Tatizo la kutokwa na damu kwenye fizi: Fahamu chanzo na namna ya kutatua tatizo hili

Usisahau na juice ya ubuyu, ina vitamin c nyingi.
Mkuu ushauri wa King'asti na wegine ni mzuri sana, lakini kuna ushauri mwingine wa ziada ambao watu wengi awajawahi kuhusikia nao ni kama ufuatao: Ukiamka asubuhi kabla ujapiga mswaki, mimina a tablespoon full ya mafuta ya kupikia aina ya ALIZETI (siyo KORIE) weka mdomoni sukutua kwa robo saa hivi mpaka povu jeupe litokee - tema. Baadae unaweza kupiga mswaki kama kawaida - usipuuzie inasaidia sana nilijifunza dawa hii nilipokuwa nje - wenzetu wanajua sana alternative medicine. Yote tisa lakini ni vema kumuona daktari wa meno vile vile.
 
Habari ndugu zangu? Poleni kwa majukumu. Meno yangu kadha huwa yanatoa damu, japo si nyingi, kwenye fizi, hususani wakati niyafyonza. Huwa hayaumi. Hali hii imedumu kwa muda mrefu, bila ya mimi kutojua suluhu. Je hali hiyo inasababishwa na nini? Na nini suluhu yake? Karibu utoe mchango wako.
 
Vidonge vya vitamin c vinatosha. vinginevyo tumia machungwa au malimao au ndimu. kama tatizo litaendelea waone madaktari wa meno.

Ahsante! Ila hayo machungwa au malimao nayatumia vipi? Je nayakamua juisi au nayatafuna pamoja na maganda yake? Kuuliza si ujinga!
 
Ahsante! Ila hayo machungwa au malimao nayatumia vipi? Je nayakamua juisi au nayatafuna pamoja na maganda yake? Kuuliza si ujinga!
Kamua na kunywa juice yake . Sababu ya kukushauri kutumia juice ya machungwa au vidonge vya vitamin c ni kwamba tunadhani una ugonjwa wa ukosefu wa vitamin c uitwao scurvy
 
pamoja na kutumia matunda/vinywaji/vyakula vyenye vitamini C, jenga utaratibu wa kwenda kusafishwa kinywa kwa dentist walau mara 2 kwa mwaka. Zingatia pia kupiga mswaki kila baada ya mlo, hasa usiku! Tumia dawa sahihi ya meno.
 
Habari ndugu zangu? Poleni kwa majukumu. Meno yangu kadha huwa yanatoa damu, japo si nyingi, kwenye fizi, hususani wakati niyafyonza. Huwa hayaumi. Hali hii imedumu kwa muda mrefu, bila ya mimi kutojua suluhu. Je hali hiyo inasababishwa na nini? Na nini suluhu yake? Karibu utoe mchango wako.

Naomba utuorodheshee kwa majina dawa unazotumia on a regular basis (kwa mfano dawa za blood pressure, kisukari, gauti, nk.)
 
Periodontal diseases hizo, specifically chronic periodontitis, gingivitis. Huo ni ugonjwa hatari sana kwa meno yako na hivi punde utaona yakianza kulegea na kuanza kung'ooka bila hata kutoboka wala kuuma. Muone daktari wa meno aliekaribu mapema iwezekanavyo kabla haujapata ukibogoyo. Kama uko dsm njoo muhimbili nitakusaidia.
 
Ahsante Access Deniad. Hali hii imedumu miaka mingi, nimeichukulia poa tu, ila nimeanza kupata wasiwasi kwa kuwa naamini kuna mapungufu katika mwili. Nitamwona daktari wa meno. Ningekuja MNH, ila nipo mbali sana.
 
Poa nenda ukamuone na wala usihangaike na vit c au malimao, hiyo hali husababishwa na mabaki ya chakula yaliyokaa mda mrefu na kufanya kitu kinaitwa calculus or calcified plaque. Na husababisha kulika kwa mfupa unaoshikilia jino na kuliacha jino likielea na kung'ooka. Nenda ukachunguzwe na kupewa matibabu sahihi toka kwa dentist. Angalizo ni kwamba unatakiwa uonane na dentist(dds) hao wngn wanafanya wrong diagnosis finally wakaishia na wrong treatment.
 
Access Dinied Naomba nikuona hapao muhimbili unisaidie ninatatizo la meno kweli nimetoa mengi na karibu yataisha. Aksante
 
Naombeni msaada wenu katika hili. Nina miaka sasa natokwa damu kwenye fizi. Sijui tatizo ni nini. Ninapokuwa napiga mswaki tatizo huwa kubwa zaidi, lakini nimegundua hata niamkapo asubuhi hujikuta kinywa kina damu. Nimezunguka haspitali mbalimbali na kwanza nilipewa vidonge vya vitamini C, haikusaidia, Muhimbili wakanisafisha (kwangua) meno, bado haikusaidia. Nikaambiwa nipige mswaki mara tatu au zaidi....kila baada ya mlo, nalitimiza kwa ukamilifu bila mafanikio. Aidha, nikaambiwa nihakikishe napiga mswaki kwa sio chini ya dakika mbili na ikiwezekana hata kuongeza dawa mara mbili...natimiza, na tatizo liko palepale. Wajuzi nisaidieni, what next should I do?
 
Back
Top Bottom