Tatizo la kutokwa na damu kwenye fizi: Fahamu chanzo na namna ya kutatua tatizo hili

Kuna muda iwe asubuhi mchana kuna wakati nikitema mate najikuta natema damu nyepesi...inasababishwa na nini hiyo hali?
 
pia na mimi nina tatizo hilohilo mara nyingi kilila mkate au chungwa naacha alama ya damu kwenye kipanda kilicho baki hari hiyo si ipendi inatoweka nikipiga mswaki mara 2 au 3 kwa siku naomba maelezo yakutosha kabla sija muona Dr
 
Fisi za mdomo zina cavity and plague. Nunua mouth wash usukutue baada ya kuswaki pia muone dentist
Mkuu...sky Eclat,vp mouthwash unaitumiaje,make Kuna siku doctor aliniderect kutumia dawa hyo kwa siku 6,but baada ya kutumia kwa siku tatu fizi zangu zikaanza kuwa na mabaka meusi ikabidi nizame Google, ndo kukuta wanaseme you have to mix with distilled water.
 
Mara nyingi kuvimba au kutokwa na damu kwenye fizi huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya kinywa na meno ambayo husababishwa na kutofanya vizuri usafi wa meno kwa usahihi au maambukizi ya bakteria ambao usababisha utando mgumu kwenye meno.

Utando huu hauwezi kutolewa kwa kupiga mswaki bali kwa kutumia vifaa maalumu na wataalamu wa meno. Pamoja na maambukizi au kutofanya usafi pia kutokwa na damu kwenye fizi usababishwa na magonjwa ya damu, kupiga mswaki kwa nguvu, ukosefu wa vitamini C na K.

FANYA YAFUATAYO KUJITIBU MWENYEWE

Tumia mswaki laini kusafisha meno kila siku na hakikisha unabadili mswaki kila baada ya miezi mitatu.

Usichokonoe meno mara kwa mara, ila tu baada ya kula ili kuondoa mabaki ya chakula. Matatizo ya hormoni asa kwa wajawazito.

Epuka uvutaji wa sigara na tumbaku ambao huchangia matatizo mengi ya kinywa na meno.

Epuka matumizi ya dawa za Aspirin ispokuwa kwa maelekezo maalumu na wataalamu wa afya

Kula mboga za majani, matunda na vyakula vyenye vitamini C na K kwa wingi

Tatizo likizidi onana na madaktari wa meno na kinywa walau mara moja kwa miezi 6 kinywa kwa ushauri zaidi kuhusu dawa za kusukutua na kuua maambukizi, kuziba meno yaliyotoboka au kung'oa meno yaliyoharibika.
 
Naombeni mnisaidie fidhi zangu zinatoa damu mara kwa mara nimejaribu kubadili dawa za meno ninazotumia lakin wapi naombeni msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
Una upungufu wa Vitamin C mwilini mwako kunywa kwa wingi Machungwa, na pia utengeneze Juisi ya limao kwa maji ya moto uwe unakunywa asubuhi na usiku kila siku utapona. Dawa ya pili tumia njia hii hapa itaweza kukusaidia.

Jinsi ya kuzuia fizi kutoka damu!

Majani ya mpera:

Mpera wengi tunaufahamu tulizungumza tena na tena kwa upana kuhusu mti huu na matumizi yake ki lishe na tiba leo tena nakukumbusha jinsi ya kuzuia fizi kutoa damu kwa kutumia majani machanga ya mpera,

Kwanza kabisa utayachukua hayo majani na kuyaosha vizuri kwa maji safi na salama pili.

Utachukua kias hicho kidogo cha hayo majani na uyatafune pole pole kwa dakika km kumi hivi utafanya hivi mara 3 au 2 kwa siku 7 , 11, hadi 14 kutokana na uzito wa tatizo baina ya mtu na mtu tatizo litaisha kabisa.

Ukiwa na Shida yoyote ile
 
Sasa jamani kuna hii mdomo kutoa harufu kama unatumika kwa haja kubwa, jamani! Hebu tusaidiane,kuna watu huwezi hata kumsikiliza akikunong'oneza.
 
Back
Top Bottom