jpg
    96.1 KB · Views: 3
Tulia hivyo hivyo, wewe bado ni mtoto haujui mengi.

Siku zote wazazi wanawajua vizuri watoto wote, hivyo wao wanajua kwa nini wawekeze kwako na si kwa wengine.

Usithubutu kuhoji wazazi wala kuomba ushauri kwa ndugu yako mwingine juu ya hali hiyo.

Acha niishie hapo, nijitulize na uzee wangu.
 
Si useme wewe ni last born.

Me mwanzako lastborn na uzee wa mama angu nikionana nae atanishawishi anitumbue hadi chunusi zilizo iva namuuliza hivi huoni watu wataona nadeka.

Anasema ndevu zinakudanganya sana hizo wewe bado mtoto😒😒
 
Tumsifu yesu kristu.Bwana Asifiwe.

Tumezaliwa Watoto wengi kidogo ni zaidi ya 10. Hii imeanza nikiwa Bado mdogo inshort sijajielewa kivile majirani na hata wanazengo walikuwa wakiyasema haya bayana kuwa waguse Watoto wote lakini usiguze huyo kijana! Nilichukulia utani wa watu tu lakini kadiri nilivyo zidi kujielewa zaidi nikawa nagundua hili.

Wazazi wetu sio kwamba hawapendi Watoto wengine lahasha wanawapenda sana na hakuna hata mmoja anaye sema Mimi wazazi hawanipendi.

Nimeligundua hili baada ya ndg zangu kaka na dada wakubwa wakiwa na jambo Kwa mzee au mama lazima waniambie live kuwa mwambie mzee kuhusu hili na hili maana wewe ndiwe anakuelewa na kukusikia sana kiuchumi Mimi Bado najitafta japo uhakika wa kula na kunywa bia2-5 sio wa kuuliza daily kama nikiamaua ila wakubwa zagu wapo vizuri sana wamejenga na Wana usafiri wote.

Hii imenifanya niwaze na kujisikia vibaya kidogo kuwa kama wamefikia hatua hii ya Mimi kunitumia kufikisha ujumbe Kwa mzee Ili Hali wao ndo wakubwa naona hii ni shida Kwa mtazamo wangu!

Mzee au mama anaweza kuja kwangu akakaa hata siku2-3 (na nimepanga tu) bila kwenda Kwa dada yng mkubwa na kaka ambae tupo sehemu Moja na anakupa angalizo usiwaambie akitaka kuondoka ndo anawaambia
Nilikuwa hapa Kwa Fulani na Leo narudi. Naona hii si sawa!

Pia mzee hawezi maliza siku 1 bila kunipigia simu! Issue yoyote ya familia lazima aniambie Mimi niwaambie !!

Ni vitu vya kawaida sana navyo fanya Kwa wazazi

Mfano kukiwa na shida ya mhimu hata ya kawaida Huwa naenda chap sana kuwaona
Zawadi Watoto wote Huwa wanawapa lkn Mimi nikinunua hata shati litavaliwa Kila sehem ya mhimu nk Hadi ndg walalamike Hilo shati mzee unatutia aibu wee hubadirishi.

Kuna kitu nilikipinga Mimi mzee alikuwa amekubali hapo kabula ila nilipopinga nayeye akabadiri GIA angani na kukataa pia.

Ni mengi lakini Sasa nahitaji niwaambie wazazi ila nashindwa nianze vipi pengine wanaweza kuhisi sipendi wawe wanakuja kwangu.

Kama Kuna mtu nae ilimtokea anipe mawili matatu ya kuwaeleza Ili nijitoe kwenye hili sio kwamba siwapendi no nawapenda sana hata wife alishaniambia mara kibao kuwa wazee wanakupenda sana kuliko wengine.
Mwisho.

Mvua zinanyesha Sasa tupandeni miti ya matunda Kwa faida ya Afya zetu si Kila kitu ununue tu sio poa.

Ahsante.

View attachment 2832016
Usijipe kazi ya kuwachagulia watu wengine (hata wazazi wako) watu wa kuwapenda au kuwachukia. Ni kazi ngumu na hutoiweza! Wewe tenda yaliyo mema na timiza wajibu wako kwa kila mtu (wazazi wako na ndugu zako) na hilo la kukupenda ama kukuchukia waachie wenyewe. Jiulize hata wewe mwenyewe, kuna mtu mwingine anakupangia wa kumpenda na umpende vipi?
 
Back
Top Bottom