Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Katika hali inayoashiria hali si shwari kwa upande wa ccm, wameingiza wapiga kura feki katika kata ya vijibweni.
Taarifa za ndani kabisa zimedokeza kuwa kiasi cha kadi 1700 zimetengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia kuongeza kura.
Baada ya kupatikana taarifa hizo, Chadema iliwafahamisha mawakala na kuwaelekeza namna ya kuzitambua. Katika zoezi la kutambua kadi feki, watu kumi na tano wamekamatwa wakiwa na kadi feki katika vituo vya Nunge, Shule ya msingi Vijibweni na Ofisi ya mtendaji Vijibweni.
Baada ya kunaswa kwa watu hao kumi na tano inaonekana wameambizana na sasa hakuna kadi feki inayopatikana.
Tunaendelea kufuatilia matukio na tutawajuza kadri yanavyopatikana.