Jinsi ya kutibu meno kirahisi meno yanayouma na kutoa damu.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
Miaka ya nyuma nikiwa chuo nilikuwa nasumbuliwa na meno kuuma hasa baada ya kutafuna nyama. Pia nilkuwa nikila mua tu naona damu zinatoka kwenye vizi. Muda mwingine hata nimechill maumivu ya kiaina yanakuja. Nilitumia mouthwash bila ya mafanikio.

Sasa ndio classmate wangu mmoja akanipatia trick moja ilionisaidia. Aliniambia nunua dawa ya colgate na uwe unatumia kupigia mswaki ila hakikisha baada ya kupiga mswaki usiwe unasukutua bali unaacha dawa inabaki kinywani siku nzima. Unaweza ukasutua ila baada ya hapo chukua dawa yako kolgate hata kidoleni kikiwa kisafi alafu uisambaze kwenye meno vizuri bila kusukutua dawa ile kwa siku.

Sikumbuki muda sahihi wa maumivu kuisha ila naamini after a month ni kama meno yangu yalitulia kabisa. Kwakweli njia hii ilinisaidia hadi leo sina shida yoyote ya maumivu ya meno wala kutoka damu ila hakikisha dawa inakuwa ni COLGATE kwa maana iko more medicated kuliko whitedent.
Niliendelea kufanya hivi ikawa sasa ni tabia.
edbe0d2d6b620f651adfd570c34c97e3.jpg


Shida ikiwa kali sana kimbia kwa dentist.
 
Nikitoka kupiga mswaki kitu chochote nitakachokula lazima kiwe kichungu kwasababu ya ile harufu ya dawa.... Sipati picha uiweke dawa yenyewe, halafu kwa siku nzima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom