Msaada maumivu ya meno/fizi

Ngurukia

JF-Expert Member
Feb 25, 2023
1,481
6,221
Hali zenu waungwana,

Kwa atakaekuwa na ujuzi/msaada juu ya maumivu ya meno na fizi nitamshukuru mno.

Ninasumbuliwa na meno kuuma hasa ya upande mmoja wa kinywa (kulia), yanavuta mpaka kwenye fizi na midomo ya chini.

Hakuna jino lililoharibika ila maumivu yake yanakithiri hasa yakiguswa na ubaridi.

Nilienda hospitali ya meno jibu nilililopewa ni kuwa mafizi yangu yamelika kupelekea kuwa na meno sensitive.

Nimekuwa natumia sensodyne sensitive na sensodyne rapid relief lakini huwa napeta ahueni kwa siku chache tu kisha huanza tena.

Nimejaribu kufuatilia chakula ninachokula kuona kuwa kama kuna trigger lakini sijaona cha mno ninachokula kuweza kuleta athari/maumivu.

kwa yeyote mwenye tiba nitashukuru mno.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
 
Rudi tena hospitali. Mbali na kutumia hizo sensodyne, kuna matibabu ya kufanya coating ya hayo meno kwa dawa(material) inayoitwa composite utafanyiwa, ambayo ndio itakuwa mwarobaini ya hiyo sensitivity.
 
Kuna mti mmoja unaitwa "mkuyu"
fanya uutafute na
hakikisha unapakaa utomvu wake kwenye jino linalokuuma.
jino likiacha kuuma nitafute nikupe maelekezo mengine.
 
Back
Top Bottom