JamboJema
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 1,143
- 209
Naombeni msaada wenu katika hili. Nina miaka sasa natokwa damu kwenye fizi. Sijui tatizo ni nini. Ninapokuwa napiga mswaki tatizo huwa kubwa zaidi, lakini nimegundua hata niamkapo asubuhi hujikuta kinywa kina damu. Nimezunguka haspitali mbalimbali na kwanza nilipewa vidonge vya vitamini C, haikusaidia, Muhimbili wakanisafisha (kwangua) meno, bado haikusaidia. Nikaambiwa nipige mswaki mara tatu au zaidi....kila baada ya mlo, nalitimiza kwa ukamilifu bila mafanikio. Aidha, nikaambiwa nihakikishe napiga mswaki kwa sio chini ya dakika mbili na ikiwezekana hata kuongeza dawa mara mbili...natimiza, na tatizo liko palepale. Wajuzi nisaidieni, what next should I do?