Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Status
Not open for further replies.

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,489
Reaction score
18,379
Bismillahir Rahmanir Rahim
Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Kwa mara nyingine tena mbingu zitafunguka na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa nasi.

Fungueni nyoyo zenu kwani Ramadhani na baraka zake zote pamoja na uzuri wake unawadia.

Ramadhani sawa na huko nyuma kwa usahali na bila ria lakini kwa kina na wingi wa maana inawadia ili nyoyo zetu zilizochoka zinufaike na chemichemi yake na rehma za Mwenyezi Mungu zitushukie.

Mwezi wa Ramadhani unatoa bishara njema kwa Watu wote kuhusu kufunguliwa milango ya peponi na kuanza karamu ya Mwenyezi Mungu.

Itakiwa ni mda muafaka wa kumrudia Mola ili aikumbuke Nchi yetu na kutujaza hekima ya kujitambua kuwa wote ni ndugu wa baba mmoja Allah.

Inshaallah!.
 
Bismillahir Rahmanir Rahim
Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Kwa mara nyingine tena mbingu zitafunguka na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa nasi.

Fungueni nyoyo zenu kwani Ramadhani na baraka zake zote pamoja na uzuri wake unawadia.

Ramadhani sawa na huko nyuma kwa usahali na bila ria lakini kwa kina na wingi wa maana inawadia ili nyoyo zetu zilizochoka zinufaike na chemichemi yake na rehma za Mwenyezi Mungu zitushukie.

Mwezi wa Ramadhani unatoa bishara njema kwa Watu wote kuhusu kufunguliwa milango ya peponi na kuanza karamu ya Mwenyezi Mungu.

Nafuu tutapumua kwenye kitimoto, uteja,uchangu, ujambazi huko kote ni vuluvulu.
 
huu mwezi huwa naupenda sana, vurugu zote mjini zinakuwa likizo
 
vunja jungu wapi?

Vunja Jungu ni fikra chafu...

‘vunja jungu' humaanisha kwamba Ramadhani ni jambo zito, la dhiki, usumbufu na lenye kunyima raha na utamu wa maisha. Kiasi kwamba huona wakomoe kwa mara ya mwisho ndani ya hatima ya mwezi wa Shaaban.Hii ni fikra chafu, hatari na haina nafasi katika Uislamu wala katika hali halisi.
Uislamu umetuwekea wazi kwamba sisi ni waja wa Muumba na hatuna letu ila kunyenyekea Kwake tu.

Na pia Uislamu ni dini inayowafikiana na maumbile ya mwanadamu, na kamwe haikuja kumtia uzito wala dhiki mwanadamu katika kushibisha mahitaji yake ya kibaologia kama chakula, maji nk.

Na wala haikuja kumpa mashaka katika kushibisha mahitajio yake ya kighariza kama ya kiibada, kuendeleza kizazi, ambayo ndani yake hupatikana matamanio ya kijinsia nk.

Bali Uislamu umekuja kupanga utaratibu mwanana na mzuri kwa wanaadamu ili wakidhi mahitajio yao yote bila ya pingamizi.
 
Ahsante kwa kutukumbusha...

Tuingieni katika Ramadhani kwa furaha, moyo mkunjufu na uchamungu.

Na tuiage Shaaban kwa furaha na tusijiingize katika maovu.

Tukivuruga ndani ya Shaaban ndio kuvuruga ndani ya Ramadhani.
 
Vunja Jungu ni fikra chafu...

‘vunja jungu’ humaanisha kwamba Ramadhani ni jambo zito, la dhiki, usumbufu na lenye kunyima raha na utamu wa maisha. Kiasi kwamba huona wakomoe kwa mara ya mwisho ndani ya hatima ya mwezi wa Shaaban.Hii ni fikra chafu, hatari na haina nafasi katika Uislamu wala katika hali halisi.
Uislamu umetuwekea wazi kwamba sisi ni waja wa Muumba na hatuna letu ila kunyenyekea Kwake tu.

Na pia Uislamu ni dini inayowafikiana na maumbile ya mwanadamu, na kamwe haikuja kumtia uzito wala dhiki mwanadamu katika kushibisha mahitaji yake ya kibaologia kama chakula, maji nk.

Na wala haikuja kumpa mashaka katika kushibisha mahitajio yake ya kighariza kama ya kiibada, kuendeleza kizazi, ambayo ndani yake hupatikana matamanio ya kijinsia nk.

Bali Uislamu umekuja kupanga utaratibu mwanana na mzuri kwa wanaadamu ili wakidhi mahitajio yao yote bila ya pingamizi.

kiwatengu big up asante kwa ufafanuzi
 
Last edited by a moderator:
kiwatengu
Waleykum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,
Nashukuru sana kwa ukumbusho wako huu ndug yangu,hakika ukumbusho huwafaa wale wenye kuamin,
Insha allah tuingie kwenye Ramadhan Kareem kwa twaah na unyenyekevu wa hali ya juu...
 
Last edited by a moderator:
Bismillahir Rahmanir Rahim
Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Kwa mara nyingine tena mbingu zitafunguka na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa nasi.

Fungueni nyoyo zenu kwani Ramadhani na baraka zake zote pamoja na uzuri wake unawadia.

Ramadhani sawa na huko nyuma kwa usahali na bila ria lakini kwa kina na wingi wa maana inawadia ili nyoyo zetu zilizochoka zinufaike na chemichemi yake na rehma za Mwenyezi Mungu zitushukie.

Mwezi wa Ramadhani unatoa bishara njema kwa Watu wote kuhusu kufunguliwa milango ya peponi na kuanza karamu ya Mwenyezi Mungu.

Inshaallah!
 
kiwatengu
Waleykum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,
Nashukuru sana kwa ukumbusho wako huu ndug yangu,hakika ukumbusho huwafaa wale wenye kuamin,
Insha allah tuingie kwenye Ramadhan Kareem kwa twaah na unyenyekevu wa hali ya juu...

Inshaallah
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom