Kuukata mzizi wa fitna: Napendekeza uchaguzi moja na muhula moja wa miaka 10 wa Urais Tanzania

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Habari zenu familia ya JF.

Naenda kwenye hoja hapo juu. Kumekuwa na mipango ya kutaka kubadilisha mfumo wa uchaguzi na mihula ya Urais humu nchini.

Mi binafsi napendekeza na kama ningekuwa na uwezo, ningependa kuona uchaguzi ukifanyika Mara moja tu ndani ya miaka kumi. Yaani Rais akishapita atahudumu miaka 10 na baada ya hapo aondoke. Uchaguzi wa bunge hivyohivyo sambamba na Urais ila sio lazima Mbunge aondoke baada ya miaka 10.

Akipenda aendelee kwani sio vizuri wanasiasa wote wawe wapya ktk nchi ktk mhula fulani. Sababu kuu za mapendekezo yangu zipo mbili. Mosi kupunguza gharama zisizo za lazima kufanya uchaguzi na pili kupunguza damu imwagikayo na roho zipoteazo kipindi matokeo ya uchaguzi yanapotangazwa na kubishaniwa.
 
Kolimba alisema haya maneno hivi yuko wapi sasa hivi vile nyie anzeni tu kujitekenya unadhani humo ndani ya chama chenu mwapendwa sana eeh
 
Back
Top Bottom